Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,424
Ninavyoona hii michango ya harusi ni mnyororo wa kutajirisha watu tu kwa kisingizio cha kuwanufaisha/ kusherehesha wanaharusi.
Kiukweli, mnyororo huu itabidi ifike wakati uvunjwe (kama sio kizazi hiki basi kijacho) kwani kamwe haupo kwa maslahi ya wanaharusi kama inavyodhaniwa na wengi, zaidi unawaacha wanaharusi na ndugu wa karibu na mizigo ya madeni isiyomithilika.
Najua povu litakuwa jingi hapa na pengine kwa tulipofika ni ngumu kuuvunja mnyororo huu hasa kwa sababu wafaidika ni wengi na kumejengeka mazoea kuwa ndo kitu "kilichozoeleka".
Kiukweli wanaofaidika ni hawa:
(i) Ma-MC
(ii) Wapambaji maharusi na kumbi
(iii) Wenye kumbi za harusi
(iv) Wapiga picha za mnato na za kutembea
(v) Wasafirishaji wa maharusi na wageni waalikwa
(vi) Waleta misosi
(vii) Waleta vinywaji
(viii) Madensa, waimbaji na wachekeshaji
(ix) Waleta vifaa kama viti, majamvi n.k
(x) Wanakamati
(xi) Waleta vipazasauti & muziki
(xii) n.k.
Sent using Jamii Forums mobile app