Truths
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 1,494
- 1,504
Kwa taarifa yako.Ndio ukweli ulivyo kwa sasa.
Ilinichukua muda kwenye miaka ya 2010 wakati huo Wasanii hawa wawili wakiwa katika ushindani mkubwa.
Ilinipa wakati mgumu kutambua ni nani, yupi mkali juu ya mwingine.
Kwa sasa siumizi kichwa tena.
Joh kaonesha njia kwa FID Q, amechoka, hana mpya, haimbi HIP HOP kwa sasa..
Ubishi wa nani zaidi umemalizwa.
Wote ni marapa wagumu.
fid Q ana video Mbovu kuliko JoE Makini.
Fid Q habadiliki (ni orthodoxy rapper)
wakati Joe Makini anajua kubadilika Hivyo hatabiriki kirahisi style yake.
Maudhui:-
Fid Q anasoma vitabu Sana. Ujumbe wake unapatikana kwenye vitabu zaidi. Mfano albamu ya Kitaolojia (Theology).
Joe makini ni simple mind. Ujumbe wake ni wa kitaa zaidi ukilenga maisha ya starehe na Burudani.
Wote wana mikito ambayo haijawahi kuchosha masikio mpaka leo.
Pamoja na mchanganuo huu bado sijajua kipi cha kuwalinganisha.