Hapa mtabishana mpaka kesho, ni lazima ujue kazi za hizo taasisi mbili yaani jeshi na idara ya usalama wa taifa. Kazi za jeshi zinajulikana na wengi, za usalama je? Ukisoma sheria iliyounda idara ya usalama wa taifa, Tanzania intelligence &, security services act ya 1996 section ya 1 mpaka ya 5 inaeleza majukumu ya idara. Na moja ni kutafuta, kuchambua na kutunza taarifa zote muhimu popote zilipo.
Hii ina maana kwamba TISS wanafuta information popote, iwe ni bungeni, kijiweni jeshini nk. Kazi hii inaweza kua kupitia 'deep cover' au 'undercover informers' kwahyo usishangae kuona wamepenyeza watu jeshini au sehem yoyote ile. Kwa sura ya nje ni kweli CDF ni mkubwa sana kuliko viongozi wengine wa ulinzi na usalama, hata kiprotocal pia. Ila ukiingia kiundani kdg utakuta hata uteuzi wa CDF ni baada ya file lake kupita Tiss na wao kutoa mapendekezo msidhani jeshi halina control, kuna watu wanaliangalia kwa karibu mno ili kulinda usalama wa nchi.
Tiss wanadominate kwenye kila kitu, iwe uchumi, siasa, utawala nk. Wao wanatakiwa kutambua na kuzuia athari yoyote inayoweza kuikuta nchi. Tiss wakifeli hapo na taifa linakua dhaifu.
Ukweli ni kwamba ile taasisi ni 'dubwana' kubwa sana lililojificha chini ya neno 'taasisi' lakini kazi zake zipo hata kwenye vijiwe vya bodaboda au kanisani. Wakati wa kumuapisha Diwani Athumani, kama DGIS mpya, hayati Magufuli aliongea statement tata kwa CDF kua ''kuna watu pale jeshini anawaona wadogo kicheo ila wanaweza kumzidi kimadaraka", na akamaliza kwa kusema "that's how government work"