Njemba Soro.
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 3,732
- 6,561
wangempa ray c
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora usinge comment mtazo ilitoka baada ya jamaa kuondoa tofauti zao kutokana na iyo tuzo
Hapana mkuu haukuwa ushindi wa mezani kabisaa, Sele alikua kalikamata jiji kwa mwaka ule haswaa na Nyimbo yake ya Darubini Kali.Mbona watu walidai jamaa alibebwa kwa ushindi wa mezani kuliko uwezo wake
Hii nilikuwa naikubali tatizo kipindi hicho hiphop ilikuwa imeshika game kabla wabanapua hawaja takeover,darubini kali ilikuwa overratedJibu hilo hapo.View attachment 1111967
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)Ahaha unanichekesha unanipa furaha au unafikiri utapata zari kama yesu alivyopaa , hacha kujidangaya kwa mungu si kwa mzungu kwamba utapita njia za panya
Mwanamke kama hataki penzi usimbake,kulazimisja penzi sawa na kulazimisha fani kisha unaleta utani, sasa inakuaje unataja taja majina nyimbo tena nyimbo nzima kwa mistari isiyo kuwa na vina
Moja ya beat kali kutoka kwa majani ni kweli jamaa alistahili ushinde ule
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)Hii nilikuwa naikubali tatizo kipindi hicho hiphop ilikuwa imeshika game kabla wabanapua hawaja takeover,darubini kali ilikuwa overrated
Fid Q hakuwepo kwenye muziki kipindi hicho
Afande sele alideserve... ila solo thang pia mkali sana.. profjizze.... pia mkali......
Afande sele aliimba nyimbo moja na watu pori mpaka leo kila siku naiskizila.. inaitwa nafsi ya mtuuuu...
Mwingine anakuja kwako anashida tena mikono nyuma amekondaa,
Unamtazama kwa huruma na kukwepa lawama unasema looo lazima nimpige tafuu, kwa moyo mkunjufu, tena bila kujali skendo zake za uhalifuu, na uchafuu wa mwili na tabia unakua nae unaishi nae kama waifuuu.. kumbe ni naifuu anakusifu machoni moyoni anakusanifuuuu..
Aiseeee acha kabisa hii.verse
Kwa maoni yangu Afande Sele alistahili kihalali..ule wimbo ulishirikisha vichwa vyenye akili sana kwenye mashairi. Ni wimbo ambao mpaka leo una ujumbe
Ndio maana mtu yeyote akiniambia Tanzania ya sasa ina rappers anaweza kufikiri ninamdharau kwakuwa nitatikisa kichwa na kuondoka.Kwakweli Afande sele alishinda kihalali kabisa..usinitenge ya Prof jize ilishika namba 2..ngoma zilikua Kali Sana
Umeitoa wapi aiseeMimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Afande anasema wote (wote kimya)
Ntakayo nena hapa yatamgusa mwenye hekima
(Hapo!) hapo ulipo
Kama waipenda pepo kwanini uogope kifo?
(Eehee) unachekesha
(Aah) wanipa raha
Unafikiri mbinguni utakwenda kwa motor car eh?
(Ama utapata zali kama Yesu alivyopaa?)
Acha kujidanganya, kwa Mungu si kwa mzungu
Unapokwenda kwa pipa ikibidi kwa njia za panya
(Loo) haiwezekani
(Hasa?) bila ya imani
Unaelipiza baya kwa jema…
(We ni shetani)
Haufai kanisani, haufai msikitini
Na hutufai kwenye fani
Take care utapotea
(Aliwazalo mjinga ndilo litalomtokea)
Na hii ndo darubini (darubini)
Wasanii muweke akilini, hasa kwa mtu makini
Makini kiusanii
Ila kama mtalii (no sweat, tupa kapuni)
Watakuokota chini
Unafanya mziki Bongo unaekti kama matoni
(Ya nini?!)
Bora kuimba katuni
Lugha ngeni za nini kwenye mziki wa nyumbani?
(Wakati Bongo Flava inapeta zaidi uswahilini)
Mi n’nacheka sana (hee)
Kuna vitu vya kuimba vyenye maana kila kona
(Sasa?)
Inakuwa vipi unataja taja majina tu, nyimbo nzima
(Tena) kwa mistari isiyo na vina!
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Yes, naona mbali, kwa darubini kali
Ndo maana mziki wangu unaegemea kwenye ukweli
Kwa mfano…
(Labda ungewapo mfano kabla hujashusha kibano)
Nasema rap ni ukweli mtupu, rap jasiri
Rap si kuimba uongo (kama siasa za bongo)
Useme kwenu una Benz wakati jumba la udongo! Mh!
Bwa’ mdogo acha upambe, unavyopelekwa tu
Unakwenda kama ling’ombe
(Simama utupe ujumbe)
Kama huwezi unyamaze
Nasema mara ya mwisho…
(Sio lazima wote tuimbe)
Watu wanataka ujumbe, sio majigambo tu
(Mnasifu ngono na pombe)
Pumbavu hamna soni eh, kwenye zama za ukimwi
Kwenye nchi masikini, ya pili kutoka chini
Afande nashangaa (hata Mungu anakataa)
Kwa msanii wa nchi hii
Kuimba nyimbo za furaha, kila saa
(Wakati huko kijijini watu wanakufa kwa njaa)
Haipendezi, kutomjali mwenzako eti kwa ajili ya mavazi (haipendezi)
Ama kujiona bora eti kwa ajili ya makazi (haipendezi)
Kuna tofauti gani kati ya Temeke na Mbezi?
Au labda ukiishi Mbezi utakapokufa hauozi? (twashangaa)
Eti Majani vipi? Kwanza stopisha beat
Nimuulize kijana alichokipata ni kipi
Aliponyoosha miguu wakati blanketi ni fupi
(Aling’atwa na mbu kwenye visigino huyo)
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Na bado tu, mwaka huu haki ya nani
Mamluki kwenye game mtatoka taka msitake
(Na hii ndo maanake)
Mwanamke kama hataki basi muache aende zake (usimbake)
Kulazimisha penzi ni hatari sawa na kulazimisha fani
(Kisha unaleta utani)
Mpumbavu, hilo ni kosa kama padri kubaka muumini
(Au kama ticha mkuu kumbaka denti ofisini)
Utafungwa! (arabuni utanyongwa)
Bwa’ mdogo, ndani ya shamba la miwa hauwezi ukavuna miogo
(Kuna tofauti kubwa kati ya wivu na usongo)
Sahau superstar, superstar
Kujifanya msanii ndani ya jumba la sanaa
(Wasanii tunashangaa) unashuka si tunapaa
(Unainuka si tunakaa)
Ukipotea? (Kwetu furaha)
Adui? (Muombee njaa)
Ntanyoosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Mimi ni msanii (mimi ni msanii)
Kioo cha jamii (kioo cha jamii)
Mimi naona mbali (mimi naona mbali)
Kwa darubini kali (kwa darubini kali)
Kwani huyu na yule ni ya mwaka gani?Wakati ule AfandeSele alikuwa juu ya wote!
Mimi nilikuwa form 5 nakumbuka kila kitu.
Kwnye mtazamo kuna mstari anasema " mimi naogopa sana tunavyotukanana"
"Isije huko mbele tukachinjana"
Wakati huo alikuwa amechinjwa Steve 2k jamaa akaonekana kama nabii!
Afande alikuwa kileleni bhana, watu waliridhika japo haiwezekani wote wafurahie, fid q enzi hizo Alikuwa anatumbua tu chunusi!
Jamaa mmoja anaitwa D-TossHivi bila mademu aliimba nani?
Dah umenikumbusha mbali sana hilo tukio ulikuwa ni promo ya kumpaisha afande sele kitu ambacho wasanii wengine hawakujua kabisa
Promo ilianzia kwenye wimbo wa darubini wimbo ukawa nzuri sana wajanja wa mjini wakaa chini wakasema tunampaisha vipi afande sele, likaandaliwa shindano hili nakumbuka diamond jubilee ilitapika watu maana mpambano ulikuwa mkali pia kipindi hicho bongo ndio kwanza mambo ya burudani tunajifunza
Kiukweli mshindi pale alistahili awe prof jay ila kwakua walipanga wao nani wampe promo wakampa afande sele
Hili pambano ndio lilifanya prof na solo wasishiriki video y mtazamo walipogundua afande aliwasnitch wakamzilia video yake
Acha uongo kwenye video solo yupo .prof j hakuepo kwavile wakat wana shoot video prof j alikua mwanza kwenye show ndo akashindwa kuwepo kwenye videoDah umenikumbusha mbali sana hilo tukio ulikuwa ni promo ya kumpaisha afande sele kitu ambacho wasanii wengine hawakujua kabisa
Promo ilianzia kwenye wimbo wa darubini wimbo ukawa nzuri sana wajanja wa mjini wakaa chini wakasema tunampaisha vipi afande sele, likaandaliwa shindano hili nakumbuka diamond jubilee ilitapika watu maana mpambano ulikuwa mkali pia kipindi hicho bongo ndio kwanza mambo ya burudani tunajifunza
Kiukweli mshindi pale alistahili awe prof jay ila kwakua walipanga wao nani wampe promo wakampa afande sele
Hili pambano ndio lilifanya prof na solo wasishiriki video y mtazamo walipogundua afande aliwasnitch wakamzilia video yake
zile picha ziliungwa ungwa kutoka video nyingineMkuu kuna Mahala hapa napingana na maneno yako, Nyimbo ya Mtazamo ilirekodiwa baada ya mashindano kuisha na ilikua ni kuthibitishia mashabiki kwamba hawana beef tena kati yao.
Na swala la kutoonekana kwenye video ilikua bahati mbaya tu kwa Prof Jay ndio alishindwa fika location siku hiyo maana alikua kikazi Tanga nadhani.
Solo Thang alikuepo na video walishoot morogoro ingia YouTube kaangalie vizuri tena mkuu.
Hapana mkuu napingana na wewe kwenye hili, Solo alikuepo kwenye video na wameshoot pamoja na Afande siku moja hamna clip zilizoungwa ungwa kutoka video nyinginezile picha ziliungwa ungwa kutoka video nyingine
Nashukuru umewasaidia vijana, walitaka tupigizane kelele tu
Japo najua wengine "wabishi kufa" watakubishia tu watakwambia Wikipedia hata wewe ukitaka unaweza edit.
Ila ukweli unabaki pale pale, afande sele alikuwa mkali wa rhymes kwa darubini kali.