Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
Mfano umepanga Kukutana na mtu ambaye humjui sura kwa jambo la msingi Stend ya Mabus ya Magufuli,Mbezi.
Baada ya kupanga kuwa mtakutana pale, ghafla ukapoteza simu na namba yake huijui.
Kwakua tayari mlikuwa mmepanga kuonana unaamua kwenda tu.
Baada ya kufika, unakuta kuna watu wengi, mwenyeji wako humjui sura wala mavazi ila jina tu.
Unaamua kupaza sauti na kuita Jina ili uone nani atageuka, unamuuliza mtu mmoja mmoja kama ni yeye mmepanga kukutana.
Sasa, hapo kuna mambo mawili, moja watu watakuona huna akili timamu, chizi hujielewi, pili itakua ngumu kumpata huyo mtu.
Kwenye Biashara, ni muhimu kumjua mtu/mteja unayemlenga.
Hakuna bidhaa au huduma ya kila mtu.
Iwe unauza mtandaoni au kawaida unapaswa kujua kuwa sio kila mtu ni mteja wako.
Unapaswa kutambua bidhaa au huduma yako vizuri na tambua nani atakua mteja wako, Usipoteze muda kumlenga kila mtu.
Usipoteze nguvu kwa kila mtu, Tambua ni nani uliyemlenga. Wasio na uhitaji na chako si wateja wako.
USITAPETAPE KWA KILA MTU
MBINU ZA KUTAMBUA MTEJA WAKO
1. TAMBUA BEI YA BIDHAA AU HUDUMA ZAKO
Kwa jamii nyingi hasa zetu Waafrika, mara nyingi tunanunua vitu kulingana na bei. Ndio maana jambo la kwanza tukienda dukani huwa tunaulizia bei na si ubora. Kama Unauza bidhaa ya bei kubwa ni muhimu pia kulenga wateja wanaomudu bei hizo.
2. UHITAJI
Utagundua kuwa karibia kila kitu ulichonunua ulikua na uhitaji nacho. Hivyo hivyo kwenye biashara yako ni muhimu sana kulenga watu wenye uhitaji na bidhaa au huduma yako.
Usilenge kuwauzia Mitumbwi watu wa Dodoma, hawana uhitaji nazo.
3. Wapi wateja wanapatikana
Siku hizi watu wengi tunatangaza kwenye mitandao ya kijamii. Ni ajabu kukuta mtu analipa matangazo ya kulipia lakini hajui wateja wake wako wapi.
Unapaswa kujiuliza kwanini kuna supermarket nyingi mikocheni, Posta, oysterbay, Msasani kuliko Buza, Vikindu, maji chumvi Nk.
Wapi wateja wako wapo.
4.5.6. Ni mbinu gani huwa unatumia kujua wateja wako ni wapi?
#kelvinkibenje #begood #masoko