Ndugu Wana JF habari ndiyo hiyo ni suala la muda tu lakini yule kada mtiifu wa Timu Lowasa 2015 anatajwa sana huko katika korido za Mamlaka Kumrithi Kinana ambaye juzi tulitangaziwa Umma kuwa ameamua kujiuzulu nafasi yake ya Makamu mwenyekiti Bara na Mhe Samia kuridhia kujiuzulu kwake.
Hizo ndio fununu zilizoshika kasi kwa sasa kwamba kada maarufu Dkt. Kigwangalla ndiye atakayemrithi Mzee wetu Komredi Kinana aliyejiuzulu na Kustaafu moja kwa moja