Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Inaelekea taifa hili limefikia mahali dhana ya utawala bora ambayo imeundiwa hata wizara kuwa ni kiini macho, lakini madhara yake yatatikisa hata kizazi!!!!!!!!!!! Tukishaanza kuyumba hata katika mambo ya wazi ya uzingatiaji wa katiba tunaelekea pabaya sana si muda mrefu ujao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
jambo la msingi ni kuwa pina aka mtoto wa mkulima ana jimbo analosimamia same as anna tibaijuka. Tena hakukuwepo na mwingine yeyote aliye jitokeza kumpinga. Kwa hivyo basi kikatiba wanateulika ktk nafasi ya uPm. Mbona lowassa aliteuliwa PM na wakati huo alipita bila kupingwa!
 
aah yote sawa tu kwani bungeni c meona mambo ,mshikaji kaamua anataka kila ofisi awe na vingamuzi,c unajua mkulima dizaini hapendi story zaidi ya kazi atakuwa kamboa wakati akihitaji kwenda club new york na mtu wahazi yake,mkulima akagoma,ahahahah,LINAWEZEKANA ASILIMIA ZOTE AKAMWEKA MAMA YETU,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,......................:smile-big:,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,................................./????????????????????????????????????????????????
 
Any way, mi sina tatizo na hilo, ukitolea mfano wa lowasa mwaka 2005, watanzania wengi tulikuwa tumelala, tulikuwa hatujui mambo mengi, forum kama hizi hazikuwepo za kupeana ujuzi na taarifa, kama kosa lilifanyika mwaka 2005 siyo tiketi ya kulirudia tena mwaka huu ambapo dr. Slaa ametuamsha akili watanzania. Tusubiri tuone, maana tanzania tumezoea kuona katiba inavunjwa na tunakaa kimya.
Nitatoa mfano miwili, mosi: Kitendo cha dr. Shein kuapishwa kuwa rais wa zanzibar wakati huo hajajiuzulu nafasi yake ya umakamu wa rais wa muungano ni uvunjifu wa katiba.
Pili: Ccm kuwabagua wanaume katika kugombea nafasi ya uspika ni kinyume na katiba lakini tulikaa kimya.
Kwa haya mabo ya msingi hayatapita bila kuhojiwa.
 
Wana jf, kuna tetesi kuwa mbunge wa muleba prof. Anna tibaijuka huenda akateuliwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania badala ya mh. Pinda ambaye kikatiba amekosa sifa za kuwa waziri mkuu kwa kuwa siyo mbunge wa kuchaguliwa katika jimbo kama katiba inavyoagiza. Mwenye taarifa zaidi na hili atujuze.

sioni hoja hapa, tibaijuka ana haki zote za kuwa PM hivyo hivyo kwa Pinda kwani ni wabunge wateule katika majimbo yao.
katika uchaguzi wa vyama vingi nafasi ilikua huru kwa kila chama kusimamisha mgombea wake. ccm walimsimamisha pinda sasa kama upinzani hawakusimamisha mtu hakuna haja ya uchaguzi wa mbunge katika hilo jimbo ingekua enzi zile za chama kimoja then pinda angeshindanishwa na kivuli..

Mi naona wana haki zote kikatiba
 
Wana jf, kuna tetesi kuwa mbunge wa muleba prof. Anna tibaijuka huenda akateuliwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania badala ya mh. Pinda ambaye kikatiba amekosa sifa za kuwa waziri mkuu kwa kuwa siyo mbunge wa kuchaguliwa katika jimbo kama katiba inavyoagiza. Mwenye taarifa zaidi na hili atujuze.

kama pinda sio mbunge wa kuchaguliwa na prf tibaijika naye si mbuke wa kuchaguliwa, kwani wote walipita bila lupingwa kwenye majimbo yao. So, tetesi yako haina hoja ya kuweza kuisupport.
 
Mwenyekiti wa CCM anapishana nini mawazo na Ridhwani??? tegemea blander ndugu.
 
Mwenyekiti wa CCM anapishana nini mawazo na Ridhwani??? tegemea blander ndugu. Hapo anaekuja ni yule ALIETAKA KIPINDUPINDI KIISHE NDANI YA WIKI MOJA DAR!!!!!!!!!! anaandaliwa kuwa MGOMBEA dhidi ya CHADEMA 2015. Kweli CCM wehu...
 
Bila strategy nzuri ya kiutawala awe Pinda, asiwe Pinda hamna kazi ya maana itakayofanyika.
 
Inaweza kuwa tetesi lakini ambayo haitalisaidia taifa kama itakuja kuwa kweli. Kwa hatua aliyofikia huyu mama nilidhani alipashwa kuwa anjishughulisha na shughuli za kijamii kwa tofauti kidogo na sio kwenda kugombea ubunge.

Nilidhani angaanzisha asasi ya kiraia kwa lengo la kuwakomboa wananchi kwa kuwapa fursa kama za ujasiriamali. Vile vile angaweza kuanzisha consultancy firm. Sijafurahi kabisa exposure yote aliopata bado amerudi mbio kutafuta ubunge ili achaguliwe uwaziri!! Kwa altitude hii inaonyesha wazi kabisa kuwa hawezi kutoa leadership ya kueweka kwa nafasi kama ya U PM TZ.

Prof Tiba angejishugulisha na maswala mengine kama nilivyoainisha hapo juu na kama ni swala la utumishi serikalini basi angeonekana tu kama angehitajika. Pro Tiba kama alivyo Dr Batilda she more of technocrat and not politician. She doesn't fit.
 
I once heard this....but well, it was just a story among friends. Who knows!!
 
rostam,lowasa au chenge wanafaa kwenye iyo nafasi. kwani wana pesa za kutosha. hawataweza tena kufanya mchezo wao wa kawaida.
 
rostam,lowasa au chenge wanafaa kwenye iyo nafasi. kwani wana pesa za kutosha. hawataweza tena kufanya mchezo wao wa kawaida.
 
Kwa tabia yake ya kulia bungeni anaweza kurudishwa na JK.
 
Katiba ya nchi gani hiyo, yeye ni kwamba kapita bila kupingwa, hivyo hata wangepiga kura angeshindana na kivuli. Labda kama unamaanisha mbunge wa kuteuliwa kama viki Kamata. Huyu Pinda na Tibaijuka ni wabunge tena wanaostahili kuuchaguliwa maana hata wapinzani inawezekana wanawakubali kule majimboni mwao ndo maana wakakaaa kimya.

Ninachowapendea CCM vichwa vyenu vinasahau kama vya kuku! Yaani hatujasahau ya Masha wewe unachomoka na upupu! Kazi kweli kweli
 
Ama kweli hata mimi nimeamshwa na Forum hii. nimeisoma sawasawa Katiba ambayo inaainisha waziwazi kwamba Waziri Mkuu atatokana na wabunge wa kuchaguliwa jimboni. Mi naona tusianze kuchomekea tafsiri tunazozitaka bali tuzingatie kinachosemwa na katiba ambayo imeandikwa Kiswahili na kila aisomaye ataelewa hivyo.
Kama kuna kosa lilifanywa siku za nyuma na watanzania tulinyamaza ni kwa sababu wengi tulikuwa hatujishughulisha na kusoma katiba inasema nini.
Kwa kweli ujio wa Dr. Slaa umetuchangamsha katika mengi tu ikiwa ni pamoja na kuitafuta, kuisoma na kuielewa katiba ya nchi hii. Binafsi baada ya kuisoma niligundua kile kilicholalamikiwa na wanazuo mbalimbali kwamba katiba yetu imejaa mapungufu mengi mno kiasi cha kuhitaji kutungwa upya maana kuirekebisha tu hakuwezi kukidhi mahitaji.
Isitoshe mara kadhaa
wanaoitwa wabunge "waliopita bila kupingwa" baadhi yao ni waliotumia hila za chinichini ukiwemo ulaghai kuwatisha au kuwarubuni walionia kupambana nao katika uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa kule Nyamagana na Musoma vijijini. Natoa mwito kwa wataalamu wa sheria kuhakikisha nchi inatawaliwa kwa mujibu wa katiba inavyosema na si vinginevyo.
 
magufuli ni dictator kazi ya upm haiwezi angekuwa polisi angeuweza uigp hapo mahali pake kiti kingekuwa kimepewa mwenyewe

verify unachokisema bwana muro kuwa magufuli ni dictator azawaizi utakuwa umezuwa jambo ambalo si la kweli!
 
Leo ndio lile jina la mtu ambalo Kikwete anapendekeza awe Waziri Mkuu litawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge. Je? Ni nani ataweza kufanikiwa kunyakua nafasi hii nyeti serikalini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom