Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nasikia alikuwaga babu yangu ila baada ya kutusua akampiga pin bibi na kuoa mwinginee.Mwenye ndondoo za mzee wetu huyu marehemu atushushie..inasemekana alikuwa mfadhili wa TANU..na tajiri wa kariakoo.
Mkristu Mkatoliki. Kanisa ni Chuo cha UongoziNimeweka mkristu kusudi tuu..ili wakija wale wanaotuaminishaga Uhuru walidai wazee wa mitaa wa gerezani tuu kariakoo wasome
Hivi usipoongelea dini yake huridhikiMwenye ndondoo za mzee wetu huyu marehemu atushushie..inasemekana alikuwa mfadhili wa TANU..na tajiri wa kariakoo.
Mleta mada anamuongelea Rupia,wewe unaongelea Lupia,nafikiri mnaongelea koo mbili tofautiKuna ukoo wa Lupia huko Tabora, wana macho makubwa kidogo pia ni waongeaji sana,
Bila shaka itakuwa ni sehemu ya familia yake,
Ila hawa nnao wajua mimi wanamaisha ya kawaida sana,
Wengi ni walimu.
Rekebisha hilo neno, badala ya MKRISTU andika MKRISTO. kuna tofauti kubwa sana kati ya mkristU na mkristO. Ova
Mzee mudi wa saigon.Aliekwambia alikuwa tajir WA kwanza mweusi kariakoo ni nani!?
Jamaa mduanzi sanaSioni sababu kuandika 'mkristu'
Waja watageuza mjadala kuwa wa dini badala ya kile ulichokusudia.
Wakusoma,Mwenye ndondoo za mzee wetu huyu marehemu atushushie..inasemekana alikuwa mfadhili wa TANU..na tajiri wa kariakoo.
Abdulwahid, Nyerere, Dossa Aziz na Rupia walikuja uwanja wa ndege kuupokea ujumbe wa TAA toka kwenye mkutano mkuu wa vyama vya siasa vya Afrika ambao kamwe hawakuhudhuria. Makao makuu ya TAA yalikuwa yakifuatilia matukio nchini Rhodesia ya kusini na kaskazini kwa fazaa. Gazeti la Tanganyika Standard lilikuwa na haya ya kueleza:Wakusoma,
Unahitaji nondo za Mzee John Rupia...
Nondo hizi kama unavyoziita zimo katika kitabu cha Abdul Sykes:
Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie. Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.