Nani yupo nondo kati ya alie fanya Masters au aliesoma vitabu vingi kwenye eneo husika?

Nani yupo nondo kati ya alie fanya Masters au aliesoma vitabu vingi kwenye eneo husika?

Kwa mfano mtu alie fanya Masters in Psychology vs mtu alie soma let's say vitabu elfu moja about psychology. Nani anakuwa nondo zaidi katika kwenye eneo husika la kitaaluma kwenye nyanja hiyo ya Psychology.
Si swali lenye jibu la moja kwa moja(one way traffic). Kuna mambo mengi ya kuyahusisha ili kufikia mwafaka.

Na hapo ndo majibu yatawategemea wahusika kwenye elimu. Kuna sababu za ndani ya mhusika na nje ya mhusika:

1: Njia ya kusoma kwa mhusika ni kwa mapenzi yake/anaimudu au ni baada ya kuwepo vikwazo vya kupata elimu kwa njia nyingine? Je amejikubali huko aliko?

Hii itapelekea mhusika kuweza kuyachukua maarifa kikamilifu.

2: Upatikanaji wa viinilishe/contents vya elimu husika/relevance ya anachokisoma.

3: Uwezo wa uchukuaji wa materials husika na ku-internalize elimu husika.
Una uwezo wa ku-extract knowledge/theme?

Mfano: uwezo wa kumsikiliza kocha na kufanya anachotaka na zaidi kwa wenye uwezo binafsi au kushindwa kufikia maelekezo.

4: Taranta ya mhusika inaendana na elimu husika aliyoipata. Kuna watu wanaweza kuwa na elimu nzuri na uelewa mzuri lakini kwenye kazi husika anahangaika/strugle kwa kuwa kule alipo si eneo lake la msingi.

Mfano: ni kama wacheza mpira, waliokuzwa kwenye academy na mtu mwenye taranta yake watahitaji nguvu tofauti kuwafikisha kwenye viwango vya mafanikio yaliyo bora.
 
Kwa mfano mtu alie fanya Masters in Psychology vs mtu alie soma let's say vitabu elfu moja about psychology. Nani anakuwa nondo zaidi katika kwenye eneo husika la kitaaluma kwenye nyanja hiyo ya Psychology.
Aliye nondo ni yule anayetumia elimu ndogo kwenye hio fani kutatua matatizo ya jamii yake.
Mfano ingawa Nigeria ina wasomi wengi wenye master na PhD kuliko Tunisia na Morocco ila Morocco na Tunisia ipo nondo kuliko Nijeria.
Ingawa Zanzibar inaongoza kufelisha matokeoya form four na six kuliko Kagera ama Kilimanjaro ila Zanzibar ipo nondo/smart kuliko Kagera na Kilimanjaro.
Narudia tena Anayetumia elimu ndogo aliyonayo kutatua changamoto na kuboresha maisha yake,ndio yupo nondo
 
Si swali lenye jibu la moja kwa moja(one way traffic). Kuna mambo mengi ya kuyahusisha ili kufikia mwafaka:

1: Njia ya kusoma kwa mhusika ni kwa mapenzi yake/anaimudu au ni baada ya kuwepo vikwazo vya kupata elimu kwa njia nyingine? Je amejikubali huko aliko?

Hii itapelekea mhusika kuweza kuyachukua maarifa kikamilifu.

2: Upatikanaji wa viinilishe/contents vya elimu husika/relevance ya anachokisoma.

3: Uwezo wa uchukuaji wa materials husika na ku-internalize elimu husika.
Una uwezo wa ku-extract knowledge/theme?

Mfano: uwezo wa kumsikiliza kocha na kufanya anachotaka na zaidi kwa wenye uwezo binafsi au kushindwa kufikia maelekezo.

4: Taranta ya mhusika inaendana na elimu husika aliyoipata. Kuna watu wanaweza kuwa na elimu nzuri na uelewa mzuri lakini kwenye kazi husika anahangaika/strugle kwa kuwa kule alipo si eneo lake la msingi.

Mfano: ni kama wacheza mpira, waliokuzwa kwenye academy na mtu mwenye taranta yake watahitaji nguvu tofauti kuwafikisha kwenye viwango vya mafanikio yaliyo bora.
Nondo ni yule anayeleta matokeo na mabadiliko kwenye jamii kupitia knowledge aliyoipata.

Tunapima kwa results - Matunda!!
Unaweza ukasomea halafu no Impact.
Unaweza ukasoma vitabu na ukaleta Impact.
 
Nondo ni yule anayeleta matokeo na mabadiliko kwenye jamii kupitia knowledge aliyoipata.

Tunapima kwa results - Matunda!!
Unaweza ukasomea halafu no Impact.
Unaweza ukasoma vitabu na ukaleta Impact.
Ndiyo.
Je njia ya kupata maarifa inaweza kujisimamia kwa mtu huyo kuwa nondo?
 
Ukiongelea nondo kwenye hayo mambo mawili unagusia umahiri japo hili swala limekuja kitaaluma basi tutajibu kwa namna hiyo.

Masters degree yaani shahada ya uzamili huwa inatolewa ama kutafutwa na mtu anaetaka ajikite kwenye uwanda fulani ila kwa utafiti wa kina lakini ambao matokeo yake si mapya sana kwenye eneo husika la kiutafiti japo matokeo hayo yanaweza leta mabadiliko fulani kwenye eneo analofanyia utafiti ama kazi

Mfano; anae chukua masters ya uchimbaji wa madini ni eneo pana sana, lakini utakuta mmoja shahada yake ya uzamili yaani masters amejikita kwenye aina za udongo na namna zinavyo badilika mpaka kumuwezesha mtaalamu kutambua wamefika sehemu ambayo ni rahisi kupata madini fulani

Sasa ukija kupata madini kuna mwingine ata specialize yaani atabobea kwenye aina ya madini fulani kutokana na udongo fulani lakini huyu atakuwa na uelewa ama maarifa zaidi juu ya madini na udongo unao zunguka madini husika lakini kuna mwingine alitambua mabadiliko ya udongo jinsi unavyo enda chini mpaka wakafika hapo kwenye mwamba wenye madini

Huo ni mfano naimani umeelewa

Sasa ukija kwa mtu anaesoma vitabu itategemea yeye anasimama katika angle gani maana masters ni lazima uwe na area of research na uwe umeshalisoma vya kutosha ukimaliza una andika kitu kinaitwa thesis yaani yalio fanyiwa utafiti huko nyuma na yanafanana na ya kwako yalifanywaje na matokeo yalikuwa yapi na wewe uliona lipi halikuweza kufanyika umelifanya kwa namna ipi na matokeo yalikuwa ni yapi na lina mchango gani kwenye mazingira ya sasa je umetatua shida fulani katika eneo lako la kitaaluma na wengine wanaweza endelea ulipo ishia au ndio mwisho na kipi unadhani haujaweza kufanya ila kinaweza fanyika?

Sasa kama mwingine anasoma madini kwa juu juu na kuyafahamu kwa uchache sidhani kama atayajua kwa undani kama yule anae tenga muda wake kusomea kitu hicho kwa miaka miwili, mitatu na sehemu nyingine masters mpaka miaka minne

Nakaribisha maswali.
 
Kusoma ni mfumo wa utaratibu na nidhamu na kufuata ratiba ya masomo research mitihani na masomo yanayohusiana na taaluma yako, mkulima atasomea pia mambo ya biashara ya kilimo, mazingira fani mbadala pia atapata miongizo ya sera za serikali kuhusu hiyo fani, unaweza kuwa fundi mzuri lakini ukashindwa kuiuza taaluma yako, sawa na kuwa na aplication nzuri lakini window yako ipo slow hakuna update n.k kwahiyo ninashauri mtu akasone kwenye taasisi rasmi aanze na vitabu vilivyoainishwa kwanza ndipo aendelee kusoma vitabu vingine, cheti ni pongezi kwa kupoteza muda wako na kuweza kuendana na ratiba na kukidhi vigezo complucated
 
Ndiyo.
Je njia ya kupata maarifa inaweza kujisimamia kwa mtu huyo kuwa nondo?
Hapana mpaka maarifa hayo yawe yamepimwa na yaonekane yana uelekeo wa kubadili akili na tabia za watu kwasababu siyo kila kilichoandikwa ni maarifa vingine hisia.

Kuitwa nondo na watu wengi si kigezo cha kuwa na maarifa ya kweli, mda mwingine ni umaarufu tu.
Umaarufu unaweza kutokana na mzungumzaji kuibua hisia kali bila kutoa solution mfano watu Wanaogusa dini, siasa na mila huvutia hisia, lakini mara nyingi hawabadili maisha ya watu sababu hujikita kwenye kusimulia au kukosoa zaidi.

Maarifa ya kweli hupimwa kwa matokeo, na siyo makelele. Tusimlinganishe mtu anayeibua mijadala na yule anayeponya akili, nafsi na tabia hatakama katulia kimya mfano Dr. Ellie Waminian.
 
Kusoma ni mfumo wa utaratibu na nidhamu na kufuata ratiba ya masomo research mitihani na masomo yanayohusiana na taaluma yako, mkulima atasomea pia mambo ya biashara ya kilimo, mazingira fani mbadala pia atapata miongizo ya sera za serikali kuhusu hiyo fani, unaweza kuwa fundi mzuri lakini ukashindwa kuiuza taaluma yako, sawa na kuwa na aplication nzuri lakini window yako ipo slow hakuna update n.k kwahiyo ninashauri mtu akasone kwenye taasisi rasmi aanze na vitabu vilivyoainishwa kwanza ndipo aendelee kusoma vitabu vingine, cheti ni pongezi kwa kupoteza muda wako na kuweza kuendana na ratiba na kukidhi vigezo complucated
This is very useful.
 
Kwenye ligi kama hizi huwa tunawapima kwa matokeo kwa jamii - matunda.

Hivyo waliosomea wanatupiga gap tuliookota okota vitabuni.
Sisi tutakua wanoma kwenye kuongea wao wanakua wanoma kwenye kutekeleza.

Anayeongea na anayetekeleza kwa vitendo nani mnoma!?
Unakuwa unasoma huku unafanyia kazi,mfano umesoma kuhusu human behaviour unaweza kwenda kuangalia na kanza ku predict action za watu mi nahisi kati ya watu 50 ishirini unaweza uka predict vizuri,

Ila challenge inakuja kwenye uandishi mwingi wa vitabu unatokana na research za watu wa magharibi na asia mara nyingi wanaongea lugha za ulaya, kichina, japan na lugha chache za middle east ila sidhani kama wanafanya kwa kutumia lugha za afrika na wanasema asilimia kubwa lugha unayoongea ina shape ufikiri wa mtu hivyo unaweza kutumia mbinu ambazo hazita kuwa na effect kubwa kwa lugha za afrika
 
Nondo ni yule anayeleta matokeo na mabadiliko kwenye jamii kupitia knowledge aliyoipata.

Tunapima kwa results - Matunda!!
Unaweza ukasomea halafu no Impact.
Unaweza ukasoma vitabu na ukaleta Impact.
Kwa namna hii ukisema neno kuleta mabadiliko kwenye uwanda wa utafiti tunaongelea uwe na results yaani matokeo yalio kuwa na mkakati, mchakato wa kufanyika, mpaka kupata majibu husika kwenye hilo eneo, na kwa namna hiyo mtu wa masters anaweza kuwa na impact yaani athari nzuri kwenye eneo lake.

Lakini hii Itachangiwa na taasisi anayo soma, supervisor anae msimamia, na uwezo wa kitivo chake (college) kulipia machapisho yaani publications (publication fee), na hapa unakuta andiko moja linaweza lipiwa mpaka million 7 kwenye magazeti (journals) za kawaida ila maarufu na nyingine zinaweza gharimu mpaka 42 million kulipia tuu taarifa yako ya kiutafiti ipate nafasi ya kuandikwa kwenye kurasa za haya magazeti yaani a research work to be published via a certain journal.

Sasa kwa hawa wa kusoma na kisha kuhadithia ni nzuri japo haina mashiko ikifika wakati wa kuwasilisha jambo kwa wabobezi wa eneo hilo ulilosoma kwa sababu mpaka kitu kinaundwa let's say chanjo unakuta kuna wataalamu wamebobea kwenye kuchunguza genes behaviors zikiwa exposed kwenye mazingira tofauti ya kemikali

Na mwingine amebobea namna ya chanjo inavyo undwa hapo tunaweza gusia swala zima la nano technology yaani kwa namna gani dawa inaweka ndani huku nnje kukiwa na kasha lenye udogo zaidi ya punje ya mchanga inaundwa ili iweze kupenya mpaka kwenye cell za mwili

Sasa watu hawa wote wakikutana ndio wanaunda chanjo na wengine sijawataja hapo

Kwahiyo mtu wa masters akipata mazingira sahihi na kwenye swala la utafiti yaani research, haya mazingira sahihi yana jumuisha ni fundings za kutosha, hela iwepo na technologia mengine yatafanyika, na sisi africa nchi yetu ikiwemo tumekosa utendaji ila utafiti wa kusoma Africans wako vizuri mno lakini kwenye mazingira sahihi.
 
Sasa umeandika ujinga gani? Aliefanya masters alikuwa anasoma cherehani au?
 
Unakuwa unasoma huku unafanyia kazi,mfano umesoma kuhusu human behaviour unaweza kwenda kuangalia na kanza ku predict action za watu mi nahisi kati ya watu 50 ishirini unaweza uka predict vizuri,

Ila challenge inakuja kwenye uandishi mwingi wa vitabu unatokana na research za watu wa magharibi na asia mara nyingi wanaongea lugha za ulaya, kichina, japan na lugha chache za middle east ila sidhani kama wanafanya kwa kutumia lugha za afrika na wanasema asilimia kubwa lugha unayoongea ina shape ufikiri wa mtu hivyo unaweza kutumia mbinu ambazo hazita kuwa na effect kubwa kwa lugha za afrika
Sahihi mkuu.
Lakini tukumbuke maarifa hayana mipaka ya lugha.
Sisi tuchukue kinachofaa, tukitumie.
Tukikaa kungoja vilivyoandikwa kwa lugha za Afrika pekee, tutakosa mengi.
Tujifunze kwao, kisha tutengeneza maarifa yetu.
 
Hapana mpaka maarifa hayo yawe yamepimwa na yaonekane yana uelekeo wa kubadili akili na tabia za watu kwasababu siyo kila kilichoandikwa ni maarifa vingine hisia.

Kuitwa nondo na watu wengi si kigezo cha kuwa na maarifa ya kweli, mda mwingine ni umaarufu tu.
Umaarufu unaweza kutokana na mzungumzaji kuibua hisia kali bila kutoa solution mfano watu Wanaogusa dini, siasa na mila huvutia hisia, lakini mara nyingi hawabadili maisha ya watu sababu hujikita kwenye kusimulia au kukosoa zaidi.

Maarifa ya kweli hupimwa kwa matokeo, na siyo makelele. Tusimlinganishe mtu anayeibua mijadala na yule anayeponya akili, nafsi na tabia hatakama katulia kimya mfano Dr. Ellie Waminian.

Suala kubwa ni ubebaji wa maarifa halisia yenye matokeo chanya kwenye jamii na namna ya upatikanaji wake ndo msingi mkuu.
 
Kwa namna hii ukisema neno kuleta mabadiliko kwenye uwanda wa utafiti tunaongelea uwe na results yaani matokeo yalio kuwa na mkakati. Mchakato wa kufanyika mpaka kupata majibu husika kwenye hilo eneo na kwa namna hiyo mtu wa masters anaweza kuwa na impact yaani athari nzuri kwenye eneo lake

Lakini hii Itachangiwa pia na taasisi anayo soma supervisor anae msimamia na uwezo wa kitivo chake kulipia machapisho yaani publications

Sasa kwa hawa wa kusoma na kisha kuhadithia ni nzuri japo haina mashiko ikifika wakati wa kuwasilisha jambo kwa wabobezi wa eneo hilo ulilosoma kwa sababu mpaka kitu kinaundwa let's say chanjo unakuta kuna wataalamu wamebobea kwenye kuchubguza genes behaviors zikiwa exposed kwenye mazingira tofauti ya kemikali

Na mwingine amebobea namna ya chanjo inavyo undwa hapo tunaweza gusia swala zima la nano technology yaani kwa namna gani dawa inaweka ndani huku nnje kukiwa na kasha lenye udogo zaidi ya punje ya mchanga inaundwa ili iweze kupenya mpaka kwenye cell za mwili

Sasa watu hawa wote wakikutana ndio wanaunda chanjo na wengine sijawataja hapo

Kwahiyo mtu wa masters akipata mazingira sahihi na kwenye swala la utafiti yaani research mazingira sahihi ni fundings za kutosha hela iwepo na technologia mengine yatafanyika
Ni kweli kabisa.
Elimu ya kweli huleta mabadiliko pale inapoungwa mkono na mazingira husika.

Kusoma bila kutengeneza mabadiliko ni kama kama yule jamaa aliyekatisha jeshini na gari, akakamatwa, akajaziwa mafuta full tank, akaambiwa azunguke uwanja mdogo mpaka yaishe [Fictious].
Unazunguka tu bila kufika.
 
Suala kubwa ni ubebaji wa maarifa halisia yenye matokeo chanya kwenye jamii na namna ya upatikanaji wake ndo msingi mkuu.
Sahihi Tajiri!
Umaarufu wa kupendwa na wengi si issue. Issue ni kubeba maarifa halisi yenye matokeo chanya kwenye jamii.

Na msingi wa kweli ni namna unavyoyapata hayo maarifa, si kwa kuamini kila unachosoma bali kwa utafiti na tafakari.
 
Kwa mfano mtu alie fanya Masters in Psychology vs mtu alie soma let's say vitabu elfu moja about psychology. Nani anakuwa nondo zaidi katika kwenye eneo husika la kitaaluma kwenye nyanja hiyo ya Psychology.
Kusoma ni kusoma na kote kunaelimisha. Ila kujisomea binafsi hutapewa cheti na itakuwa vigumu kujinadi kuwa una uelewa wa hiyo taaluma.
 
Tofauti, mmoja ana cheti cha kujibu maswali na mwingine ana uelewa kupitia vitabu mbalimbali.

Nb. Mgonjwa anatibiwa kwa ujuzi na si cheti.​
unaweza kuwa na cheti na ukawa na ujuzi pia, watanzania wengi huwa tuna assume mtu mwenye cheti na ana GPA kubwa moja kwa moja alikuwa ana kariri kwenye masomo wala hakuwa ana elewa. Kuna hii comment # 31 kasema ibn unuq

"Kumbukeni kuwa mtu aliyesomea psychology bado anachance ya kusoma na vitabu vingine vingi.

Elimu ya psychology + Vitabu tofauti = Mnoma!!"
 
Sahihi Tajiri!
Umaarufu wa kupendwa na wengi si issue. Issue ni kubeba maarifa halisi yenye matokeo chanya kwenye jamii.

Na msingi wa kweli ni namna unavyoyapata hayo maarifa, si kwa kuamini kila unachosoma bali kwa utafiti na tafakari.

Hili swala ni gumu sana hasa tukienda kwenye msingi wa kuwa nondo kama uelewa/maarifa na uwasilishaji vs uwezeshi/knowledge.

Ili kupima uelewa inabidi upime maeneo mengi kwani inahusisha:
1:Uwezo wa kurudia kitu husika
2: Uwezo wa kutafsiri kitu husika
3: Uwezo wa kutumia maarifa husika
4: Uwezo wa kuchakata/analysis
5: Kujenga hoja za kitaalamu
6: Kufanya upembuzi wa mawazo kwa kutumia taarifa sahihi za kitaalamu kwa vigezo zingatifu.

Ingawa 3 na 4 hubeba uzito zaidi, kama tulivyoainisha kule juu kwenye jamii ya kawaida. Kwa wasomi watakupima pia kwa 5 na 6.

Hivyo, si jambo jepesi hata kwa mifumo ya elimu yenyewe kupima maarifa vizuri ndani ya mtu.
Wakati mwingine hatupimi vs hatupimwi vyema juu ya maarifa waliyonayo watu kwa kuangalia vipengele vichache sana na hii inaweza kutokana na kutokujua au kwa kujua ila uvivu.
 
Back
Top Bottom