Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Watu gani wewe.. Jamaa alishinda kwa haki....
Niliona ujinga sana watu walianza kumponda afande...kisa ni wa Moro kipindi kile walitegemea dar ingechukua hahahaaaa.....

Ila ukweli ni kuwa uwezo wa Afande ulikuwa ni wa kawaida sana mbele ya Professor Jay
 
.... Kwenye huu mtazamo naona vingi vihoja, yaani watangazaji ndio sasa mameneja,
Vidato sita nilivyopitia ndivyo vinavyonisaidia, uamuzi ukizingatia hata wakinibania ni kipaji tu, ni mtazamo tu.....

Mwanazuoni aliyekomaa.
Jamaa alikuwa music genius kwa wakati ule alafu alikuwa ndo msanii aliyesoma sana
 
Darubini ilitoka baada ya kupewa tayari ufalme was rhymes lakini kwenye mashindano aliingia na wimbo mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii Wawili.Afande sele alibebwa sana katika ushindi ule kwa kuchukuwa wimbo ambao tyr alibebwa pia
Nakataa Kipindi ambacho Afande anachukuwa Ufalme wa rhymes wimbo wa tarubini kali ulikuwa hautoka Mkuu.
Darubini ulitoka baada ya kupewa ushindi
Mkuu darubini kali ft ditto ndio afande alichukulia tuzo.
Mzee mwenzangu hebu tuwekane sawa mtazamo imetoka mwaka gani na darubini kali imetoka mwaka gani?
Nakumbuka mkali wa ryhmes afande sele aliperfom darubini kali.
Kidhati kabisa afande sele alistahili.
Acha kupotosha, Darubin kali ndiyo wimbo uliompa ushindi Afande Sele.
darubini kali ilitoka mwaka gani tuanze hapo.Kama kumbukumbu zangu haziko sawa utanirekebisha ila nakumbuka Afande sele aliingia na mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii wengine.We unadhani kwanini Solo theng alilaumu sana?
Jibu hilo hapo.
Screenshot_2019-05-30-11-28-58-1.jpeg
 
darubini kali ilitoka mwaka gani tuanze hapo.Kama kumbukumbu zangu haziko sawa utanirekebisha ila nakumbuka Afande sele aliingia na mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii wengine.We unadhani kwanini Solo theng alilaumu sana?
wewe hukumbuki vizuri, solo thang aliwalaumu kwenye wimbo wa kilio changu feat q chilla na sio kwenye mtazamo
 
Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.
mbona mgumu kuelewa hivyo, wimbo alioingia nao kwenye shindano ni darubini kali na sio mtazamo
 
kwa kumbukumbu zangu ,darubini kali ni wimbo uliotoka mwishoni mwa mwaka 2003 na kwa kiasi kikubwa wimbo huu ndio uliompa ushindi afande sele..
 
Alafu nashangaa solotheng alilalamika sana wakati hakuwa na ngoma kali sana kwa wakati ule.
We kweli ulikuwa bado kinda kipindi hicho!!!.
Solo hakuwa na ngoma kali!?.
Unaijua albamu yake ya HOMA YA DUNIA?.
Solo ndio alistahili ufalme wa ryhmes.
Ndio mtaalam wa vina kuwahi kutokea bongo.
"Bila shaka Solo thang nakubalika
Kama unabisha muuliza John kalamashaka
Hakuna utani hii fani mi nainyaka
Acha masihara
Mi kinara
Bongo kenya n'tang'ara
Sina papara
Ndio maana bora
Wenye vilemba vya ukoka wamedorora
Hili kombora
Msururu mrefu watanibeba na vingora....
 
Nakumbuka baada ya mfalme sele kupewa ule ushindi Solo theng alitoa ngoma ya Ndugu zangu ndugu zangu alitoa hisia zake nje alishindwa kuvumilia kabisa.
Ila jamaa alikuwa anajuwa kuchora mistari na flow tamu Sanaa
Ngoma ilikuwa inaitwa KILIO CHANGU.
Ulamaa alikuwa na flow za hatari na lugha safi kabisa.
 
Washindi...

1. AFANDE SELE

2. INSPECTOR HAROUN

3. MANDOJO NA DOMOKAYa

4. Mwanafa

5. Prof Jay

Sele alistahili.. Ila Solo kukosekana hata 5 bora hakika walizingua sana..
Man Dojo na Domokaya waliingia kwenye top 5?
 
Back
Top Bottom