Mfalme wa rhymes ilikuwa inachukuliwa kwa nyimbo za ndani ya mwaka, sio uwezo wa mwanamuziki kiujumla, ni wimbo fulani katika mwaka husika ndio unashindanishwa.
Sasa kwa mwaka 2003/2004 darubini kali haikuwa na mpinzani tizama mistari yake mule, kidogo nhoma nyingine kali nadhani ni msinitenge ya prof jize..
Fid q hakuwa na ngoma kali msimu huo..
Ila fid alikuwa anaelekea kuchukua ya mwaka 2005 na ngoma yake ya mwanza mwanza kama sikosei, ila watu ndio wakaleta zengwe shindano likafa na wasanii walileta utata baada ya kuona mshindi ameshajulikana..
Ukisikiliza ngoma ya nako2nako na fid inaitwa hakuna mahali kama, fid ameongelea hii ishu.