Nani kati ya Makamu wa Rais na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi analidanganya taifa kuhusu suala la Samaki?

Nani kati ya Makamu wa Rais na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi analidanganya taifa kuhusu suala la Samaki?

Nakwambia tena hivi, VP alikurupuka. Hayo mambo hayaendi hivyo. Kama VP alisikia hayo maneno huko mitaani na hakuuliza watu walioko kwenye sekta iwe huko Halmashauri au Wizarani akayaongea hadharani amekurupuka. Period.
Hayo unayoyasema hapa hayaongezi thamani yoyote katika swala la uozo uliopo huko huko wizarani.
Kama yanasemwa na watu huko mitaani hadi yakamfikia Makamo wa Rais, na wizara haina habari nayo unataka watu waelewe kitu gani kuhusu hiyo wizara!

Watu wawe wanasubiri hadi kiongozi mkuu ayasikie kwa wananchi ndipo wizara iyatolee ufafanuzi?
 
My dear Kalamu bado hujaelewa madhara ya mtu wa "kawaida" kutangaza maneno ya mitaani na "VP" kufanya the same.
 
Kama wananchi walikuwa nayo huko mitaani ni kwa nini hawakupeleka hayo malalamiko kwenye Wizara husika mpaka wamsubiri VP ndiyo waseme hayo unayoita wewe malalamiko? Ina maana VP asingeenda huko hicho kitu kisingezungumzwa?? Huo ni unafiki na kutaka kuchafua watu!!!
 
My dear Kalamu bado hujaelewa madhara ya mtu wa "kawaida" kutangaza maneno ya mitaani na "VP" kufanya the same.
Duh!
Naona unataka tushindane tu hapa kwa kitu kilicho dhahiri kabisa.

Philip Mpango, hata ukiweka umakamo mbali, hadhi yake tu inatosha kukwambia kuwa siyo mtu anayeweza kuropoka tu ili asikike!
Hivi huwezi kutumia akili kidogo na kuona hali halisi?

Hili siyo jambo la mtu kuropoka tu, ni jambo linaloleta sintofahamu katika jamii!

Sasa wewe niambie, wizara yote ile isiwe hata imesikia hao watu wa kawaida wakizungumza maneno ya ajabu ajabu kama haya; ila VP ndiye mtu wa kusikia tu huko mitaani na kuamua kulizungumzia kirahisirahisi tu!

Kwani kazi ya wizara ni nini hasa? Huko hakuna watu walioajiriwa kufuatilia mambo ya wizara hadi kwa wananchi?
Una maana wizara haikuwahi kusikia haya maneno yakisemwa huko mitaani; au iliyasikia ikaona ni upuuzi tu na ikaghairi hata kufuatilia kwake tu kwa nini pawe na uvumi wa kipumbavu namna ile?

Hata sijui kama wewe ni mwajiriwa huko wizarani au hata huko serikalini. Kama wewe ni mwajiriwa, sina shaka kwamba mahali pako pa kazi hupatilii maanani sana. Na hili ndilo tatizo lililoenea kwa watumishi wote wa umma.
 
Kama wananchi walikuwa nayo huko mitaani ni kwa nini hawakupeleka hayo malalamiko kwenye Wizara husika mpaka wamsubiri VP ndiyo waseme hayo unayoita wewe malalamiko? Ina maana VP asingeenda huko hicho kitu kisingezungumzwa?? Huo ni unafiki na kutaka kuchafua watu!!!
Unaona sasa; nimekwishasema katika jibu langu nililoweka sasa hivi kwamba hizi ndio tabia za watumishi wetu serikalini.
Hawa watu wapo kazini kufanya kazi gani hasa? Mnamfanyia nani kazi au nyinyi ni mabosi tu mnasubiri mletewe matatizo?

Attitude kama hizi ndani ya serikali hazitatufikisha popote!
 
Na kama haitoshi, inakuwaje Makamu akatoa taarifa nzito kiasi kile bila kuwasilianan na wizara husika katika serikali yake?
Jibu uliandika since day one nashangaa kwa nini tunabishana sasa hivi. Ngoja nikuache.
 
Kama wananchi walikuwa nayo huko mitaani ni kwa nini hawakupeleka hayo malalamiko kwenye Wizara husika mpaka wamsubiri VP ndiyo waseme hayo unayoita wewe malalamiko? Ina maana VP asingeenda huko hicho kitu kisingezungumzwa?? Huo ni unafiki na kutaka kuchafua watu!!!
Hivi unajua ni kwanini, hayo malalamiko yalipelekwa kwa VP?

Ni kwa kuwa walijua wakizifikisha wizarani, ni kama vile wamepeleka Kesi ya ngedere kwa nyani!

What do you expect?🥺
 
Hivi unajua ni kwanini, hayo malalamiko yalipelekwa kwa VP?

Ni kwa kuwa walijua wakizifikisha wizarani, ni kama vile wamepeleka Kesi ya ngedere kwa nyani!

What do you expect?🥺
Siyo kweli
 
Jibu uliandika since day one nashangaa kwa nini tunabishana sasa hivi. Ngoja nikuache.
Naona huelewi chochote.

Unataka kujionyesha kuwa mtu usiye na uelewa wa jambo unalosoma; kama mtu mwenye elimu pungufu.

Hilo ulilonukuu hapo siyo jibu la kutwisha Makamo jukumu la kuwasiliana na wizara. Wizara ndiyo yenye jukumu la kumpa usahihi wa jambo husika.
Wewe huoni kuwa ni swali linaloulizwa,; au hujui tofauti kati ya swali na jibu?
 
Siitaji ukweli au uongo ninachohitaji ni hivi sili tena samaki labda wale wanaletwa manyara
 
Jiulize kwanza: Philipo yeye kalitoa wapi jambo hilo, maana hawezi kuamka tu usingizini na kwenda kulitamka alivyofanya.

Na kama haitoshi, inakuwaje Makamu akatoa taarifa nzito kiasi kile bila kuwasilianan na wizara husika katika serikali yake?
Hili ni jambo la kushangaza sana.

Sasa turudi kwenye hiyo dawa yenyewe: Haiwezi ikawa chloroform. Chloroform haitumiki kuhifadhi maiti.

Hata hivyo, chloroform ni dhaifu zaidi katika kusababisha saratani. Miaka siyo mingi sana iliyopita, chlorofrm hiyo hiyo ilikuwa ikitumika kuchanganyia dawa za binaadam, na imetumika kwa muda mrefu kiasi, na hapakuwa na wingi wa hiyo saratani. Ndiyo, baadae inadhaniwa kuwa na madhara hayo, lakini siyo kwa kiasi hicho cha kutia woga.

Bila shaka dawa inayozungumziwa hapa itakuwa Formaldehyde (Formalin), ambayo ndiyo hasa kazi yake ni kuhifadhi maiti, na haijawahi hata mara moja kutumika kwa matumizi ya binaadam kwa kumeza au kupaka. Inajulikana zaidi kuwa na madhara ya kusababisha saratani.

Na mwisho: Haya yanayotokea ni dalili wazi kabisa za taasisi zetu kutofanya kazi ipasavyo. Haiwezekani kabisa watu wawe wanatumia vitu hatarishi kwa maisha ya binaadam kirahisi namna hii bila kujulikana.
Hii ni dalili moja wapo ya nchi yetu kuwa 'Banana Republic' kwelikweli.

Ndiyo maana gonjwa hatarishi kabisa linaingia nchini, halafu wanasiasa ndio wanakuwa mstari wa mbele kupinga uwepo wa gonjwa lenyewe!

Si ajabu hata 'Panya Road' wanatamba!

Sijui ni jambo lipi tunaloweza kujivunia kama nchi kwa sasa. Labda mafanikio ya CCM kuwalaza akili waTanzania. Katika hili hakuna mfano unaotufikia sisi.
Mkuu hili la kuhifadhia samaki lina ukweli na Dr Mpango hakukurupuka. Hata nchi zenye scandal za uchakachuaji kama Indonesia hili tatizo limewahi kutokea.

''Scandals have broken in both the 2005 Indonesia food scare and 2007 Vietnam food scare regarding the addition of formaldehyde to foods to extend shelf life. In 2011, after a four-year absence, Indonesian authorities found foods with formaldehyde being sold in markets in a number of regions across the country.[89] In August 2011, at least at two Carrefour supermarkets, the Central Jakarta Livestock and Fishery Sub-Department found cendol containing 10 parts per million of formaldehyde''
 
Ukweli watazania hatujalivalia njuga suala hilo, Hivi makamo wa raid alikurupuka kusema hayo? lazima alikuwa informed, mind you kabala teuzi huko nyuma aliishi mwanza sana !!
Je mtakumbuka ya Tume ya Bunge na taarifa ya Mto mara?
ukweli tunataka taarifa sahihi maana kuna shida na hofu na kuchanganyikiwa kwa wanunuzi na wauzaji halali
 
Back
Top Bottom