Nani mwenye shaka juu ya demokrasia ya nchi za Magaharibi hasa baada ya Waziri Mkuu Uingereza kujiuzulu?

Huwezi kuelewa kwa sababu unamshabikia Xi Jinping rais wa milele.
Hakuna demokrasia hapo bali ni uozo mtupu, lazima kiongozi utatue matatizo ya wananchi wako sio kuya kimbia kwa kigezo cha kujihuzuru.

:Rundo la Watanzania wajinga ni mtaji wa wanasiasa mafisadi wa hii nchi [ Ccm, Chadema, Nccr, Act, Cuf n.k ]
 
Tofauti iliyopo n kwamba, huko Magharibi wao wanaingia madarakani wakiweka kichwani kwamba wanakwenda kuwatumikia wananchi na nafasi hiyo inaweza kuchukuliwa na mtu yoyote muda wowote. Huku kwetu hiyo ndio Ajira yake, hawezi kuwajibika akifikiria maisha yake baada ya hapo
 
Labda niongeze kitu kuwa Liz ni waziri mkuu wa nne wa Uengreza kujiuzulu ndani ya kipindi cha miaka minne.
Your browser is not able to display this video.
 
Taasisi madhubuti hutokana na watu/wananchi imara na wanaojielewa katika kudhibiti viongozi.
Watawala wengi wa kiafrika huteua chawa/mbwa wao kusimamia taasisi.
Utamaduni huu husababisha wananchi wengi kuamini kuwa ili uchaguliwe au kuteuliwa lazima ujipendekeze kwa viongozi na matokeo yake nchi humilikiwa na viongozi ambao pia kwa sababu ya tabia ya uchawa wao kabla hawajawa viongozi, hujikuta wakijifanya chawa wa mataifa makubwa.
Ili kuondokana na hali hii, ni lazima wawepo wananchi watakaojitoa mhanga kudhibiti viongozi ili nchi zirudi mikononi mwa raia.
Ni lazima kuwezesha wananchi wazawa kiuchumi bila kuwapa uongozi wa kisiasa ili waweze kuilinda nchi kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Viongozi wengi wanaotokana na uchawa hawawezi kuilinda nchi na hata kumsaidia mwananchi wa kawaida.
 
Udikteta au umwinyi ??! Yaani udikteta au Ufalme !! = my take Dikteta hamuogopi MTU bali yeye ndio anaogopewa kwahiyo kila MTU atatimiza wajibu wake au anaondoka kwenye nafasi !! Mfalme naye hamuogopi MTU yeyote maana Nchi ni yake na watu ni watu wake !! Hafikirii uchaguzi wala nini yeye anataka aone nchi yake na watu wake wananawiri na wanamtukuza mtukufu Mfalme !! Kwisha habari yake !!
 
Maneno mazito !!
 
Mkuu wala usipate shida au kuumiza kichwa kwa sababu ya matendo maovu na low performance za watawala wa Afrika. Hawa sio viongozi bali ni wachumiatumbo wakubwa. Utasubiri hadi Yesu anarudi humuoni mchumiatumbo hata mmoja akijiudhuru hata kwa unafiki tu.
 
Duh !! Hatar sn !
 
Kigezo number moja cha wapiga kura wa United Kingdom kwenye uchaguzi mkuu ni trust ya kiongozi wa chama. Huyo mtu anayo majibu pasi na shaka ya kutatua changamoto zao hilo halina mjadala.

Majibu wanayotaka watu kwa sasa ni uchumi (mainly cost of living) sasa wewe ndani ya siku 45 umebadili sera zako zote za uchumi energy price freeze, 45p tax, umesababisha interest rate kupanda na kuwapa wakati mgumu wanaolipa mortgages, umefukuza waziri wa uchumi, umefukuza waziri wa mambo ya ndani kwa sababu isiyo ya msingi; to name a few of her backtracking decisions.

Unadhani mtu kama huyo jamii ya waingereza itamuamini kweli kama awezi kusimamia sera zake, maamuzi yake na wala sio muangalifu kwenye teuzi zake.

Uingereza hizi wizara tatu mambo ya nje, mambo ya ndani na fedha ni muhimu sana kwenye siasa zao (wanaziita great offices) wewe kwa mara ya kwanza katika historia yao hizo wizara ujaweka mzungu ata mmoja.

Isitoshe upande wa pili wana shadow chancellor ambae ni mchumi wa kweli mwenye uwezo wa kuigaragaza serikali kwa hoja ukimpa chancellor dhaifu.

Kwakuwa uingereza awachagui PM directly wao wanachagua wabunge tu ukifikisha 360 (kama sijakosea) kiongozi wa chama husika ndio PM, ila kiongozi wa chama ana aminika vipi kwenye jamii ni big issue kwenye kupiga kura (kwao mmbunge uitaji porojo nyingi) kwenye uchaguzi chama kikishakupitisha.

Uchaguzi aupo mbali busara na huruma ya Liz Truss kwa wabunge wenzake ambao wangepoteza viti ni bora aachie, walau she is not selfish kama ilivyokuwa kwa Jeremy Corbyn wakati labour leader sera zake zilikuwa mbovu, aaminiki na wapiga kura lakini ataki kuachia nafasi matokeo yake aliwapotezea wenzake majimbo mengi sana ambayo yalikuwa Labour safe seats. Liz Truss doesn’t want that route.

There is more than democracy kuondoka kwake mambo ni mengi including aina ya wanachama wa conservative (wabunge) kuwaridhisha wote ni ngumu. Ni hivi siasa za uingereza ni complicated zaidi ya democracy hao conservatives wenyewe vary in ideologies ndani ya chama kimoja.
 
Etwege na Magonjwa Mtambuka watabisha. Kwao demokrasia ni kuunga juhudi
 
Yana ukweli na uzito wa kijisahihisha kiafrika zaidi, kwa faida ya wote.
Tatizo wengine ukiwaambia ukweli unakuwa ni Adui yao !! Watakuja banyamulenge wa kukudhuru au kukutusi !!
 
Katika yote uliyoandika sijaona demokrasia imeingiaje hapo


Labda utupe maana yako ya demokrasia
 
Hao wanaofuata Demokrasia wanajiweza kiuchumi. Tofauti na Afrika kiongozi anatafuta madaraka ili iwe ni channel ya kula keki ya Taifa,wenzetu wanatafuta madaraka kutengeneza heshima kwenye Taifa na ikitokea watu hawamkubali inakua rahisi kujiuzulu.
 
Nchi kuwa unstable na uongozi ndo demokrasia?.. kiongozi anapimwaje Kwa mwezi mmoja Tu?..ni upumbavu mtupu
Uongozi si sehemu ya kumpima mtu, sio sehemu ya majaribio.
Sababu ina effect moja kwa moja kwa watu na maisha yao.
Ukizingua hata uko na siku moja, uondolewe au ujiondoe. Ili mradi sheria na kanuni mlizojiwekea zinafuatwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…