Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Vyakula vilivyohesabika ni Najisi wakati wa Torati,(Walawi11:1-43)
Katika Agano Jipya vimetakaswa kwa Neno la Kristo.
Ndiyo maana Yesu anasema,
(Marko7:16-19)-Kimuungiacho mtu hakimtii Unajisi bali kimtokacho.Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Tena maandiko yanasema,
(Matendo10:11-16)-Alivyovitakasa Mungu usiviite Najisi.
(Warumi14:14)-Hakuna kilicho Najisi kwa asili.
Kinachotakiwa ni kushukuru kabla ya kula,(1Timo4:2-5)

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Katika dini ya Ukristo, maandiko matakatifu ya Biblia yanapinga ulaji wa nguruwe kwa sababu inachukuliwa kuwa ni mnyama najisi.

Hii inapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11:7-8 ambapo inasema " Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. .Hamtakula nyama yao, wala hamgusi mizoga yao. Hao ni najisi kwenu."

Pia, kuna vifungu vingine vinavyopinga ulaji wa nguruwe kama vile Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:8 ambacho kinapinga ulaji wa nguruwe, na Matendo ya Mitume 15:28-29 ambayo yanahimiza waumini kuepuka kula nyama iliyotolewa kwa sanamu na damu.

Kwa upande wa Uislamu, Quran inapinga ulaji wa nguruwe na inachukuliwa kuwa ni haramu kwa Waislamu. Kifungu cha Quran Surat al-Baqarah 2:173 kinakataza ulaji wa nguruwe pamoja na nyama ya wanyama waliochinjwa kwa njia ya kuchinjwa bila kumtaja Mungu, damu, nyama ya wanyama wanaouliwa kwa sababu ya miungu, na wanyama waliofariki kwa kifo cha asili. Kwa hivyo, Waislamu wanachukulia ulaji wa nguruwe kama jambo la kinyume na mafundisho ya dini yao.


NB: TUJADILI KWA AYA NA VIFUNGO MBALIMBALI ZA VITABU MBALIMBALI VYA DINI NGOJERA HAZITAKIWI.

View attachment 2613342
Kasome Wakurya 6:6 :6 Inasema tule vinono ili tuwe na nguvu ya kumpiga adui na Mnyama anayefaa zaidi ni yule Nguruwe safi na Ugali au ndizi. Usiishie kusoma Waarabu na Wazungu tu Soma Waafrika 10 mstari wa saba Mvivu wa kufikiri na kuwinda atakula vilivyo dhaifu na visivyo na mafuta.
Mpuuzi fulani wewe. Mungu yupo Afrika kabla hajaja Mzungu wala Mwaarabu ndiyo maana neno Mungu walilikuta wakaweka kwenye vitabu vyao. Halafu kumbuka tu hizo Amri Walipewa Walawi na Waarabu wewe Mtu Mweusi huna dhambi .
 
Back
Top Bottom