Nani mwenye historia ya John Rupia, Mwana TANU na tajiri wa kwanza mweusi mitaa ya Kariakoo?

Nani mwenye historia ya John Rupia, Mwana TANU na tajiri wa kwanza mweusi mitaa ya Kariakoo?

Abdulwahid, Nyerere, Dossa Aziz na Rupia walikuja uwanja wa ndege kuupokea ujumbe wa TAA toka kwenye mkutano mkuu wa vyama vya siasa vya Afrika ambao kamwe hawakuhudhuria. Makao makuu ya TAA yalikuwa yakifuatilia matukio nchini Rhodesia ya kusini na kaskazini kwa fazaa. Gazeti la Tanganyika Standard lilikuwa na haya ya kueleza:

Reuter imearifu kwamba Itla Ung, mjumbe wa Burma katika Umoja wa Mataifa, amewasili Lusaka kuhudhuria mkutano mkuu wa vyama vya kisiasa vya Afrika, ambao unatafuta njia za kuimarisha ‘’harakati za kitaifa,’’ katika nchi husika za Afrika.
TANU ilihitaji takriban shilingi elfu kumi na mbili kumwezesha Nyerere kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa, New York. Kamati ya Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes ilikuwa imekusanya kiasi cha fedha kutoka majimboni ambacho kilitumika katika ile safari ya Ally na Phombeah kwenda kwenye Pan African Congress mjini Lusaka. Kilichosalia hakikutosha kumpeleka Rais wa TANU, Nyerere Amerika. Ilibidi fedha za ziada zitafutwe kutoka kwa wananchi ili kumwezesha Nyerere kufanya safari hiyo. John Rupia alichangia zaidi ya theluthi moja ya fedha zilizotakikana.
 
TANU ilihitaji takriban shilingi elfu kumi na mbili kumwezesha Nyerere kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa, New York. Kamati ya Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes ilikuwa imekusanya kiasi cha fedha kutoka majimboni ambacho kilitumika katika ile safari ya Ally na Phombeah kwenda kwenye Pan African Congress mjini Lusaka. Kilichosalia hakikutosha kumpeleka Rais wa TANU, Nyerere Amerika. Ilibidi fedha za ziada zitafutwe kutoka kwa wananchi ili kumwezesha Nyerere kufanya safari hiyo. John Rupia alichangia zaidi ya theluthi moja ya fedha zilizotakikana.
Al Jamiatul Islamiyya haikuwa na jingine isipokuwa kumuomba Idd Faiz asafiri kwenda Tanga na kupata fedha zaidi kutoka huko. Mwalimu Kihere alikuwa tayari amekusanya fedha hizo na alikuwa anasubiri tu zije zichukuliwe na kupelekwa makao makuu. TANU ilipata habari kwamba yeyote ambaye angeenda Tanga kuchukua fedha hizo kwa ajili ya safari ya Nyerere angekamatwa. Kabla ya kuondoka, Oscar Kambona, Katibu Mkuu wa TANU, na John Rupia, Makamo wa Rais wa TANU, walikwenda kuonana na Idd Faiz nyumbani kwake Ilala kumuaga, kumtakia safari njema na kumpa maelezo kwa ufupi. Safari ya kwenda Tanga haikuwa na tatizo lolote, lakini katika wakati wa kurudi basi ambalo Idd Faiz alikuwamo lilisimamishwa njiani Turiani na makachero. Idd Faiz alikamatwa, akavuliwa nguo na kupekuliwa, lakini hakukutwa na fedha. Hili lilimshangaza na kumchanganya yule afisa aliyemkamata kwa sababu walikuwa na taarifa kwamba Idd Faiz alikuwa amechukua fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere kule Tanga. Idd Faiz aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa Dar es Salaam kwa usaili zaidi wakati wote akiwa analindwa na askari wenye silaha. Baadaye Idd Faiz aliachiliwa huru. Zile fedha za TANU zilifika makao makuu ya TANU Dar es Salaam, salama salimini. Zilizokuwa zimepewa kubeba msichana mdogo aliyekuwa abiria ndani ya basi lile alimokuwa Idd Faiz.
 
Mi nilijua we wazijua habari zake kumbe nawe unauliza?
 
umeandika kitu ambacho una uhakika nacho ila kwa kukufumbua macho kabla ya kupata uhuru tulikuwa na watanzania weusi matajiri mmoja wao ni Marehemu Mzee Lupembe wengine wataongezea wanaowafahamu huyu pia alikuwa miongoni mwa watanzania waliomchangia Mw. Nyerere tiketi ya kwenda umoja wa mataifa
...huyo alikuwa wa wapi mkuu
 
TAMBAZA

Mohamed Said January 22, 2018 0


Shajara ya Mwana Mzizima:

''BWANA MKUBWA'' JOHN RUPIA

Na Alhaj Abdallah Tambaza


[https://4]Kushoto John Rupia, Julius Nyerere na Zuberi Mtemvu, nyuma yao ni Bantu Groups walinzi wa viongozi wa TANU
na wahamasishaji, 1955[https://3]Raia Mwema 22-23 Januari 2018


KATIKA ukurasa huu wa Shajara ya Mwana Mzizima, Jumatatu iliyopita, tuliandika kuhusu madhila na manyanyaso waliofanyiwa watu weusi katika taifa hili wakati wa utawala wa kishenzi wa Wakoloni wa Kingereza pamoja na vibaraka wao wa Kihindi waliowaleta hapa kuwasaidia kazi.

Tulieleza kwa kirefu namna sisi, wana wa nchi hii, tulivyobaguliwa katika nyanja mbalimbali kuanzia makazi, ajira, elimu na tiba mpaka ikawa inakera sana kuvumilia hali ile. Hali zetu zilikuwa zinatisha—dhalili kupita maelezo.


Sijui kama watu wa kileo ambao hawakuyashuhudia haya wanaweza kuamini, lakini wakoloni – tena wote Mngereza na Mjerumani— hawakututawala kwa wema na upole, pamoja na kwamba ilikuwa ni sisi tuliochangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi zao kwa jasho na nguvu zetu.


Kwa kutumia ile dhana ya ‘Mercantilism’, ambayo maana yake ni kwamba kwenye makoloni ya Kiingereza, watu walime kwa nguvu sana na kusafirisha malighafi kwa ‘bwana mkubwa’ ambaye atatengenezea bidhaa kwenye viwanda vyake na kuuza kwenye nchi nyingine na yeye kufutika faida yote—wizi mtupu.


Hakuna faida kurudi kwenye koloni au nchi husika kuja kusaidia maendeleo, bali fedha zote zilibaki kwenye himaya ya mtawala. Hapa zililetwa fedha kiduchu sana kwa ajili ya uendeshaji ofisi na kununulia sare za kazi (uniforms), karatasi, penseli, kalamu na vidawati vya wino maofisini mwao.


Elimu ile ya kibaguzi na finyu, ilitolewa katika mazingira magumu sana. Hawakuta kusomesha mtu mazungu yale bali walitaka wasaidizi tu kidogo. Mwandishi huyu, alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Mnazi Mmoja kuanzia mwaka 1958 mpaka 1961 alipohamia shule ya kati ya Kitchwele Boys Middle School mjini DSM, mwaka 1962.


Shuleni tulivishwa magwanda ya khaki ngumu kuanzia kaptura na mashati; yote ni khaki tu bila kujali mji wa DSM una joto sana. Walimu, ingawa wengi walikuwa ni waafrika wenzetu, lakini walifuata maadili na maelekezo ya ‘mabwana wakubwa’ ya kuendesha taasisi zake kibaguzibaguzi.

Pale shuleni Mnazi Mmoja, hatukuruhusiwa kwenda shule tukiwa tumevaa viatu vyovyote hata kandambili! Sheria za shule hazikuruhusu. Ni nini hiyo kama si udhalilishaji, wakati walimu wao wakiwa wamepiga tai, wei kichwani (ni ule mstari unaogawa nywele kichwani mafungu mawili), wakipendeza kama mabwana zao Wazungu.


Kutovaa viatu pale maana yake ni kwamba, hata chooni tulikuwa tukiingia na kupishana hivyo hivyo watoto wote; na miguu yetu ikawa inakumba na kukanyaga vimajimaji vya chooni na haja ndogo kutwa nzima— Subhanallah!


Katika shule hizo, vichocho, visonono na magonjwa mengine ya kuambukiza yalikuwa ni kama kila mtu anaugua wakati wowote. Sasa unapopata ugonjwa huo hapo ni sindano! Sindano! Sindano tu kila siku— kali sana zenye kuleta kichefuchefu, kutapisha na kutia homa. Kila nikikumbuka hapa nasikia uchungu sana, kwani ni mara nyingi sana nimekumbana na kadhia hizo pale shuleni.


Kwenye ajira vilevile, nimeshuhudia watu wazima wakienda maofisini bila viatu. Juu wameweka magwanda yao na soksi ndefu mpaka magotini—viatu usivae ukafanana na mkubwa Mzungu!

Kwenye mchezo wa mpira waliotuletea; wenyewe ukicheza nao wao wanavaa viatu vyenye njumu za kuchoma; wewe pekupeku huku wakikuumiza na misumari kwenye viatu vyao. Kwenye Ligi ya DSM ya Soka, Wazungu walikuwa na timu yao kutoka Gymkhana na Wahindi (Magoa) nao walikuwa na timu ikiwa Goans Institute (ikitamkwa na wenyeji Goanisi)— hata maana yake walikuwa hawajui masikini. Timu hizo zote zilikuwa zikicheza na viatu wanapokutana na Yanga, Sunderland (sasa Simba), pamoja na timu za makuli wa bandarini za Dockyard na Cargo and Handling. Hawa wote wakicheza wamefunga mabandeji miguuni.


Katika timu ya Dar Combine kulikuwa na wachezaji watatu wa ‘daraja za juu’. Sentahafu wa timu ambaye pia ndio kepteni alicheza na viatu; Goalkeaper alikuwa mzungu mmoja mnene ‘tipwatipwa’ akiitwa Mavrodis yeye naye alikuwa na viatu na mwingine Tony Fernandes kutoka Goanisi yeye naye alicheza na viatu.


Waliobaki wote wa wakati huo, pamoja na kwamba walikuwa wanacheza timu moja ya Dar Kombaini walicheza bila viatu na ikaoneka sawa tu! Waafrika weusi; viatu vya nini. Timu ile naikumbuka vizuri sana nikiwa nasoma pale Kitchwele Middle School. Walikuwamo akina Ayoub Mohammed, Ishaka Mzee, Billy Bandawe, Wilcokson, Yahya Mbiki, Lukongo, Chaurembo, Yussuf Mwamba na Waziri.


Mambo hayo na mengineyo mengi tukipata muda tutayaelezea, ndiyo yaliyowasukuma kwa uchungu mkubwa wazee wetu wale wakajiunga pamoja kimyakimya, wakaanda mipango madhubuti kwa hali na mali ili wao— na sisi tujao— tuondokane na mateso yale.


Mmoja katika wazee waliojitolea pakubwa ni hayati Mzee John Rupia. Huyu ‘Bwana Mkubwa’ wetu, wakati wa ukoloni hakuwa lofa hata kidogo. Alimiliki majumba hapa mjini, mashamba makubwa kule Mbagala na Kigamboni, malori ya kusomba mawe, kokoto na mchanga pamoja na machimbo ya mawe kule Kunduchi kukiitwa Maweni.


Mzee Rupia alijihusisha na biashara nyingine nyingi sana. ‘Bwana Mkubwa’ yule hakuwa na shida ya fedha ndogo wala kubwa. Kwa kiasi fulani aliishi kama wale jamaa wengine wa madaraja ya pili (Wahindi) na la tatu (Waarabu).


Mzee John Rupia asili yake ni Msukuma wa maeneo ya Mwanza, lakini aliishi hapa Mzizima kwetu kwa miaka mingi toka utotoni kwake hivi; na hivyo kuwa sehemu ya historia ya mji huu. Alikuwa mmoja wa Waswahili wa mwanzo kabisa kujenga mjengo wa ghorofa katika makutano ya Barabara ya Kitchwele (sasa Uhuru) inapokutana na Msimbazi. Kwa wakati ule halikuwa jengo la kuchezea. Lipo pale mpaka leo likisomeka kama Rupia Building. likiwa limesheni maduka ya biashara na ‘flats’ za kukaa watu juu ghorofani.


Mwenyewe, kabla ya uhuru akikaa Mtaa wa Ndanda pale Misheni Kota akila, akinywa, akilala na kushuhudia maovu yote ya Wazungu Waingereza akiwa na nduguze watu weusi. Baadaye alikuja kuishi maeneo ya Upanga karibu na Makao Makuu ya Jeshi na Ofisi za Takukuru. Sasa nini basi ‘Bwana Mkubwa’ yule alichofanya kusaidia harakati?


Japo si kwa wingi unaostahili, lakini habari zake hivi karibuni zinatajwa, zinaandikwa, zinazungumzwa na kutathiminiwa na wanaharakati mbalimbali wa historia iliyofichwa ya ukombozi wa taifa hili na washiriki wake waliofanya makubwa na mazito. Kitabu mashuhuri cha Mwanahistoria maarufu nchini, Sheikh Mohammed Said, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes, The Untold Story of the Muslim Struggle against Colonialism in Tanganyika,’’ kinachosambazwa na Ibn Hazm Media Centre, kimemtaja Mzee John Rupia kwa mapana na marefu. Msomaji kisome ujionee mwenyewe. Tusiandikie mate na wino upo.


Alikuwamo katika kuasisi na kuanzisha AA, TAA, TANU ambapo alishiriki vizuri katika baraza maarufu la wazee wa TANU wakati huo akiwa pamoja na kina Mzee Mwinyikambi, Tambaza, Mshume, Chamwenyewe, Haidar Mwinyimvua na Rajab Diwani. Kubwa ni kwamba walipotoka TAA na kuanzisha TANU, ‘Bwana Mkubwa’ Rupia alitwishwa mzigo wa kuwa Makamu Mwenyekiti wake chini ya uongozi wa Julius Nyerere, akiwa na kadi namba 7.


Tofauti na makamu wengine wa vyama kwa sasa wenye kulipwa mishahara na pensheni; kulipiwa nyumba na mashangingi ya kutembelea; kulipwa mamilioni ya posho za vikao; kulipwa mamilioni wanapotembelea mikoani kwa shughuli za chama; kuwa na wasaidizi na makatibu kibao wa kumfanyia yeye kazi zake. Rupia hakuwa hivyo kwenye ‘chama chake’ kichanga cha TANU.


Anatajwa kuwa ndiye aliyekuwa mfadhili namba moja kwa kukiendesha na kukikuza chama cha TANU. Mishahara na posho akijitolea mfukoni; alimlipia sehemu kubwa Mwalimu Nyerere katika safari yake mashuhuri ya Umoja wa Mataifa kwenda kuelezea dunia kwamba Watanganyika walikuwa tayari kujitawala. Alimnunulia suti za kuvaa safarini na kumpa pesa za kujikimu Mwalimu akiwa kule Marekani. (Angalia: Gazeti la Jamhuri www. Jamhurimedia.co.tz: Alikuwa nani katika maisha ya Mwalimu Julius Nyerere).


Mzee John Rupia ni baba mzazi wa Balozi Paul Rupia aliyepata kuwa Balozi Marekani, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika uongozi wa Alhaji Mwinyi na Ben Mkapa. Balozi Rupia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Dar es Salaam.


Watoto wengine wa Mzee John Rupia ni Alban Rupia (sasa marehemu) na mfanyabiashara maarufu jijini Stephen ‘Mpuya’ Rupia ambaye kwa kiasi fulani ndiye mwendeshaji wa shughuli za kibiashara za marehemu babake. Msomaji ukitaka kumfahamu vizuri ‘Bwana Mkubwa’ wetu huyu John Rupia, mwenye historia ya kutukuka katika taifa letu, basi mwangalie mwanawe Stephen Rupia. Mwana Mzizima huyu amepita mlemle mwa babake kwa upendo, bashasha, huruma, maingiliano miongoni mwa jamii na mambo kama hayo.


Nilimjua Mpuya kwenye miaka ya 70, sote tukiwa vijana wadogo tukifanya kazi katika Idara ya Usalama wa Anga (sasa TCAA) kwenye ‘marehemu’ Jumuiya ya Afrika Mashariki ya zamani, yeye akiwa Radar Engineer aliyehitimu Urusi; na mimi nikiwa Aeronautical Telecommunications Officer. Mpaka hii leo tumeendelea kuwa masahiba wakubwa wa kufa na kuzikana.


Sasa basi, wakati huu tukiwa tunamtazama na kumtathimini ‘Bwana Mkubwa’ huyu aliyejitolea kwake na kwetu, ili tuwe tulivyo leo, tuangalie namna ya kuutambua mchango wake kwa kutoa jina lake kwenye moja ya barabara kubwa za hapa kwao DSM.


Mbona Yusuf Makamba kapata heshima kwa kuwa Mkuu wa Mkoa tu bila kuacha haiba yeyote ile. Mbona Pius Msekwa kapata heshima ya kupewa Msekwa Hall kwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Spika wa Bunge tu? Tusiache wapite hivi hivi; tutakosa utu!


Simu: 0715 808 864; atambaza@yahoo.com.
 
uhuru wa nchi umedaiwa na wakristo wawili tu Kambarage na Rupia no more
Nimemuona japhet kirilo hapo...ila huyu kuna kipindi alikuwa anataka mamlaka kamili ya nchi ya wameru..kama ilivyokuwa kwa marialle na mamlaka kamili ya chaggas.

Hebu nisaidie hapo kunisahihisha.
 
Alikua mfadhili wa TANU Enzi za mkoloni halafu Wakoloni wala hawakutishia biashara zake; walijali uchumi if I'm not mistaken, sijui kwanini wakoloni weusi hawa wakisikia tu mtu awe na mapenzi tu na upinzani, lazima biashara zake ziingie matatizoni, hawajali uchumi, wanajali chama chao tu!
 
Nimemuona japhet kirilo hapo...ila huyu kuna kipindi alikuwa anataka mamlaka kamili ya nchi ya wameru..kama ilivyokuwa kwa marialle na mamlaka kamili ya chaggas.

Hebu nisaidie hapo kunisahihisha.
kwa kauli ya Mwl ambayo speech yake ipo hadi leo anasema hivyo hao unaowataja sio uhuru wa nchi bali makabila yao au wawe na nchi yao out of Tanganyika. hawakudai uhuru wa Tanganyika bali wa himaya zao.
 
kwa kauli ya Mwl ambayo speech yake ipo hadi leo anasema hivyo hao unaowataja sio uhuru wa nchi bali makabila yao au wawe na nchi yao out of Tanganyika. hawakudai uhuru wa Tanganyika bali wa himaya zao.
Kuweka kumbukumbu sawa, hao wazee walifika UN kudai mamlaka kamili ya Maeneo yao Kabla ya JK. So wakagonga mwamba.

Ndipo alipotokea JK na TANU kudai uhuru wa Tanganyika wakampa support. Umeona michango ya wadau Kwamba alichangia Zaidi ya theluthi ya pesa ya kwenda UN. Hapo unasema hakutoa mchango wa kuikomboa Tanganyika?
 
Kuweka kumbukumbu sawa, hao wazee walifika UN kudai mamlaka kamili ya Maeneo yao Kabla ya JK. So wakagonga mwamba.

Ndipo alipotokea JK na TANU kudai uhuru wa Tanganyika wakampa support. Umeona michango ya wadau Kwamba alichangia Zaidi ya theluthi ya pesa ya kwenda UN. Hapo unasema hakutoa mchango wa kuikomboa Tanganyika?
Mzee Rupia hakwenda UNO kudai uhuru wa Wasukuma, yeye alichangia zaidi ya Theluthi ili Mwl Nyerere akadai uhuru wa Tanganyika.
 
Leo hii nyumba ya familia ya mjane wa Balozi John Rupia inapigwa mnada na benki moja nchini.Ni jambo la kusikitisha kwa sababu mjane huyo bado anaishi katika nyumba hiyo iliyo mkabala na Coco Beach Dar es salaam
 
Back
Top Bottom