Nani wa kusimama badala ya wapinzani wanapoumizwa na maamuzi ya viongozi wao?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Leo nimekuja na swali mahususi kwa wapinzani lakini pia linaweza kuulizwa hata kwa CCM ikiwa nao wataanza kurithi tabia hii ya wapinzani ya kususa.

Watu wana ndoto na mipango wanapojiunga na siasa na kwa siasa zetu zinafanyika kupitia vyama hivyo ninaweza kusema ndoto na mipango ya kisiasa ya wanachama ipo mikononi mwa vyama vyao.

Hili lilikuwa ni wazo zuri sana kwamba siasa zinatakiwa kuratibiwa kupitia mfumo rasmi ambao ni vyama.

Miaka ya karibuni jambo hili limegeuka suala linalohitaji mjadala wa kina na tusije zalisha mgogoro mbeleni.

Kutokana na uhitaji wa wanachama kutaka kugombania nafasi mbalimbali na ikatokea viongozi wakagoma kushiriki. Je, nani wa kusimama nao wanapoumizwa na maamuzi hayo?
 
1.soma katiba ya chama husika
2.nenda mahakamani kama hujaridhika
3.Hama chama
Katiba ya nchi inatakiwa isimame badala ya katiba ya chama chochote.

Kuna mifumo mingi inayolinda haki za msingi za kikatiba za mwanachama. Yawezekana nasema tena yawezekana wale Wabunge 19 wana haki.

Uamuzi wa kuhama chama ni kuonesha tamaa ya uongozi. Ni vema wakapambana humohumo
 
Kama katiba ipo na inafuatwa vema.Tambua tena kuna mambo mtambuka ambayo hufanya kuleta maamuzi ya dharula/suluhisho la wakati huo.Kubaki unang'ang'aniza lifanyike utakalo wakati walio wengi hawaafiki ni ukengeufu.Ni aidha ujumuike nao au ushike njia yako nyingine.
 
Katiba ya nchi inatakiwa isimame badala ya katiba ya chama chochote.

Kuna mifumo mingi inayolinda haki za msingi za kikatiba za mwanachama. Yawezekana nasema tena yawezekana wale Wabunge 19 wana haki.

Uamuzi wa kuhama chama ni kuonesha tamaa ya uongozi. Ni vema wakapambana humohumo
nenda nao mahakamani hao ambao hawajaridhika.
 
Leo nimekuja na swali mahususi kwa wapinzani lakini pia linaweza kuulizwa hata kwa CCM ikiwa nao wataanza kurithi tabia hii ya wapinzani ya kususa.

Watu wana ndoto na mipango wanapojiunga na siasa na kwa siasa zetu zinafanyika kupitia vyama hivyo ninaweza kusema ndoto na mipango ya kisiasa ya wanachama ipo mikononi mwa vyama vyao.

Hili lilikuwa ni wazo zuri sana kwamba siasa zinatakiwa kuratibiwa kupitia mfumo rasmi ambao ni vyama.

Miaka ya karibuni jambo hili limegeuka suala linalohitaji mjadala wa kina na tusije zalisha mgogoro mbeleni.

Kutokana na uhitaji wa wanachama kutaka kugombania nafasi mbalimbali na ikatokea viongozi wakagoma kushiriki. Je, nani wa kusimama nao wanapoumizwa na maamuzi hayo?

Unataka wapinzani wasisuse, ila waendelee kushiriki kwenye mambo kihuni huku wafuasi na wanachama wake wakibambikiwa kesi, kuachwa na vilema vya maisha hata kuuwawa, lengo ni kuipa uhalali ccm isiokuwa nao. Mwanachama asiyekubaliana na msimamo wa chama anaweza kuhamia chama kingine, au kuanzisha chama kitakachoendana na matamanio yake binafsi.
 
Back
Top Bottom