Mkuu hiyo ni mechi ya watani wa jadi, si kila anayezimia ni mwanayanga, wengine ni wanasimba wanavaa jezi za Yanga, Simba kishinda wanajifanya kuzimia ili kunogesha ushindi wao. Tumewashtukia maana hili tukio la kuzimia limechukua kasi katika hizi mechi za hivi karibuni.
Na mimi najiandaa kuvaa jezi ya Simba katika mechi zijazo, siku Yanga ikishinda ni lazima Simba wanibebe kwa machela maana ni lazima nizimike kabisa wala siyo kuzimia tu! Si unakukumbuka kale ka usemi, siyo kila king'aacho ni dhahabu.