Nani wa kulaumiwa kati ya wazazi au watoto ikiwa nyumbani kwa wazazi kuna hali duni?

Nani wa kulaumiwa kati ya wazazi au watoto ikiwa nyumbani kwa wazazi kuna hali duni?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huwa kunakuwa na maneno mengi sana kwa watu wanaoishi mjini wakiwa na mafanikio hata kidogo huku nyumbani kwao kukiwa bado duni mfano bila nyumba nzuri ya wazazi.

Hiii hutokea rafiki zao wanapofika nyumbani kwao kwa sababu mbalimbali lakini hasa wakati wa msiba, hapo utasikia

"Huyu jamaa anakula bata tu mjini wakati hajajenga hata kwao",

Katika hali hii kwa nini watoto wanalaumiwa na kudharauliwa badala ya wazazi ambao ndio mji wao hasa na wao ndio walipaswa kujenga??
20241025_002858.jpg
 
Kama mtoto ana uwezo wa kuboresha hali ya maisha ya nyumbani kwao kijijini kwao ni vyema na ni busara ,pia ni heshima na ni sifa njema pia ni baraka.
JAMII ina standards zake au tuseme morals au matarajio,jamii inatarajia mtoto akifanikiwa aboreshe hali ya nyumbani kwao,awe msaada.Na hii ndio normal.Ukifanya jambo ambalo jamii inatafsiri ni jema inaonekana ni kawaida na inaonekana umetimiza wajibu.
Ila ukifanya jambo ambalo jamii haikutegemea ulifanye inakuwa si kawaida abnormal na hapa unaoneka hujatimiza wajibu.
MAONI YA JAMII AU JUDGEMENT ZA JAMII
Hizi huwezi kuzizuia chochote unachofanya kikiwa kizuri chema jamii inaweza ikanyamaza kwa sababu ni kawaida ndio tuliumbwa na maadili yanatutaka tufanye hivyo,tena unaweza hata usisifiwe wala kupewa hongera kwa kufanya mema mana ni kama kitumiza wajibu wako.
Ila ukifanya kinyume na matarajio ya jamii au ukifanya baya kwa mtazamo wa jamii hapa ndio sasa itakulaumu,hata jamii yako isipokutamkia bayana ila ndani ya mioyo yao tayari wanakunungunikia au wanakuhukumu.
 
Huwa kunakuwa na maneno mengi sana kwa watu wanaoishi mjini wakiwa na mafanikio hata kidogo huku nyumbani kwao kukiwa bado duni mfano bila nyumba nzuri ya wazazi.

Hiii hutokea rafiki zao wanapofika nyumbani kwao kwa sababu mbalimbali lakini hasa wakati wa msiba, hapo utasikia

"Huyu jamaa anakula bata tu mjini wakati hajajenga hata kwao",

Katika hali hii kwa nini watoto wanalaumiwa na kudharauliwa badala ya wazazi ambao ndio mji wao hasa na wao ndio walipaswa kujenga??
View attachment 3134987
Wazazi wazazi wazazi wazazi threads close
 
Kwa uzoefu wangu kama mchaga, unatakiwa upachukulie kwa wazazi kama nyumbani kwako hata kama umeacha kuishi hapo.

Kwahiyo upatapo mafanikio, unatakiwa upaboreshe kadri uwezavyo.

Sasa watu wakiona una nyumba nzuri halafu kwenu pabaya, watakushangaa.
Hawawezi kuona unaishi kwa shida hujiwezi kisha wakulaumu unapasahau nyumbani.
 
Umenena vyema mkuu.
 
kuwajali wa nyumbani kwenu ni baraka ,wengine ndio lengo letu kubwa la sisi kupambana huku mjini ni ili tubadilishe/turekebishe/tuboreshe hali ya nyumbani kwwtu,tuweke heshima nyumbani,tuonyeshe kuwa wazazi wetu hawakukosea kutuzaa na kutulea.Tuwape matunda ya kazi yao ya kutulea watufurahie sisi matunda yao na sisi tuwafurahishe na tuwaheshimishe.
Wengi wetu tukifika mjini tunaweka heshima mjini kwa anasa na starehe tunawatelekeza na kusahau nyumbani na kuwasahau wazee wa nyumbani kwetu.

Siku ikitokea tatizo ndio unakumbuka nyumbani au siku ikitokea msiba watu uliotoka nao mjini hata kama ulikuwa unawapa ofa za bia za lete kama tulivyo
wakifika na hata wafanyakazi wenzako au marafi au hata mpenzi wako,akifika kijijini kwenu akapaona hujapaboresha hupapa/kupa heshima hujapaheshimisha kama ulivyojiheshimisha mjini.
NI RAHISI KUJISHUSHIA HESHIMA ,hata wasipokwambia ila moyoni ,au wakikaa pembeni wana weza wakawa wana ku diss.(dharau) au wengine utawashangaza kwa sababu wengine hawakutegemea sio kawaida ,kuwa hutapajali nyumbani kwenu kwa kiasi hicho
Tena kwa baadhi ya makabila hata baadhi ya wachaga KUBORESHA nyumbani ni kama utamaduni mzuri waliojiwekea.
Baadhi ya makabila au watu wapo radhi hata kuwakataa wazazi au ndugu zao au kabila lao au kupakataa kwao au kupadharau kwao.
MKATAA KWAO MTUMWA.
 
Attachments

  • Screenshot_20241025-204401.jpg
    Screenshot_20241025-204401.jpg
    81.2 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241027-212004.jpg
    Screenshot_20241027-212004.jpg
    82.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom