Nani kapita hapa?

Nani kapita hapa?

Miaka ya 2001 mkuu ila Gowele ni katibu wa waziri now kipindi ninasoma alikuwa mwalimu wa kiswahili
Kumbe huyu jamaa kaula, alikuwa jamaa tozi sana hahaaa
 
Ndanda boys daah kitambo sana nilipangwa hapo kusoma PCB, physics alikua anafundisha mmarekani Joseph chow (r.i.p) , chemistry Ka madam flani Ka kijapan (sikuwah kuelewa kitu kwenye pindi lake) afu bios mtu mzima ominde aka cha pombe
Niliona ndoto zangu ndo zinaishia hapo, likizo fupi nilibeba kila kilicho changu nikasepa home nikawaambia kuliko kurudi bora nikae mtaani
Mkuu na madevu ndo alikuwa lab technician wenu bila shaka hahaaa
 
Nimepita hapo 2009-2011 tulipokelewa na Lulukila (Master) Bweni nililofikia Shelaton, Room Wanyama ( The Animals)

ktk vitu ninavyovikumbuka shule nzima ilikuwa na wanafunzi 976 kombi 9 ila walimu 13, yaan kila mwalim akipewa darasa lake hawaenei maana Form5&6 jumla ilikuwa madarasa 18.

Sowani (master) ndo tulimuacha, naskia sasa marehemu, Maticha vituko kama, Mpemba, Mkandawile, kuna mmoja tulikuwa tumamwita Niaje,

Daah Ndanda kuna mengi saanaa sita pasahau pale!!!
Mkuu hiyo shelaton ina historia yake, kuna miaka palitokea mafuriko, mabwen ya wasichana yakasombwa ndo zikajengwa Mpya, ndo maana zilikuwa tofauti na za mkoloni hahaaaa
 
Hongereni wana Ndanda, siku hizi kusini kuchere. Ni masaa 5 tu DSM to Lindi then 40min to Ndanda. Karibuni sana.
 
Peruree ruleee ndanda boys peru peru ndanda boys.
2006-2008 kilimanjaro-mawenzi room 21 tuliita horizon deep.

Tv room mv bukoba .
Lecture room ukumbi wa Manchester.
Head Master ..Mzee Mmoja ivi (mlemavu flani)
Makamu nadhani alikuwa Sowone.
Makota G (rip)
Halafu kuna Muhidin (Mjahidina)
Kulikuwa na kimadam flani ivi kilikuwa laboratory, achana na mama tesha.

Yumba Kabobo,alikuwa mtata balaa
Yumba Kaboboooo !!!
 
Hongereni wana Ndanda, siku hizi kusini kuchere. Ni masaa 5 tu DSM to Lindi then 40min to Ndanda. Karibuni sana.
Haa aaa aa
Unatembeaje kwa dk 40 toka Lindi hadi Ndanda?
 
Mademu zetu walikuwa masas girls Na mtwara girls
 
NDABO
Intake ya 2011-2013 (Nilihama )
Maji matamu sana ya ndanda.Hata maji ya bombani baridi matamu sana.
Juu kule kwenye bookshop ukipanda juu kuna sanamu ya wakatoliki

Kulikuwa na saa ya sa kumi na mbili inagonga very loud.Upande wa pili huku kanisa la wakatoliki linatazamana na shule,

Kulikuwa kuna nyoka sana story ilikuwa wakoloni walileta nyoka kumaliza issue ya panya.

Kulikuwa na mhindi flani ana duka la jumla mitaa ya madeko nadhani.Afu kuna branch ya NMB pale stand karibia na barabara ya kwenda shule,unapita hospital ndio unaenda shule.Mitaa tulivu sana,wa Benedicyino waliweza.

Nakumbuka kuna time hela ilizingua nikaenda kuuza flash yangu kule madeko (kulikuwa na kisehemu cha ku burn cd[emoji13])

Kuna kipindi pumbu erosion bweni la kule juu mlimani ilikuwa kipengele sana.
 
Back
Top Bottom