Ibn Unuq
JF-Expert Member
- Oct 9, 2020
- 5,508
- 10,086
Mkuu mi naona kama unachanganya maelezo, nakushauri upitie pitie utofauti kati IQ, Emotional, Creative, Practical, Adaptive na Spiritual Intelligencies.Hili swala ni gumu sana hasa tukienda kwenye msingi wa kuwa nondo kama uelewa/maarifa na uwasilishaji vs uwezeshi/knowledge.
Ili kupima uelewa inabidi upime maeneo mengi kwani inahusisha:
1:Uwezo wa kurudia kitu husika
2: Uwezo wa kutafsiri kitu husika
3: Uwezo wa kutumia maarifa husika
4: Uwezo wa kuchakata/analysis
Hivyo, si jambo jepesi hata kwa mifumo ya elimu yenyewe kupima maarifa vizuri ndani ya mtu.
Wakati mwingine hatupimi vs hatupimwi vyema juu ya maarifa waliyonayo watu kwa kuangalia vipengele vichache sana.
Mtoa mada alitaka kujua nani ni Noma zaidi kati ya Msomi wa vitabu na aliyesomea saikolojia - Yaani Adaptive Intelligence.
Kumbuka, vitabu vya saikolojia vimeshapitia hatua ya kupimwa kitaalamu (IQ Test) maana yake ni kwamba kimeandikwa juu ya uelewa uliothibitishwa.
Lakini pia Mtu aliyebobea kwenye saikolojia pia amepitia mitihani migumu ya kiakili (IQ Test) kwa vitendo na kwa nadharia.
Kwa hiyo, maoni yake yana uzito wa kitaalamu pia.
Albert Einstein aliwahi kusema - The Measure of intelligence is the ability to change, Hapa alimaanisha kwamba akili ya mtu siyo kiasi cha mambo anayoyajua tu, bali ni uwezo wake wa kubadilika, kukua, na kubadilisha mazingira au kuwabadilisha watu wengine kwa ufanisi.
Sasa unasemaje maarifa hayapimiki?
Haijalishi umepataje hayo maarifa au uelewa wako ukoje, Haijalishi wewe ni msomi wa saikolojia au msomi wa vitabu.
Kinachozingatiwa ni namna unavyoweza kutumia hayo maarifa kuleta matokeo na siyo kuishia kupiga porojo tu.
Kumbuka mabadiliko ni hali, mabadiliko siyo mali.