Nani mwenye makosa kesi hii ikiwekwa mezani?

Nani mwenye makosa kesi hii ikiwekwa mezani?

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Nipo kwenye kampuni fulani, kila siku nakusanya cash ifikapo jioni nafunga hesabu zangu namkabidhi boss.shida ni kwamba boss ajawahi kuhesabu pesa ninazompa kila siku, ukifika mda wa makabidhiano utasikia tu nakuamini weka kwenye droo, Mimi akinambia hivyo naziweka lakini moyoni silizikagi na jibu lake nimesoma uhasibu hata yeye pia ni mhasibu, sasa nashangaa mambo yake yakutohakiki pesa anapopewa.

Binafsi naonaga ni vizuri kukabidhiana pesa kimahesabu,sasa nilimpa miamala kama minne milioni NNE zilikuwa mbili, na milioni tatu na point zilikuwa mbili, by then miamala ilikuwa ya siku NNE, sasa cha kushangaza siku ya tano kazibeba pesa kama zilivyo bila kuzihesabu,zikaenda kuhesabiwa huko huko bank na mtu wa bank,anarudi toka bank ananiambia 60000/= (sitini elfu haipo) katika zile pesa nilizomkabidhi, Mimi nilibaki kumshangaa tu nikamwambia boss Mimi sielewi pesa zote zilikamilika na kila pesa niliitenga kwenye bahasha yake na kuandika Amount niliyoipata kwa siku.

Hiyo loss nashindwa kuelewa imetokea wapi. Boss mvivu sana kwenye kurudia kuhesabu pesa,sasa nimemshauri anunue machine ya kuhesabia ili kuepuka mambo kama aya!!!!! Alinistress mood yote ya kazi ikaisha hadi Leo, akili haijakaa sawa, kwasababu pesa nilihesabu vizuri kila pesa ilitimia na sikugawa ata senti, hadi Leo hii sijaelewa hiyo loss ya elfu sitini imetoka wapi. Je, Sitini elfu niilipe Mimi?

Wakati pesa nilishamkabidhi boss lakini hakuzihesabu, kama nilivyowaelezea hapo juu,Angehesabu siku ile ile ya makabidhiano angeniambia pesa haijatimia ningemuelewa.lakini pesa nimekupa juzi ujahesabu Leo unaniambia haijatimia kweli jamani?

Mimi simuelewi boss mwezenu kuhusu hii loss, eh wana sheria nisaidieni hapa kwa mnavyoona nyie kutokana na maelezo aya nani mwenye makosa hapa?
 
UNGEMWAMBIA AHESABU TU MAPEMA HELA HAINA UNDUGU MKUU
My dear ata umlazimishe vipi atakuambia amechoka hawezi kuhesabu ,yeye kila siku mwendo ni huo huo weka kwenye droo hapendi mambo ya kuhesabu pesa by hands si umeona ata siku ya mwisho kaenda kumuhesabia mtu wa bank.alipoenda kui deposit? Kwanini asingehesabu kabla ajaenda bank.
 
Boss sio mvivu anakuamini. Na kuthibitisha hilo anaoption mbili.
1: Kuendelea kukuamini na hiyo kesi airusishe bank au ajisingizie mwenyewe.

2: Kuanzia sasa hii itumike kama kesistadi ya yeye kuanza kuhesabu pesa kabla hazijahamia kwenye himaya yake.
Au mnunue kale kamashine ka kuzihesabu.
 
  • Hela nyingine zinalindwa na midukule, ukiiba tu nyota yako inakwrnda kutumika kwa bosi.
  • Utajiri una siri nyingi.
Kabisa
Tulifanya kazi kwa muarabu fulani....kila tukipiga jangusho...tunapata hela halafu hakuna cha maana tunafanya...na mwezi huo mwarabu ndio anapata faida balaa.
 
My dear ata umlazimishe vipi atakuambia amechoka hawezi kuhesabu ,yeye kila siku mwendo ni huo huo weka kwenye droo hapendi mambo ya kuhesabu pesa by hands si umeona ata siku ya mwisho kaenda kumuhesabia mtu wa bank.alipoenda kui deposit? Kwanini asingehesabu kabla ajaenda bank.
Huyo ni boss mpumbavu pamoja na kwamba ana hela mpaka amekuajiri! Hiyo hasara mwambie ni ya kwake! Akiendelea kugoma kuweka mashine wiki ijayo chukua milioni kwenye hiyo hesabu na hiyo hasara mwambie ni ya kwake!
 
Akufukuzae hakwambii toka, boss ana lake jambo anaanza kukutengenezea mazingira ya kukuondosha.
 
Ulikosea toka mwanzo kukubali awe anachukua hela bila kuhesabu na wew hukujihami kwa maneno mapema...!! pole sana mambo ya hela magumu.. mwambie kwa sasa kama hatahesabu hela bhasi kwa upotevu wowote hutahusika
 
Huyo anakuchora tu, anacheza na saikolojia yako

Anafanya hivo ili hata siku moja usithubutu kuiba hata mia yake, pesa ipo kamili.
 
Back
Top Bottom