Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Pamoja na kuwa Mpoto yuko sahihi, ila nae apunguze unafiki na kujipendekeza sana, pia Afande sele angetutajia walau majina ya wasanii waliondolewa kwenye orodha ya wimbo husika tupate kuwapima kama kweli ni wazalendo au lah
 
Ila hapa mrisho mpoto kajibu kwa akili sana!!!
Mifano hai justify uzalendo wa Bella, angesema Bela amefanya nini zaidi ya wengine. Mrisho Mpoto anachangany kati ya UZALENDO na UMOJA. Ingekuwa ni kampeni ya UMOJA (UNITY) tungewashirikisha watu wa pande zote meaning mataifa mbalimbali......uzalendo una uhusiano wa moja kwa moja na homeland.......Atuambie basi kwanini anathani Bela ni mzalendo kuliko wazawa....
 
 
MPOTO YUKO SAHIHI ILA KWA TAHADHARI



KWA MFANO
IKITOKEA MGONGANO WA MASLAHI KATI YA DRC NA TZ, CHRISTIAN BELA ATAKUWA TAYARI KUTUMWA NA DRC DHIDI YA TZ ILA HAWEZ KUTUMWA NA TZ DHDI YA DRC.

NADHANI NIMEELEWEKA
Jibu sahihi umelitoa ila hujiamini. Mpoto HAYUKO SAHIHI kuhusu uzalendo na sababu ni hiyo ambayo wewe umeieleza vyema. Mpoto aweke akilini kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya UZALENDO na USHIRIKIANO.
 
Ni aibu kujivunia mipaka iliyowekwa na wazungu , Mpoto kamaliza kila kitu
 
Nyimbo ya uzalendo inahusu nchi yangu bado niimbiwe na wasanii wa nchi jirani shubaaaamiti ubata uo
 
saaaafiiii
 
Sipendi ili neno Wanyonge
 
Kama kweli mpoto kawatoa wabongo wenzake na kumuweka huyo mzaire amekosea sn,la sivyo asingewatoa watz na huyo mcongo angemwacha aimbe,Messi ni mchezaji mzuri sn na ameisaidia sana barcelona kutwaa mataji lkn kamwe hawez kuitwa timu ya taifa ya Hispania
 
Huyo jamaa nisiyemkubali aitwaye Mrisho Mpoto ana hoja za nguvu.
Mia sana, upo sahihi wanasema humbleness is to obey and follow what is right no matter nani kasema, jamaa kajibu kistaarabu na kwa point nzito sana, hii mipaka yenyewe imewekwa juzi juzi tu ma wazungu walipokuwa "wanagawana" Afrika
 
Nenda Kaishi hapo Kenya wewe Mtanzania uone utakavyobaguliwa ndio utajua Afande Sele yuko sahihi.....Mrisho Mpoto ni mjinga kumuingiza huyo mcongo
 
Afande Sele yupo sahihi kwasababu hoja kubwa hapo ni kuwatoa baadhi ya wasanii wa Tanzania na kumuweka msanii wa Congo Bella, unawatoaje wasanii wenzio kwasababu ya msanii mwingine ambaye hata si raia na kuita ni uzalendo hii si sawa.
 
Kwanza kumsirikisha mtu ambaye si Mtanzania kisa tu ana sauti nzuri ni kukosa uzalendo, maana yake umejikataa jinsi ulivyo sasa utaipenda nchi yako kweli wakati watu wake huwapendi
 
Afande Sele yupo sahihi kwasababu hoja kubwa hapo ni kuwatoa baadhi ya wasanii wa Tanzania na kumuweka msanii wa Congo Bella, unawatoaje wasanii wenzio kwasababu ya msanii mwingine ambaye hata si raia na kuita ni uzalendo hii si sawa.
Wasaniii gani wametolewa? hakuna msanii aliyetolewa .....wasanii fulani kutoimba sio kwamba walitolewa..... hapo kuna nyimbo zaidi ya mbele....Afande ameokoteza maneno ya mitaani na vijiweni... Hapo kinacho muuma Afande ni Bela kuimba na si hivyo tuuu Afande ana wivu kweli muziki umemshinda kabaki kuwapiga madongo walio fanikiwa na wanaopiga hela kwa sasa.

Majuzi alikuwa anaongelea maswala ya maadili akawa anaponda nyimbo za kina Msaga sumu,GIgy na Zaidi kisa watanzania wana zisikiliza sana...
Lakini najiuliza wakati yeye ana vua nguo kule club na kubaki na chupi alikuwa ana hubiri maadili gani?
Afande maneno yake ya mejaa chuki na wivu dhidi ya walio fanikiwa...
Mpoto anapiga hela kweli kweli kwa hiyo Lazima Afande kwa hali aliyo nayo atafute njia ya kumfanya mpoto aonekane mtu mbaya.........
 
Sawa alikosea kuvua nguo stejini,je hilo linahalalisha wasanii wengine kuimba matusi?huoni kuwa Afande Sele amekuwa balozi mzuri wa kukemea vitu visivyofaa pengine baada ya kuhisi kuwa aliteleza huko nyuma?Tukubali tukatae,Afande Sele anabaki kuwa mmoja wa watunzi bora wa muziki tanzania.Hoja kuwa muziki umemshinda sitaki kusadiki kwasababu ni sisi wenyewe wanajamii ndio tuliokataa nyimbo zenye ujumbe ili tuimbiwe matusi na akina giggy na msaga sumu.Hivi tungo za nyimbo kama
1.Mayowe
2.Mkuki moyoni
3.Darubini kali
4.Usinichukie
5.Malaria
6.Mbele yako nyuma yangu
7.pesa
8.Nitarudi na roho yangu?
Unaanzaje kuziweka nyimbo tajwa hapo juu katika kapu moja na mwanaume mashine au nampa papa?Ifikie mahali tuwe wakweli,inawezekana ni kweli kuwa humpendi Afande Sele kwa kadiri moyo wako unavyokuagiza ila kusema kuwa muziki umemshinda hapo sio kweli.Kama "mwanaume mashine" unakuwa namba moja katika chati za muziki wetu,huo unaoshika namba 10 utakuwaje sasa?UPENDO KWA WOTE CHUKI SI KWA YEYOTE
 
Apa najaribu kuwaza ila nakumbuka kitu alafu muniambie huu ulikuwa uzalendo au kitu gani?,kombe la dunia 2002 wachezaji wengi wa Senegal kila walipokuwa wanaimba wimbo wao wa taifa walikuwa na hisia sana na wengine walikuwa wanaimba uku machozi yanawatoka alafu wakiwa uwanjan iyo shughuli yake wafaransa walipata shida hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…