Mlinzi hawezi kumiliki nyumba, japo umempa mamlaka ya kulinda kufuli lako unapokuwa umelala, ramani ya nyumba yako unaijua wewe, taarifa za familia yako unazo wewe, mpaka taarifa za idadi ya hao wanaokulindia nyumba yako unazo wewe,
ndio inafikia hatua ukihisi Ulinzi wa mwenye kichwa Cha familia hautoshi wewe ndio unaetafuta mlinzi wa kuongeza nguvu na kuimarisha Hali ya usalama,
Kuna wakati unawaambia walinzi wako wawatrain watoto wako, Kuna wakati unawapa heshima walinzi wa nyumba yako ili tu uwe salama na walinde wajua kuwa wao ndio wenye mamlaka ya geti, lakini haimaanishi wao ndio wajuzi sana isipokuwa mamlaka ya wanayoyafanya Ni Mali yako wewe, ilitakiwa uilinde familia yako mwenyewe, wao wanakuwakilisha tu..ukiamua kuwabadili pia unaweza.
Tembelea hata ferry, mlinzi ana mamlaka kuliko hata meneja pale wakati hata taarifa tu za makusanyo ya siku hajui, lakini akikaa getini unaweza kuhisi yeye ndio mnunuzi wa kivuko.