Bukwabi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 3,352
- 1,148
watakiona cha mtema kuni
Teh teh teh! Na cha moto pia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
watakiona cha mtema kuni
Nawauliza wadau wa mpira au TV yoyote hapa nchini mechi hiyo, tv ipi itaoneshwa live
KiliLager.com
================
UPDATES
VIKOSI VYA LEO YANGA VS SIMBA
YANGA:
Deo Dida
Abdul Juma
Oscar Joshua
Nadir Haroub
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
Haruna Niyonzima
Emerson Roque
Simon Msuva
Kpah Sherman
Coutinho
SIMBA:
Ivo Mapunda
Nassor Chollo
Mohammed Hussein
Hassan Isihaka
Juuko Murishid
Jonas Mkude
Rama Singano
Awadh Juma
Elius Maguri
Simon Sserunkuma
Emmanuel Okwi
Dk 2, Okwi anapiga mkwaju wa faulo lakini unadakwa vizuri na Dida.
Dk 3, Yanga wanafanya shambulizi, Sherman anampa pasi nzuri Msuva anapiga shuti linadkwa na Ivo
Dk 5, Sserunkuma Jr anatolewa nje anatibiwa baada ya kugongwa na Yondani
Dk 7, Sherman anawachambua mabeki watatu wa Simba lakini anashindwa kumalizia
Dk 11 Emerson anapiga krosi safi lakini Coutinho anaukosa mpira
Dk 13 vurugu zinazuka, lakini mwamuzi anachukua maamuzi magumu na kutotoa kadi...ubabe unatawala
Dk 17, Okwi anawachambuamabeni wawili wa Yanga lakini anaangushwa na kuwa faulo, anaipiga Okwi...goal kick
Dk 23, Sherman anagongeana vizuri na Msuva na kutoa pasi nzuri....lakini hakuna mmaliziaji
Dk 25 Sherman anampa pasi nzuri Msuva naye anaachia shuti kali lakini linapiga nyavu za nje.
GOOOOOOOOOOOOO DK 30, Awadhi Juma anauwahi mpira wa faulo wa Okwi na kuukwamisha wavuni ilikuwa ni baada ya Dida kuutema.
Dk 33, Coutinho anapiga shuti saafi lakini linatoka nje sentimeta chache
Dk 40, Yanga wanamtoa Twite aliyeumia, nafasi yake anachukua Hassan Dilunga
GOOOOOOOO Dk 41 Maguri anaifungia Simba bao baada ya kuunganisha mpira wa kurusha wa chollo ambao uligonga mwamba, mabeki wa Yanga wakazubaa, akarudi na kufunga tena.
MAPUMZIKO
Yanga wanamtoa Coutinho wanamwingiza Danny Mrwanda
Dk 46 Simba wanamtoa Murishi wanamwingiza Joseph Owino
Dk 48, Msuva anapiga shuti kali lakini mpira unazuiwa
Dk 49, Sherman anawaacha mabeki wa Simba, wanamuangusha, inakuwa faulo inayookolewa na mabeki wa Simba
Dk 52 Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Messi Singano. Simba bado wanatawala katikati ya uwanja
Dk 56, Yanga inamuingiza Salum Telela na kumtoa Mbrazil, Emerson
Dk 63, Mliberia Sherman anatoka nje mwenyewe baada ya kuumia. Awali alirudi, lakini anaonekana kuzidiwa
Dk 65 Yanga wanamuingiza Mrisho Ngassa kuchukua nafasi ya Mliberia Sherman aliyeumia
Dk 66, Mrwanda anapiga mpira langoni kukiwa na mabeki tu, Owino anaruka juu na kuokoa kwa kichwa.
Dk 65, Simba wanamtoa Tshabalala Mohammed Hussein aliyeumia, nafasi yake inachukuliwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya'
Dk 72, Simba wanamtoa Messi na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dk 76, Ngassa anapiga krosi lakini inaishia mikononi mwa Ivo Mapunda
Dk 78 Yanga inamtoa Juma Abdul na kumuingiza Javu
Dk 84 Simba wanamtoa Maguri, nafasi yake inachukuliwa na Danny Sserunkuma. Mwamuzi anampa Maguri kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 86, Simba wanamtoa Simon Sserrunkuma na kumuingiza Shabani Kisiga
Dk 87, mashabiki Yanga wanaanza kutoka uwanjani, Simba wanawazomea
Dk 89, Mrwanda anaangushwa, Niyonzima anapiga lakini Ivo anadaka kiulaiiinii
Zimeongezwa dakika nne.
Mpira umekwishaaa!
Full time: Yanga 0-2 Simba.
kwa mkopo au niwa siku zote..
Mlokole wacha uoga. Jitokeze utetee ulichoandika. Mdomo mrefu ukikojolewa kimyaaaaaa kama umekunywa gundi.
muulize anajua maana ya simba ?
simba ni moto,simba mfalme,simba ndo kila kitu
yanga ndala nadhani unajua ni muhimu ila haina thamani
pole sana mkuu ndio mchezo tu huo..
Asante sana Mkuu. Mimi siumii kufungwa bali naumia maamuzi mabovu kiasi kile nadhani Jamal Malinzi na safu yake ya uongozi wanatakiwa kutambua kuwa mechi ya Yanga na Simba siyo ya kujifunzia kupuliza kipenga, kama huyo dada wanampenda ni vyema wakampeleka 'Sheraton' badala ya kumpa mechi kubwa kama ile hata kama ni ya mchangani.
Niko disappointed sana na mchezo wa jana!
Asante sana Mkuu. Mimi siumii kufungwa bali naumia maamuzi mabovu kiasi kile nadhani Jamal Malinzi na safu yake ya uongozi wanatakiwa kutambua kuwa mechi ya Yanga na Simba siyo ya kujifunzia kupuliza kipenga, kama huyo dada wanampenda ni vyema wakampeleka 'Sheraton' badala ya kumpa mechi kubwa kama ile hata kama ni ya mchangani.
Niko disappointed sana na mchezo wa jana!
haha.. barafuyamoto jibu la swali lako hilo hapo
Ila ndugu yangu, magoli yale hayahusiani kabisa na refa kuchemsha, au yale mliokosa wala hayahusiani na refa. Ni kosa lipi ambalo jana lilikuwa kubwa la kuigharimu yanga upande wa refa?
Asante sana Mkuu. Mimi siumii kufungwa bali naumia maamuzi mabovu kiasi kile nadhani Jamal Malinzi na safu yake ya uongozi wanatakiwa kutambua kuwa mechi ya Yanga na Simba siyo ya kujifunzia kupuliza kipenga, kama huyo dada wanampenda ni vyema wakampeleka 'Sheraton' badala ya kumpa mechi kubwa kama ile hata kama ni ya mchangani.
Niko disappointed sana na mchezo wa jana!