Nani kati ya Makamu wa Rais na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi analidanganya taifa kuhusu suala la Samaki?

Kwani ni lazima kila jambo litatuliwe Kwa matamko kwanza? Mambo mangapi serikali inayadhibiti bila raia kujua?
Mimi sijasema "kila jambo litatuliwe kwa matamko kwanza", inawezekana ni akili yako ndiyo inayokutuma wewe kufikiri hivyo.
 
Kikubwa hapa ni tatizo la mawasialiano ndani ya Serikali! ingawa taarifa ya Makamu wa Rais zina uhakika zaidi kwakuwa anazungukwa na taarifak kutoka vyanzo vingi vya usalama
Hapana.

Tatizo siyo "mawasiliano" pekee, bali tatizo kubwa ni kushindwa kufanya kazi kwa taasisi zilizopewa majukumu kulinda afya za wananchi na mambo mengine.

Hayo mambo mengine ya "ubepari" n.k., huo ni mjadala mwingine, ambao nao ningekataa hiyo dhana yako unayoiamini wewe.
 
Sawa, mjadala mzuri ni pamoja na ww kutoa mawazo mbadala!

Makamu wa Rais anavyanzo vingi vya taarifa kuliko waziri! Nalo unabisha??

Nilizungumza athari za taarifa aliyotoa Vice katika uchumi na impact yake!

Mifano niliyotoa, juu ya silaha na mapebari, ni kuonesha tu namna gani nchi zilizoendelea ziko makini na mambo ya uchumi na fedha
 
Duh, mkuu 'Lubengera', unajitahidi sana kunivuta kwenye mjadala huu mwingine, ambao kwa kweli kwa sasa sina muda mzuri nao.

Lakini itoshe tu kukueleza kwamba, biashara ya silaha, ni biashara, kama zilivyo biashara nyingine zote. Mnunuzi anayo hiari ya kununua anapohitaji. Hili linalojadiliwa hapa ni tofauti kabisa. Hii siyo biashara iliyohalalishwa na sheria yoyote, in fact inakiuka sheria zote katika nchi yoyote ile.

Sasa kama bado hunielewi kwa maelezo haya mafupi ambayo nimeyafanya 'direct', hapo utakuwa na jambo jingine kabisa.
Kuhusu hilo la Makamo wa Rais kuwa na "vyanzo vingi", unataka nibishe kitu gani katika hilo! Kuwa na vyanzo vingi vya kupata habari, ndiyo iwe sababu ya kuficha jambo la hatari kwa raia? Ili habari ziwe za chini chini na biashara inayokiuka sheria zote iendelee?
Haya ni mawazo ya namna gani haya!
 
Itoshe kusema, Vice hakupaswa kutoa taarifa hii hadharan maana ina impact kubwa hata katika biashara na uchumi
 
Itoshe kusema, Vice hakupaswa kutoa taarifa hii hadharan maana ina impact kubwa hata katika biashara na uchumi
Kwa hiyo ulitaka sisi raia, tuendelee kufa kwa kansa?🥺
 
Itoshe kusema, Vice hakupaswa kutoa taarifa hii hadharan maana ina impact kubwa hata katika biashara na uchumi
Naona hukuelewa nilichoeleza hapo juu, pamoja na wewe kunipa 'like' kama ulivyofanya!

Basi shikilia msimamo wako huo, pamoja na kwamba ni msimamo potofu.
 
Sasa hicho ndicho kilichofanyika. Angewasiliana na Wizara husika Naibu Waziri asingeongea aliyoongea.
 
Naibu Waziri ni mtaalam wa hayo mambo. Hajajibu kisiasa. VP ndiye aliyekurupuka
 
Tume tena! Ya watu wangapi? Ifanye kazi siku ngapi? Iwajibike kw nani? Ilipwe kiasi gani? Na je ikikuta Mh. Mpango ndo mwongo isemeje? Kwamba Makamu wa Rais wa Tz ni muongo! Au huyo mwingine!?...nk. Ni hivi, ktk nchi yenye viongozi wenye kujiheshim na wawajibikaji, mambo haya hayahitaji tume. Hakuna kutofautiana hadharani-mkubwa na mdogo, kwamba ikiwa mdogo ana la kumpinga bosi wake, anajiuzulu kwanza halafu akaelezee kwa nni baadae. Ona ss, watu wanajadili uwezekano wa Mak. Rais kuwa aliropoka au muongo na hawezi tena kutoa ufafanuzi wa aliyosema! Haya matume yanakula muda, yanakula kodi zetu bure, yanaongeza tozo na hayana tija... fatilia uone
 
Ndani ya polisi Kuna vitengo vingi mpaka vya udukuaji na ushushushu. Yeye kama mkubwa ameshindwa Nini kutuma kikosi kazi Cha kupeleleza na kudhibiti?
Inawezekana ni kweli, unadhani wataacha kutumia hizo kemikali kwa matamko ya majukwaani?
Je Nchi za nje wakapiga marufuku ya usafirishaji minofu kutoka Tanzania, watanzania wakakosa ajira, huyu atalisha familia zao?
Matamko yake Yana athari mbaya zaidi kuliko faida.

Eti "transparency" Dunia Yako hii!
Corporate espionage isingekuwepo kama pangekuwa na transparency

Kwa hiyo wewe unaacha kula Samaki, unajiona unachukua tahadhari, hongera.
Ila nikwambie tu, hakuna kilicho na usalama kuanzia kuku unaokula, nyama ya buchani, mayai, njegele unazokula, maharage, sembe n.k Mimi nipo kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji miaka 8. Kuna matumizi ya madawa ambayo hayafuati masharti. Labda uwe unajilimia chakula chako. Take care mwerevu!
 
Sasa hicho ndicho kilichofanyika. Angewasiliana na Wizara husika Naibu Waziri asingeongea aliyoongea.
Hapana.
'Protocol' haipo hivyo. Katika ziara hiyo Wizara husika ilitakiwa iwe imejiandaa, na katika msafara huo kuwe na mwakilishi, kama siyo huyo huyo Naibu waziri mwenyewe kuwepo hapo na kumfahamisha Makamu usahihi wa mambo kama upo.Makamu wa rais hawajibiki kwenda kutafuta taarifa wizarani. Wewe vipi bhwanah!
 
Tume. Tume ya nini, kuchunguza uzembe?

Jambo sahihi hapa ni kuwajibisha watendaji wasiotimiza wajibu wa kazi zao, basi.
 
Ukisema kila ziara ya VP viongozi wa Wizara mbalimbali wawepo kwenye msafara hakuna kazi itakuwa inafanyika na kutakuwa na matumizi mabaya sana ya fedha. Katika mikoa mingi karibu kila sekta ipo sasa Manaibu Waziri wangapi waongozane na VP ili kutoa maelezo? Yeye VP hata kama aliambiwa au kusikia kuhusu hiyo issue HAKUPASWA kuitangazia dunia kuwa kuna kitu hiki kinafanyika bila kupata ufafanuzi wa kina kutoka sekta husika. Mara nyingi kama uko sehemu ukapata taarifa za namna hiyo na huna uhakika huwa tunasema serikali imelichukua na italifanyia kazi then anatuma wasaidizi wake au PM kuhoji suala hilo kwenye Wizara husika.
 
Kwa hiyo una maana ya kwamba hao walioko mikoani hawajui yaliyoko woizarani?
Kama walikuwepo, mbona hawakutoa ufafanuzi ili Makamo asiongelee jambo ambalo hana ukweli nalo?

Bado unajisikia wizara yako haitimizi wajibu wake? Unatetea kitu gani hapa kama siyo uozo!
 
Nakwambia tena hivi, VP alikurupuka. Hayo mambo hayaendi hivyo. Kama VP alisikia hayo maneno huko mitaani na hakuuliza watu walioko kwenye sekta iwe huko Halmashauri au Wizarani akayaongea hadharani amekurupuka. Period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…