Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,228
- 2,064
Habari zenu!
Hasa wapenda burudani wa mziki huu wa bongo fleva miondoko ya hip hop kwa Hapa Tz.
Unajuwa miaka ya zamani kidogo kuanzia 1997~2009 mziki wa Tanzania ulipiga hatua kubwa sana katika uandishi wa mashahiri kuliko miaka hii ya hivi karibuni,ingawa katika miaka hiyo nilikuwa mdogo lakini nilipenda sana kusikiliza miondoko ya hip hop kutoka nyumbani Tanzania.
Wasanii kama Afande Sele,Solo Theng(traveler),Juma nature,East Coast team,Balozi,Imamu Abasi,Adili,Fanani,Soggdog,Jaymo,Sugu,na wengine wengi hawa walifanya nipende mziki wa hip hop kwa Bongo.
Lakini nakumbuka mwaka 2004 kuliandaliwa shindano lililopewa jina la mfalme wa rhyme ambalo liliteka vichwa vya habari Tanzania na nchi Jirani.Nakumbuka katika mwaka 2004 nilikuwa darasa la 4 lakini nilikuwa nafuatilia kwa umakini sana Haya mashindano.Wasanii wengi sana walishiriki katika shindano la mfalme wa rhymes ambalo liliandaliwa na Global publisher(Erick shigongo).Kama yalivyo mashindano mengine yale lazima apatikane mshindi hivyo katika mashindano Haya msanii Afande sele Aliibuka mshindi.
Kwa umri wangu sikujuwa kama mshindi Alipatikana kwa njia gani?Kama kupiga kura au alichaguliwa na majaji(ushindi wa mezani).Lakini ninachojuwa baada ya kutangazwa Afande sele kuwa ni mshindi kuliibuka migogoro,sintofaham,chuki,na wivu miongoni mwa wasanii hivyo ule umoja na urafiki ulipotea kabisa.
Kwa kuwa uongo ukisemwa sana kwa kurudia rudia bila kukanushwa hugeuka/huwa kweli na kwa kuwa historia haibadiliki ila inasahihishwa basi ni nani alistaili kuwa mshindi wa rhymes kwa mwaka ule 2004.Kumb ilifanyika mwaka mmoja tu na hii kutokana na matatizo yaliyojitokeza.
Karibuni.
Hii ilikuwa ni moja ya collabe kali kabisa iliyokutanisha vichwa 3 ndani ya track moja.Mtazamo By Afande sele ft Joseph Haule na Solotheng.