Pinda ni kweli anafaa, tatizo kubwa yeye ni mtaalamu wa kujibu maswali bungeni, kuchair vikao, kuzima vuguvugu kitaalamu bila mtu kujua kama kuna suluhisho au hakuna, mfano Richmond, leo hii nikikuuliza hata yale mambo serikali iliyoambiwa ishughulikie we unajua yamefikia wapi? Pia ni mwadilifu
Inapokuja utendaje wa nje wa hayo niliyotaja hapo jamaa hayupo kabisa, mpole mno. Lowasa ni mfuatiliaji mzuri ila tatizo lake uadilifu.
Dr Magufuli yeye yuko kote kote, uadilifu, kupangua hoja kwa mifano na live data, na pia ni mfuatiliaji wa mambo. Pia hana jazba ya kugombeza watu hadharani. Tukitaka TZ isonge mbele kote kote, DR MAGUFU ni mtu sahihi kwa sasa. Ila kama tunataka mtu wa kupangua hoja na kujibu maswali vizuri bungeni Pinda ni mtu sahihi kwa sasa.
Ila ujue wananchi wanataka zaidi ya hapo, kuona miradi ya serikali ikikamilika kwa wakati na pia kua na value of maney. Magufuli alipokua Ujenzi, ardi, Uvuvi na Mifugo, amefanya kazi zinazoonekana.
Hii kazi mpeni Dr Magufuli, CCM itarudi 2015 bila kuweka mabango kama mwaka huu. Ila wakimwachia huyu aliyetoka theni wajiandae kuongeza budget ya mabango ya kampeni mara 4 zaidi ifikapo 2015.
Dr Magufuli sii mchezo, Jamaa alikua anafuatilia barabara, ujenzi umefikia wapi, ameziweka kichwani, anatoa tathmini zitaisha lini, wakandarasi wazembe walipigwa chini, Samaki alikua anadeal nao mpaka watu wakazika nyavu haramu wakaweka na misalaba ukidhani marehemu kumbe nyavu za kuvulia samaki. Alishawahi kukamata magari mengi ya serikali yanayofanya shuguli binafsi, anapangua hoja kwa hoja.
Pia jamaa kasomea Sayansi, na unavyojua science haihitaji longolongo ni facts tu, kwenye science hamna uongo kabisa.
Mpeni Dr Magufuli muone, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa wilaya+Mikoa wataacha kunukia Perfume/Marashi na watachapa kazi, then wananchi nao watachapa kazi
Huyu jamaa Dr Magufu, ni mtaalamu sana, alipopewa wizara ya Ardi, cha kwanza alichokifanya alienda darasani zaidi ya miezi 3 kusoma seria za ardi na mabaraza ja miji/vijiji. Alipoanza kazi ardi palianza kua pasafi, sasa sijui aligusa maslahi ya wakubwa akuchukua muda pale akapelekwa Mifugo na Uvuvi, nako huko akafanya mambo, meli ilikamatwa hana utani na haina maana zilikua haziibi samaki ili waliokuwepo walikua hawafuatilii
Ila SISIEMU tunawajua, watafanya kituko, tusubiri.