Nani mwingine analichukia jina lake?

Nani mwingine analichukia jina lake?

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2020
Posts
653
Reaction score
1,698
Sipendi kusikia jina langu linatajwa. Hata mtu akiniuliza ninaitwa nani natamani nimdanganye. Maana sijisikii poa kulitamka jina langu. Bora kuliandika na sio kutamka. Nikilitamka najiona sijui natamka kitu gani. Hadi pumzi zinakata.

Baby alinitaja jina langu kwenye sita kwa sita nilishtuka kama vile sio jina langu[emoji23][emoji23][emoji23]. Hadi hamu ikakata. Nilijua hili tatizo ninalo mimi tu, ila leo nimegundua ni tatizo la wengi. Usimlaumu mtu akikudanganya jina, kuna wengine hatuyapendi.

Haya, mlale salama.
 
kuna mwana kutoka familia ya kilokole wamempa jina la TUOMBE ni muhuni aliye pindukia afu ni mgomvi kinyama hakawii kuanzisha ugomvi

jamaa kafika umri flani sasa hataki kuitwa hilo jina amejichagulia jina lake eti GERALD sasa we bugi muite jina lake la zamani

sijui expectation za wazazi zililenga nini walidhani atakua mcha mungu kama wao sijui
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
mi nalipenda jina langu sema kuna mtu alinipaga nickname nikatokea kuipenda na ikapendwa zaidi basi mpaka leo nickname yangu ndo inajulikana sana kuliko jina langu
Ukijitambulisha kwa mtu mpya ni jina gani unapenda kumpa? Hiyo nickname ? Au jina la kweli?
 
Umenikumbusha muigizaji mmoja bongo anaitwa NDUMBANGWE MISAYO. Aisee nawaza hivi ilikuaje akapewa hilo jina.
 
Jina langu ni unique na ni amaiz, sijui wazazi wangu walitoa wapi yaan. Daaah a [emoji178] ma name

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mimi jina langu nalipenda ila huwa nalitamani jina la dada yangu
 
Back
Top Bottom