Mpoyoyo naye sio mbongo huoni kichwa chake hakina ubuyu. Anajinafikisha kwa ssm utafikiri mdada. Afande piga kazi babaMpoto kichwa chake Siku hizi hakina akili tumbo limejaa fikra za ccm
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpoyoyo naye sio mbongo huoni kichwa chake hakina ubuyu. Anajinafikisha kwa ssm utafikiri mdada. Afande piga kazi babaMpoto kichwa chake Siku hizi hakina akili tumbo limejaa fikra za ccm
Mifano hai justify uzalendo wa Bella, angesema Bela amefanya nini zaidi ya wengine. Mrisho Mpoto anachangany kati ya UZALENDO na UMOJA. Ingekuwa ni kampeni ya UMOJA (UNITY) tungewashirikisha watu wa pande zote meaning mataifa mbalimbali......uzalendo una uhusiano wa moja kwa moja na homeland.......Atuambie basi kwanini anathani Bela ni mzalendo kuliko wazawa....Ila hapa mrisho mpoto kajibu kwa akili sana!!!
Maneno Makali ya AFANDE SELE kutoka Instagram Kwa MRISHO MPOTO na Majibu ya MPOTO kwa AFANDE SELE...
Afande Sele King - Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara ktk kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu christian bella kushiriki ktk wimbo huo unaowahusu watanzania wkt ukijua wazi kuwa bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lkn bado yeye sio mtz bali ni mcongoman....ktk hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini...
Majibu
Mrisho Mpoto Akijibu - Kaka yangu @afandeseleking Bado narudia kusema kwamba heshima nnayokupa inatoka Mbali sana kwenye chumba cha nne cha moyo Wangu... Sihitaji kupoteza wino Mwingi kukukumbusha tofauti iliyopo kati ya UZALENDO, UZAWA na URAIA kwasababu nina uhakika unazifahamu vyema isipokuwa huenda leo haujaamkia ule ubavu sahihi na ule wa ukarimu wako ulionao siku zote, mpaka ukakataa uwepo wangu hapa Duniani Kwa kunichagulia adhabu ya kupigwa risasi tano tena za kichwa... kwakua hukuniuliza hili jambo kabla Itoshe kusema hunitaki tena...hivyo basi kabla sijapigwa hizo risasi tano nitakachofanya ni kukupa maelezo machache yatakayokufanya uipate picha ya UZALENDO.. Hivi unajua kama John Okello alipigania uhuru wa Zanzibar!? Majeshi yetu yamepigania uhuru wa msumbiji na hata Chegu sio mcuba na alipigania uhuru wa Cuba na Congo pia.. Na je unajua kama kuna wazawa wanaoangamiza maslahi ya nchi na kuna wazalendo wasiobagua!? Kaka, Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zetu ( umajumui Afrika, tena ukichimba huko sana kwa hapa nchini utakuna na Prof Shivji) .. na ndio maana hata mwenge wa uhuru uliwekwa juu ya mlima kilimanjaro ili kumulikia nchi nyingine.. Kumbuka hiyo mitizamo ya KIUZAWA Mwalimu aliita mitizamo membamba.. kwa maana ya kwamba ipo kwa ajili ya Kuiangamiza afrika
Na mwisho ningependa kukuuliza--->Je umezisikia shangwe za wazalendo na wazawa leo hapa dodoma baada ya kusikia Babu Seya na familia yake wamepewa msamaha wa rais!!? Wewe ni RASTA kaka.. kumbuka siku zote CHUKI HUMUUMIZA ANAYEIHIFADHI.. [HASHTAG]#AfrikaUnite[/HASHTAG] ✊
Nani yupo sahihi kati ya hawa mafahari wawili?
Je kuwa Mzalendo ni lazima uwe mzawa wa nchi husika?[/Q
afande yupo sahihi vp mwanamuziki wa bongoHii imenikumbusha alivowakilisha kenya uko nchi za watu kwenye tamasha la kiswahili japo alijitetea sana
Jibu sahihi umelitoa ila hujiamini. Mpoto HAYUKO SAHIHI kuhusu uzalendo na sababu ni hiyo ambayo wewe umeieleza vyema. Mpoto aweke akilini kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya UZALENDO na USHIRIKIANO.MPOTO YUKO SAHIHI ILA KWA TAHADHARI
KWA MFANO
IKITOKEA MGONGANO WA MASLAHI KATI YA DRC NA TZ, CHRISTIAN BELA ATAKUWA TAYARI KUTUMWA NA DRC DHIDI YA TZ ILA HAWEZ KUTUMWA NA TZ DHDI YA DRC.
NADHANI NIMEELEWEKA
saaaafiiiiManeno meeeeengi na ngonjera hakuondoi definition ya Uzalendo.
patriotism
ˈpeɪtrɪətɪz(ə)m/
noun
noun: patriotism
the quality of being patriotic; vigorous support for one's country
Huwezi kuwa mzalendo kwa nchi isiyo yako. Askari wetu kwepo Congo, hakumaanishi wao ni Wazalendo wa DRC, NO. Christian Bella anaweza kuipenda Tanzania, lakini hawezi kuwa mzalendo kwa nchi yetu. Hawezi kuipigania Tanzania dhidi ya nchi yake, na hapo ndio maana ya uzalendo inapatikana.
Sipendi ili neno WanyongeUzalendo sio rangi au asili ya nchi unakotoka!Bali ni fikra na utayari kuipigania nchi kwa ajili ya maendeleo na ukombozi wa wanyonge!Alichoeleza mpoto kina maana na ndio fikra hasa za uzalendo!Kuna mijitu imezaliwa hapa na mijizi haina huruma na wanyonge,kisa mweusi utamwita mzalendo?lakini kuna mtu mfano prof shivji ni muasia kwa asilia lakini ana imani na yuko tayari kuipigania TZ mpaka kifo tutamwitaje??
Afande sele akue....
Mia sana, upo sahihi wanasema humbleness is to obey and follow what is right no matter nani kasema, jamaa kajibu kistaarabu na kwa point nzito sana, hii mipaka yenyewe imewekwa juzi juzi tu ma wazungu walipokuwa "wanagawana" AfrikaHuyo jamaa nisiyemkubali aitwaye Mrisho Mpoto ana hoja za nguvu.
Nitarudi na roho yangu?Mkuu hujanijibu bado .nitajie wimbo wa afande sele wa peke yake mkali/uliohit ambao hata leo unaweza ukausikiliza na ukakukonga moyo.
Wasaniii gani wametolewa? hakuna msanii aliyetolewa .....wasanii fulani kutoimba sio kwamba walitolewa..... hapo kuna nyimbo zaidi ya mbele....Afande ameokoteza maneno ya mitaani na vijiweni... Hapo kinacho muuma Afande ni Bela kuimba na si hivyo tuuu Afande ana wivu kweli muziki umemshinda kabaki kuwapiga madongo walio fanikiwa na wanaopiga hela kwa sasa.Afande Sele yupo sahihi kwasababu hoja kubwa hapo ni kuwatoa baadhi ya wasanii wa Tanzania na kumuweka msanii wa Congo Bella, unawatoaje wasanii wenzio kwasababu ya msanii mwingine ambaye hata si raia na kuita ni uzalendo hii si sawa.
Sawa alikosea kuvua nguo stejini,je hilo linahalalisha wasanii wengine kuimba matusi?huoni kuwa Afande Sele amekuwa balozi mzuri wa kukemea vitu visivyofaa pengine baada ya kuhisi kuwa aliteleza huko nyuma?Tukubali tukatae,Afande Sele anabaki kuwa mmoja wa watunzi bora wa muziki tanzania.Hoja kuwa muziki umemshinda sitaki kusadiki kwasababu ni sisi wenyewe wanajamii ndio tuliokataa nyimbo zenye ujumbe ili tuimbiwe matusi na akina giggy na msaga sumu.Hivi tungo za nyimbo kamaWasaniii gani wametolewa? hakuna msanii aliyetolewa .....wasanii fulani kutoimba sio kwamba walitolewa..... hapo kuna nyimbo zaidi ya mbele....Afande ameokoteza maneno ya mitaani na vijiweni... Hapo kinacho muuma Afande ni Bela kuimba na si hivyo tuuu Afande ana wivu kweli muziki umemshinda kabaki kuwapiga madongo walio fanikiwa na wanaopiga hela kwa sasa.
Majuzi alikuwa anaongelea maswala ya maadili akawa anaponda nyimbo za kina Msaga sumu,GIgy na Zaidi kisa watanzania wana zisikiliza sana...
Lakini najiuliza wakati yeye ana vua nguo kule club na kubaki na chupi alikuwa ana hubiri maadili gani?
Afande maneno yake ya mejaa chuki na wivu dhidi ya walio fanikiwa...
Mpoto anapiga hela kweli kweli kwa hiyo Lazima Afande kwa hali aliyo nayo atafute njia ya kumfanya mpoto aonekane mtu mbaya.........