Makamu wa kwanza wa Raisi wa SMZ kwa mujibu wa katiba, ni Lazima atoke chama kingine, kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu. NI LAZIMA. ndiyo maaana awamu ya pili ya Mh Sheni hapakuwa na Makamo wa Kwanza kwa vile CUF (Chama kilichokuwa kimeshika nafasi ya pili) iligoma kuutambua uchaguzi na matokeo yake.
Hivyo Makamo wa kwanza hawezi kuteuliwa na Raisi wa Zanzibar bali chama (ACT) kwa maana ya mwaka huu, ndio wanaotakiwa kuteua jina la mtu anayefaa kuwa makamo wa kwanza, Rais wa Znz anamwapisha tu, wala hamteui, ila anateua makamo wa pili.
Tuelewane vizuri hapo, Rais wa Zanzibar hawezi kuteua Makamo wa Kwanza wa Rais, ACT wasipopeleka jina, nafasi itabaki wazi siku zote.
Asante sana kwa maelezo yako mazuri na namna ulivyoelezea.
Hapa tumebakiwa na issue moja tu,wewe umejadili kwamba Rais wa zanzibar hateui makamo wa kwanza wa rais bali analetewa hina toka kwenye kile chama cha pili kwa ushindi ambacho kwa kesi yetu ni ACT WAZALENDO.
Hebu twende kikatiba zaidi tuone Dhana nzima ya uteuzi ,je ni ACT WAZALENDO au RAIS WA ZANZIBAR ndio mwenye mamlaka ya kuteua Makamo wa Kwanza wa Rais.??.
Twende kikatiba zaidi, Ibara ya 39(1)(2)inasema...
39.(1) Kutakuwa na Makamo Wawili wa Rais ambao watajuilikana
kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.
(2) Ndani ya siku saba mara baada ya kushika madaraka,
Rais ATATEUA Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa
Rais.
Kwa ibara hii hakuna mjadala kikatiba kwamba nani anamteua Makamo wa kwanza wa Rais...inasema kabisa Rais "ATATEUA"
Twende pamoja kikatiba zaidi,ibara hiyo hiyo ya 39 kifungu kidogo cha tatu (subsection 3) inasema..
39(3) Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za
kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na ATATEULIWA na Rais baada ya KUSHAURIANA na chama kilichotokea
nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais.
Ibara ndogo ya tatu imeelezea vyema kabisa kwamba bado Rais ATAMTEUA huyo makamo wa kwanza LAKINI baada ya Rais KUSHAURIANA na chama kilichotokea nafasi ya pili ambacho kwa case yetu ni ACT WAZALENDO. watakaa na kushauriana kuhusu Makamo wa Rais.
Usikimbie, twende kikatiba zaidi Ibara ya 39 kifungu kidogo cha 8 inasema na nainukuu
"(8) Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa
Rais hawatoanza kazi mpaka WAAPISHWE kiapo cha uaminifu na kiapo
chengine mbele ya Rais kama kitakavyoelezwa katika Sheria
iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
Siku zote anaekuteua ndio anakuapisha,unakula kiapo mbele yake hivyo ni wazi kuwa MaKamo wa kwanza wa Rais anaapishwa na boss wake aliyemteua kwenye nafasi hiyo na hawezi kuanza kazi bila KIAPO mbele yake ,hivyo ni kusema kwamba ACT WAZALENDO wana uteuzi wao wa jina huko kwenye chama kama ilivyo utaratibu wa chama chao lakini wakiwasilisha jina kwa Rais wa zanzibar upepo unageuka ,Rais wa zanzibar ndo anakua MTEUZI wa jina husika baada ya kushauriana na chama husika.
Hii inamanisha ACT WAZALENDO wanaweza kuleta jina toka chamani kwenye nafasi ya Makamo wa Rais na wakafanya MASHAURIANO na Rais wa zanzibar kuhusu jina husika na inawezekana kwenye mashauriano jina lisipite na wakarudishwa waende kuteua jina lingine..sio lazima jina wanaloleta kwa Rais wa zanzibar ndio lipite.
What if wanaleta jina la xxx ambaye kwenye classified files za serikali ya zanzibar huyo xxx ana record ya usaliti ,kushirikiana na mataifa ya nnje kuhujumu serikali ya zanzibar .
So huyo xxx hatoweza kukubaliwa na Rais maana kumpa hiyo nafasi wakati vyombo husika vina taarifa zake za tabia isiyo njema na bado tupitishe jina lake just because ACT WAZALENDO wameleta jina HAIWEZEKANI.
Litakataliwa na ACT WAZALENDO wataleta jina lingine ndo maana halisi ya KUSHAURIANA.
Twende kikatiba zaidi.
Ibara ya 39A inasema
39A.(1) Endapo, ndani ya siku saba mara baada ya Rais kushika
madaraka, chama kinachostahiki kutoa Makamo wa Kwanza wa Rais,
kitashindwa KUWASILISHA kwa Rais jina la uteuzi wa Makamo wa
Kwanza wa Rais, Rais, bila ya kujali masharti ya kifungu cha 39(1) na
(3) cha Katiba, atawacha wazi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa
Rais na kuteua Makamo wa Pili wa Rais.
Hapa 39A inasema kifupi Chama kinafanya kazi ya KUWASILISHA kwa Rais jina la UTEUZI wa makamo wa Rais.
Keywords ni Chama kinawasilisha jina la UTEUZI.
Hii ni kusema kwamba Rais wa Zanzibar ndiye ANAEMTEUA makamo wa Rais na sio ACT WAZALENDO wanamteua, wao WANAWASILISHA jina tu kwa Rais kwa ajili ya UTEUZI.
ACT WAZALENDO wanalipataje pataje jina hilo huko kwenye chama hiyo ni story ya siku nyingine lakini mpaka hapa anaetoa Uteuzi wa Makamo wa Kwanza wa Rais ni RAIS WA ZANZIBAR na anampa KIAPO.
Kikatiba zaidi"