Nani wa kuvunja mnyororo wa michango ya harusi?

Tsh laki moja inanunua mifuko sita ya cement pamoja na usafiri.. Ukiweza kuchangia harusi kumi basi hiyo ni mifuko 60 inayoweza kufyatua tofali 2,000 za block.
 
Hili ni suala la principle na utamaduni.Unaanza wewe tu kukataa kuchangia watu na ikifika zamu yako hawakuchangii basi inakuwa umekata mnyororo
 
Kwa sie wengine fungulia mbwa tunazama mwishoni kula na kucheza singeli.. Tujuane..

Yaani ntafanya makosa yote ikiwemo hilo la kuchangia. Lakini la kuondoka bila kula hilo siwezi kosea
 
MaMC kujeni hapa. Maghorofa mengi mliyojijengea yanatokana na michango ya harusi. Gharama zenu hazipungui shilingi milioni moja na hazikatwi kodi kabisa! Kwa mwezi mmoja mnaingiza si chini ya milioni nne. Vivyo hivyo kwa Wapishi, Video Shooters na wote ambao hutoa huduma katika sherehe hizi. Niliwahi kumsikia MC Pilipili akitamba kuwa yeye bila ya milioni mbili hawezi kusherehesha katika harusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…