Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Darubini ilitoka baada ya kupewa tayari ufalme was rhymes lakini kwenye mashindano aliingia na wimbo mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii Wawili.Afande sele alibebwa sana katika ushindi ule kwa kuchukuwa wimbo ambao tyr alibebwa pia
Darubini ndio nyimbo iliyompa ufalme Afande Sele, darubini ilitoka kabla ya shindano na sio baada
 
Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.
Acha ubishi darubini ilitoka kabla ya shindano na ndio nyimbo iliyombeba afande hadi akatwaa tunzo... Dito alipanda jukwani kuperform darubini akiwa bado yupo primary...
 
Niliwahi kusikia Afande Sele a.k.a Simba wa Morogoro akisema
"Eti ni bora wangempa treka kuliko kile kigari chenye milango ya kunguka juu kama mabawa"
 
Enzi izo mziki ni mziki kwelikweli
Niliandika mada kama yako miaka michache nyuma...hii hapa..

NANI HASA ALISTAHILI UFALME WA RHYMES MWAKA 2004?

Shindano la kumsaka mfalme wa Rhymes katika bongo flava ni moja ya shindano lililopata msisimko mkubwa kwa kipindi hicho, hii inawezekana ilitokana na kukutanishwa manguli wa muziki kwa kipindi hicho hali iliyopelekea uamuzi wa nani ashinde kuwa mgumu wa walio wengi!

Shindano liliwakutanisha

1. Jay moe(kama unataka demu)
2. Afande Sele(Darubini kali)
3. Prof J(Msinitenge)
4. Inspector Haroun (Bye Bye)
5. Solo Thang(Simu yangu)
6. Madee(Kazi yake Mola)
7. MwanaFA(Alikufa kwa ngoma)
8. Mandojo na Domokaya(Nikupe nini)
9. Soggy Dogy(Kulwa na Doto)
10. Dully Sykes

Ila Dully alijitoa siku chache kabla ya shindano!!

Shindano liliandaliwa na Global Publisher chini ya E. Shigongo na zawadi kwa mshindi wa kwanza lilikuwa gari, japo sikumbuki ni gari ya aina gani!!

Shindano lilifanyika usiku wa tarehe 27 June(siku ya ijumaa), na hatimaye Afande Sele kutawazwa kama mshindi na kuwa mfalme wa rhymes, huku ushindi wa pili ukienda kwa Inspector Haroun na ushindi wa 3 wakichukua akina Mandojo na Domokaya!

Ushindi huu ulipingwa na watu wengi kuanzia watu wa kawaida mpaka wasanii wenyewe!!

Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli"

Solo Thang akuishia hapo, katika wimbo wa Traveller anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo sele"

Fid Q naye katika Mwanza Mwanza aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"

Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu!!

Sasa ni takribani miaka 12 imepita toka Afande Sele atangazwe kuwa mfalme wa rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano alikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kunakoitwa kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi!!

Je Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes? Kama hakustahili nani alipaswa kupewa hilo taji?
 
We kweli ulikuwa bado kinda kipindi hicho!!!.
Solo hakuwa na ngoma kali!?.
Unaijua albamu yake ya HOMA YA DUNIA?.
Solo ndio alistahili ufalme wa ryhmes.
Ndio mtaalam wa vina kuwahi kutokea bongo.
"Bila shaka Solo thang nakubalika
Kama unabisha muuliza John kalamashaka
Hakuna utani hii fani mi nainyaka
Acha masihara
Mi kinara
Bongo kenya n'tang'ara
Sina papara
Ndio maana bora
Wenye vilemba vya ukoka wamedorora
Hili kombora
Msururu mrefu watanibeba na vingora....

Acha zarau ndugu.Sio kama nabeza uwezo wa Solotheng hapana,ila nasema kipindi cha mashindano hayo hakuwa na ngoma kali at that moment
 
Jay hakustahili hilo liko wazi kabisa, Solo Thang ni mkali sana ila kwa afande wa kipindi iko alikua kiboko.

Afande alistahili kuwa mkali wa rhymes.

Acha kuchekesha wewe.Yani Jay hakustaili kushinda ile tuzo.
Ebu soma tena maelekezo yako
 
Bila mademu nani angepiga pamba,bila mademu nani angejiona bomba .... wale mliosomba shule za bweni haya mambo mliyaona
Ninayo hiyo ngoma.. Ngoja nitakuchekia aliyeimba!!
 
Acha zarau ndugu.Sio kama nabeza uwezo wa Solotheng hapana,ila nasema kipindi cha mashindano hayo hakuwa na ngoma kali at that moment
Kwani si wewe mwenyewe ndiye uliyesema kipindi hicho mashindano yanafanyika ulikuwa bado mtoto!?.Sasa dharau imetoka wapi?.
Ndio maana kuna sehemu kuna mdau kauliza kama Solo alishawahi kuwa kundi la wateule we ukajibu hapana.Nikakushauri usijibu vitu usivovijua kwa sababu wakati hayo mambo yanatokea wewe ulikuwa bado mtoto.
Kuhusu swala la Solo kutokuwa na wimbo mkali kwa kipindi hicho,inategemea wewe na mtazamo wako juu ya wimbo mkali ukoje.
 
Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.
Mzee mwenzangu ww ndio huna kumbukumbu nzuri unataka kusema darubini kali imetoka baada ya shindano, hapo umekosea kabla ya shindano darubini kali ilikuwepo.
Na kwa kuweka kumbukumbu sawa aliperform siku ya shindano kiasi watu wakambeba juu juu.
 
Wakati Afande anaperform darubini kali nakumbuka hata Mr.2 (Sugu) alipanda stejini kumsapoti Afande, shangwe lilikua kubwa sana. Uwepo wa Sugu pale stejini ulimpa points sana Afande lkn aliyefunika zaidi alikua Dogo Ditto. Ditto alimfunika sana Afande kwenye ile shoo utafikiri yeye ndo mwenye wimbo
 
Back
Top Bottom