Kwa suala la uimbaji wa muziki wa injili wote uliowaandika wanaimba vizuri, na mchango wao ni mkubwa katika "kuelimisha na kuonya pia. " Ni kazi ya injili hiyo.
Ila ukiniuliza nani ni greatest, tuache chuki binafsi, siwezi kuacha kumtaja "Rose Muhando." Huyu mwanamke ndiye aliyeutangaza muziki wa injili si Tanzania tu, mpaka Congo, Rwanda, Burundi, Kenya na nchi zingine za kusini mwa Africa nyimbo zake zilipigwa. Ndiye aliyewavutia wanamuziki wa nje km Angela Chibalonza (RIP) kujua muziki wa injili una soko na unalipa na kuamua kuja Tanzania.
Ametengeneza soko la ajira kwa wanamuziki wengine, she really created a way for others & she deserves credit for that.
Je wajua? Rose Muhando ndiye mwanamuziki pekee Tanzania ambaye nyimbo zake zilipigwa kila sehemu; Makanisani, baa, kule kwenye kumbi za video (vibanda umiza), sherehe, hata wenzetu waliweka km milio ya simu, hasa ule wimbo wa "Nibebe." nk
Yote ni heri, lakini SIFA kuu zimfikie ROHO anayewasaidia.