Wazazi wazazi wazazi wazazi threads closeHuwa kunakuwa na maneno mengi sana kwa watu wanaoishi mjini wakiwa na mafanikio hata kidogo huku nyumbani kwao kukiwa bado duni mfano bila nyumba nzuri ya wazazi.
Hiii hutokea rafiki zao wanapofika nyumbani kwao kwa sababu mbalimbali lakini hasa wakati wa msiba, hapo utasikia
"Huyu jamaa anakula bata tu mjini wakati hajajenga hata kwao",
Katika hali hii kwa nini watoto wanalaumiwa na kudharauliwa badala ya wazazi ambao ndio mji wao hasa na wao ndio walipaswa kujenga??
View attachment 3134987
Umenena vyema mkuu.Kwa uzoefu wangu kama mchaga, unatakiwa upachukulie kwa wazazi kama nyumbani kwako hata kama umeacha kuishi hapo.
Kwahiyo upatapo mafanikio, unatakiwa upaboreshe kadri uwezavyo.
Sasa watu wakiona una nyumba nzuri halafu kwenu pabaya, watakushangaa.
Hawawezi kuona unaishi kwa shida hujiwezi kisha wakulaumu unapasahau nyumbani.