Nchi za Italy, Sweden, Belgium, Uingereza n.k zenye taasisi madhubuti za serikali kuu zenye makatibu wakuu wa mawizara na viongozi wa serikali za majimbo / serikali za mitaa madhubuti zinaweza kuendelea na kuendesha nchi hata miaka 3 na zaidi bila ya kuwa na waziri mkuu na baraza la mawaziri.
Nchi zenye taasisi dhaifu zisizokuwa huru na maafisa wakuu wa serikali makada (mfano CCM) kama makatibu wakuu na viongozi wa halmashauri za wilaya dhaifu ndiyo hutegemea jeshi la mtu mmoja yaani ulazima wa uwepo wa rais mtendaji au mkuu wa serikali waziri mkuu ili kazi ziendelee .
Mfano katiba ya nchi kumrundikia rais au waziri mkuu kuteua makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa ndani ya mawizara, wakurugenzi watendaji wa miji, halmshauri n.k ni kutengeneza taasisi hizo kuwa dhaifu.
Hii hupelekea Wateuliwa wa rais kukosa ubunifu, kushindwa kushauri, kuto kutoa nafasi ya ushiriki-mawazo wa raia na kubwa kukosa uwezo wa kufanya maamuzi makubwa kwa faida ya raia wa nchi na taifa lao maana wanangoja maelekezo ya rais ameagiza nini ametoa tamko gani, ameshauri nini n.k .
MALUNDE
https://www.malunde.com › 2021/08
rais samia ateua wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ,jiji, miji ...
2 Aug 2021 — Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendji wa Halmashauri za Jiji, Miji, Manispaa , wilaya