Nani kama Sugu?

Nani kama Sugu?

Mkuu tafuta na ngoma moja ameitoa 2010 kama sikosei, inaitwa Hold on. Isikilize kwa makini.

Hold on aliitowa akiwa unyamwezini ni full hisia yani ukiwa mbeba box ukisikiliza nyimbo ile lazima ichote hisia zako.
 
Sitaki. Kwani vipi? Hiyo nyimbo ilikuwa kwenye albamu gani? Kuflash back ni kupotea? Wewe ndio unapotea hapa.

Album ya mwisho ya Sugu ilikuwa lini?

Tutafute base ya mabishano yetu. Tusibishane ki phmbi phmbi tu.
 
Hii inanikumnbusha mbali sana..!!

Enzi hizo gheto kumetapakaa magazeti ya wasanii mbalimbali kama kina 2pac Shakur, Westlife na B.I.G hapa Bongo ndo kina Sugu, Dola Soul wanasumbua balaa, Ukienda gheto na mtoto akute room lilmepambwa namna hiyo we ndo mjanja wa mjini. Mitoko ilikuwa ni Mashati ya drafti na tisheti nyeupe chini ukivalia suruali yenye mifuko pembeni usawa wa magoti almaarufu kama Timbarland yaani we utaogopwa mtaa mzima. Siku ukitoka na Visuruali flani hivi vinaitwa vinyelamumo, almaarufu kama Bigmark, pembeni unakiredio chako cha mkononi almaarufu kama Walkman, Yaani we unasumbua mji balaaa..!!

Enzi hizo kina Prof J ndo wanachipukia na Hard brothers crew yao, Sugu anasumbua Nchi na kitu chake "Anamiaka chini ya kumi na nane," kila Barbershop utakayoingia ni Sugu Sugu Sugu enzi hizo akijiita Mr II. Kina LadyJd ndo wananusanusa, pembeni hivi kina King Creiz GK wanasogea kwa mbaaaaali daaah...!!! Kweli tunatoka mbali sana.

Mr II alikuwaga na mpaka kesho anakisauti flani hivi cha ki-hip hop haswa.. Anakitetemeshi flani hivi wakati wa kutema mashairi. Yaani enzi hizo mziki ulikuwa ni hizi tunazoita leo zilipendwa na hip-hop kwa pembeni wakisindikizwa na Taarab kidogo. Na hiphop ilikua ni hiphop haswa, siyo kama leo wasanii wa hip-hop wanavisha pua zao vidani na kutoga masikio huku wakisindikizia na kusuka nywele na full make up..!!! Huu mziki ulikuwa wa wagumu kweli kweli.. Akaja jamaa mmoja hivi ambaye alishawishiwa na hawahawa kina Sugu kurudi kufanya mziki Bongo na si kung'ang'ania USA, huyu jamaa alikuwa akiitwa Cool James mtoto wa Dandu (Rip) ndiye mwasisi wa hizi tuzo za KTMA alitoa wazo la kuanzishwa kwa tuzo hizo (siyo KTMA) sijui aliziitaje. Bahati mbaya kabla hazijaanza rasmi akafa kwa Ajali.

Kipindi hicho mziki wa kunakili miziki ya wakongwe ilikuwa ikitamba haswa na style hii ndiyo iliyomtoa Mr Paul, aliimba wimbo wa Zuwena wa Mariajan Rajab. Hivi wakuu Matola, Deo Carlione na Ruttashobolwa mlikuwa wapi enzi hizo, Mnakumbuka nini?

Halafu kwa kumbukumbu zenu mnaweza kukumbuka mwanamziki wa kwanza kuanza mziki wa kuimbaimba (Siyo Kughani mashairi) almaarufu kama Bongofleva? Note, ninaposema Bongofleva R&B weka pembeni.. Tukumbushane wadau..

BACK TANGANYIKA

James Dandu alikuwa anaishi Sweden, siyo Marekani na yeye ndio mtoa wazo wa Tuzo za kili nashangaa mpaka leo wanashindwa hata kumuenzi na Dandu award hii nchi nyoko majitu mabinafsi sana.

Kuhusu swali lako la nani kaanza Bongo fleva hujaliweka vizuri, maana kama ni kurap kaanza Salehe el Jably na na kama ni kikundi cha kurap kilichoanza ni Kwanza Unity a.k.a KU Crew. Na kama ni Bongo Fleva kwa maana halisi ni Sugu.
 
Last edited by a moderator:
Hold on aliitowa akiwa unyamwezini ni full hisia yani ukiwa mbeba box ukisikiliza nyimbo ile lazima ichote hisia zako.
Ile ngoma Sugu aliimba kwa hisia sana, Inaonekana kuna mshikaji alimwimbia maana ni kama anampa mausia fulani hivi.
 
James Dandu alikuwa anaishi Sweden, siyo Marekani na yeye ndio mtoa wazo wa Tuzo za kili nashangaa mpaka leo wanashindwa hata kumuenzi na Dandu award hii nchi nyoko majitu mabinafsi sana.

Kuhusu swali lako la nani kaanza Bongo fleva hujaliweka vizuri, maana kama ni kurap kaanza Salehe el Jably na na kama ni kikundi cha kurap kilichoanza ni Kwanza Unity a.k.a KU Crew. Na kama ni Bongo Fleva kwa maana halisi ni Sugu.

Nota bene: Just for ur information Muda mchache kuanzia sasa usiku huu, nitakuwa na Sugu Mbezi beach.
 
Hahahahahah umenikumbusha mbali sana mkuu, kipindi hicho matoz wananyoa panki za kina Shaba Ranks, Raba kubwa sana zakuitwa lakuchumpa unakuta ina tiki kubwa ya Nike.... Jeans za fubu, hapa unanoga ukipiga full jeans na koti lake... Ukionekana umebeba cd mkononi watoto wakali wote wako... Cd kipindi hicho uwe na ndugu kiwanja au ukaazime ushuani... Nakumbuka braza angu alikuwa anakanyaga mguu mpaka msasani kwa kina Roby kuazima tu cd za wakali wa mbele.

Hahahahahah Matumbo,

Nadhani unazungumzia yale Masahani makubwa ukilishika vizuri linatosha kujupepea kwa joto kali la Dar..!!! Yaani enzi hizo ilikuwa full burudani...!!

BACK TANGANYIKA
 
eAkumbukwe Sosikeneth Ambakisye Sos B.

Kwa single moja? Anyway kukurukarakara zako zitakuponza iliturusha kwa kipindi kile, hawa wote walishindwa kutoa Album ila sugu kila mwaka alimudu kushuka na album moja nzito muziki wa getto.
 
Hold on aliitowa akiwa unyamwezini ni full hisia yani ukiwa mbeba box ukisikiliza nyimbo ile lazima ichote hisia zako.
Matola nimekuomba nyimbo kadhaa za huyu gwiji, but sijapata mrejesho Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom