Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,795
Tsh laki moja inanunua mifuko sita ya cement pamoja na usafiri.. Ukiweza kuchangia harusi kumi basi hiyo ni mifuko 60 inayoweza kufyatua tofali 2,000 za block.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili ni suala la principle na utamaduni.Unaanza wewe tu kukataa kuchangia watu na ikifika zamu yako hawakuchangii basi inakuwa umekata mnyororoNinavyoona hii michango ya harusi ni mnyororo wa kutajirisha watu tu kwa kisingizio cha kuwanufaisha/ kusherehesha wanaharusi.
Kiukweli, mnyororo huu itabidi ifike wakati uvunjwe (kama sio kizazi hiki basi kijacho) kwani kamwe haupo kwa maslahi ya wanaharusi kama inavyodhaniwa na wengi, zaidi unawaacha wanaharusi na ndugu wa karibu na mizigo ya madeni isiyomithilika.
Najua povu litakuwa jingi hapa na pengine kwa tulipofika ni ngumu kuuvunja mnyororo huu hasa kwa sababu wafaidika ni wengi na kumejengeka mazoea kuwa ndo kitu "kilichozoeleka".
Kiukweli wanaofaidika ni hawa:
(i) Ma-MC
(ii) Wapambaji maharusi na kumbi
(iii) Wenye kumbi za harusi
(iv) Wapiga picha za mnato na za kutembea
(v) Wasafirishaji wa maharusi na wageni waalikwa
(vi) Waleta misosi
(vii) Waleta vinywaji
(viii) Madensa, waimbaji na wachekeshaji
(ix) Waleta vifaa kama viti, majamvi n.k
(x) Wanakamati
(xi) Waleta vipazasauti & muziki
(xii) n.k.
Sent using Jamii Forums mobile app