Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Nani kwa Hakika alistaili ufalme wa rhymes ~2004?

Niliandika mada kama yako miaka michache nyuma...hii hapa..

NANI HASA ALISTAHILI UFALME WA RHYMES MWAKA 2004?

Shindano la kumsaka mfalme wa Rhymes katika bongo flava ni moja ya shindano lililopata msisimko mkubwa kwa kipindi hicho, hii inawezekana ilitokana na kukutanishwa manguli wa muziki kwa kipindi hicho hali iliyopelekea uamuzi wa nani ashinde kuwa mgumu wa walio wengi!

Shindano liliwakutanisha

1. Jay moe(kama unataka demu)
2. Afande Sele(Darubini kali)
3. Prof J(Msinitenge)
4. Inspector Haroun (Bye Bye)
5. Solo Thang(Simu yangu)
6. Madee(Kazi yake Mola)
7. MwanaFA(Alikufa kwa ngoma)
8. Mandojo na Domokaya(Nikupe nini)
9. Soggy Dogy(Kulwa na Doto)
10. Dully Sykes

Ila Dully alijitoa siku chache kabla ya shindano!!

Shindano liliandaliwa na Global Publisher chini ya E. Shigongo na zawadi kwa mshindi wa kwanza lilikuwa gari, japo sikumbuki ni gari ya aina gani!!

Shindano lilifanyika usiku wa tarehe 27 June(siku ya ijumaa), na hatimaye Afande Sele kutawazwa kama mshindi na kuwa mfalme wa rhymes, huku ushindi wa pili ukienda kwa Inspector Haroun na ushindi wa 3 wakichukua akina Mandojo na Domokaya!

Ushindi huu ulipingwa na watu wengi kuanzia watu wa kawaida mpaka wasanii wenyewe!!

Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli"

Solo Thang akuishia hapo, katika wimbo wa Traveller anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo sele"

Fid Q naye katika Mwanza Mwanza aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"

Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu!!

Sasa ni takribani miaka 12 imepita toka Afande Sele atangazwe kuwa mfalme wa rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano alikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kunakoitwa kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi!!

Je Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes? Kama hakustahili nani alipaswa kupewa hilo taji?
 
Washindi...

1. AFANDE SELE

2. INSPECTOR HAROUN

3. MANDOJO NA DOMOKAYa

4. Mwanafa

5. Prof Jay

Sele alistahili.. Ila Solo kukosekana hata 5 bora hakika walizingua sana..
Watu walikuja na majina yao mfukoni.Ndo maana Soggy mpaka leo hamkubali afande,anakwambia wakati wako 'rosegarden' i think john dilinga alimtajia top 5 yote itakavyokuwa,na kuja kutangazwa mshindi ndo ikawa hivyo,ndo kisa cha afande na komwe kubwa"soggy" kutoelewana,kila kinterview mmoja akihojiwa lazima ampondee sana mwenzie.

Ndo' Fid akaja na ile line"Mkali wa rhymes ambaye soggy doggy hamtaki....
Anamwita kobe hawezi mshinda mbio farasi"

Sent from my SM-G900P using JamiiForums mobile app
 
"Washatabiri watu wangu wa mtaani kwamba,mimi ndo mfalme ninayefuata baada ya suleman".....mwanza mwanza!
Mfalme wa rhymes ilikuwa inachukuliwa kwa nyimbo za ndani ya mwaka, sio uwezo wa mwanamuziki kiujumla, ni wimbo fulani katika mwaka husika ndio unashindanishwa.
Sasa kwa mwaka 2003/2004 darubini kali haikuwa na mpinzani tizama mistari yake mule, kidogo nhoma nyingine kali nadhani ni msinitenge ya prof jize..
Fid q hakuwa na ngoma kali msimu huo..
Ila fid alikuwa anaelekea kuchukua ya mwaka 2005 na ngoma yake ya mwanza mwanza kama sikosei, ila watu ndio wakaleta zengwe shindano likafa na wasanii walileta utata baada ya kuona mshindi ameshajulikana..
Ukisikiliza ngoma ya nako2nako na fid inaitwa hakuna mahali kama, fid ameongelea hii ishu.

Sent from my SM-G900P using JamiiForums mobile app
 
Darubini ilitoka baada ya kupewa tayari ufalme was rhymes lakini kwenye mashindano aliingia na wimbo mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii Wawili.Afande sele alibebwa sana katika ushindi ule kwa kuchukuwa wimbo ambao tyr alibebwa pia
Acha kupotosha, Darubin kali ndiyo wimbo uliompa ushindi Afande Sele.
 
"Washatabiri watu wangu wa mtaani kwamba,mimi ndo mfalme ninayefuata baada ya suleman".....mwanza mwanza!

Sent from my SM-G900P using JamiiForums mobile app
Na ni kweli kwa mwaka 2005 hakukuwa na wakumfunika fid q, ilikuwa ni moja kwa moja fid anabeba ndoo. Wakakimbilia kujitoa kwa chuki, husda na roho mbaya za kibinadamu.
 
Mkuu darubini kali ft ditto ndio afande alichukulia tuzo.

darubini kali ilitoka mwaka gani tuanze hapo.Kama kumbukumbu zangu haziko sawa utanirekebisha ila nakumbuka Afande sele aliingia na mtazamo ambao aliwashirikisha wasanii wengine.We unadhani kwanini Solo theng alilaumu sana?
 
Mzee mwenzangu hebu tuwekane sawa mtazamo imetoka mwaka gani na darubini kali imetoka mwaka gani?
Nakumbuka mkali wa ryhmes afande sele aliperfom darubini kali.
Kidhati kabisa afande sele alistahili.

Wewe hauna kumbukumbu nzuri labda.Afande sele baada ya kushinda akaachia ngoma yake ya Darubini kali ambayo ilifanya vizuri sana kwenye chat za bongo nadhani hapa ndo unajichanganya na kuzania ilitoka kabla ya mfalme wa rhymes.
Mtazamo ilikuwa kabla ya mashindano na ndo nyimbo aliyoingia na Sele.
 
Umetukumbusha mbali. Labda ungeandika ni ngoma gani zilishindanishwa, ili tuzchambue vzuri
 
Niliandika mada kama yako miaka michache nyuma...hii hapa..

NANI HASA ALISTAHILI UFALME WA RHYMES MWAKA 2004?

Shindano la kumsaka mfalme wa Rhymes katika bongo flava ni moja ya shindano lililopata msisimko mkubwa kwa kipindi hicho, hii inawezekana ilitokana na kukutanishwa manguli wa muziki kwa kipindi hicho hali iliyopelekea uamuzi wa nani ashinde kuwa mgumu wa walio wengi!

Shindano liliwakutanisha

1. Jay moe(kama unataka demu)
2. Afande Sele(Darubini kali)
3. Prof J(Msinitenge)
4. Inspector Haroun (Bye Bye)
5. Solo Thang(Simu yangu)
6. Madee(Kazi yake Mola)
7. MwanaFA(Alikufa kwa ngoma)
8. Mandojo na Domokaya(Nikupe nini)
9. Soggy Dogy(Kulwa na Doto)
10. Dully Sykes

Ila Dully alijitoa siku chache kabla ya shindano!!

Shindano liliandaliwa na Global Publisher chini ya E. Shigongo na zawadi kwa mshindi wa kwanza lilikuwa gari, japo sikumbuki ni gari ya aina gani!!

Shindano lilifanyika usiku wa tarehe 27 June(siku ya ijumaa), na hatimaye Afande Sele kutawazwa kama mshindi na kuwa mfalme wa rhymes, huku ushindi wa pili ukienda kwa Inspector Haroun na ushindi wa 3 wakichukua akina Mandojo na Domokaya!

Ushindi huu ulipingwa na watu wengi kuanzia watu wa kawaida mpaka wasanii wenyewe!!

Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli"

Solo Thang akuishia hapo, katika wimbo wa Traveller anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo sele"

Fid Q naye katika Mwanza Mwanza aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"

Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu!!

Sasa ni takribani miaka 12 imepita toka Afande Sele atangazwe kuwa mfalme wa rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano alikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kunakoitwa kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi!!

Je Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes? Kama hakustahili nani alipaswa kupewa hilo taji?

Asante sana.Je kwa mtazamo wako nani alistahili
 
Mimi nilikuwa East Coast Team.Nakumbuka jinsi Wakina GK na AY walivyomsindikiza jukwaani FA , yani ilikuwa kama jukwaa limevamiwa na wanajeshi
Walee jamaa walikuwa ni shida sana kwa wakati ule .Walifanya vizuri sana ila sijuw jini gani aliwaingia kundi likamwagika
 
Mzee iko hivi
Kwa wakati Ule nyimbo aliyoingia nayo afande ktk hicho kinyang'anyiro ilikuwa ni mtazamo na prof jay aliingia na msinitenge
Darubini Kali ilitolewa lakini sio nyimbo aliyokuwa nominated ktk hayo mashindano
Ila baada ya kushinda mashabiki wakaomba ipigwe darubini Kali na ikawa inarudiwa mara kwa mara
Mzee mwenzangu hebu tuwekane sawa mtazamo imetoka mwaka gani na darubini kali imetoka mwaka gani?
Nakumbuka mkali wa ryhmes afande sele aliperfom darubini kali.
Kidhati kabisa afande sele alistahili.
 
That's is not the issue...mzee baba angeweza kusikikiza na kuandika pumba...jamaa alistahili tukubali hilo
Alistahili professor Jay. Afande alikua anaujua fika uwezo wa professor, hata wakati wa kurecord 'mtazamo' afande alifuta original verse yake baada ya kuisikiliza verse ya professor Jay.
 
Back
Top Bottom