Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Mpoto katumia tafsir sisi katoa mfano che guavara ajui kuwa ulikuja kwa order maalum kuanzia Cuba mpk Congo mbn alikubali kugawana keki ya taifa km pongez alicho kifanya Mpoto automatically kakosea Bella hakustaili huu ni usalit
Alafu nimsaidie mpoto che Guevara alokuwa kama mwanajeshi wa kukodiwa tu anakusaidia kufanya mapinduz baada ya apo unampa keki yake anarud zake mexico.
 
Nyie wasanii ndo kioo kama nyie mkishindwa ku maintain carrier yenu hakuna maana ya kufanya mziki mnaoufanya
 
Siku hizi kila kitu siasa vijana amkeni mlisho yupo chama gani? Na afande chama gani? Mkijibu ndio litakua jibu akili ni nywele kila mtu.......
 
Wasaniii gani wametolewa? hakuna msanii aliyetolewa .....wasanii fulani kutoimba sio kwamba walitolewa..... hapo kuna nyimbo zaidi ya mbele....Afande ameokoteza maneno ya mitaani na vijiweni... Hapo kinacho muuma Afande ni Bela kuimba na si hivyo tuuu Afande ana wivu kweli muziki umemshinda kabaki kuwapiga madongo walio fanikiwa na wanaopiga hela kwa sasa.

Majuzi alikuwa anaongelea maswala ya maadili akawa anaponda nyimbo za kina Msaga sumu,GIgy na Zaidi kisa watanzania wana zisikiliza sana...
Lakini najiuliza wakati yeye ana vua nguo kule club na kubaki na chupi alikuwa ana hubiri maadili gani?
Afande maneno yake ya mejaa chuki na wivu dhidi ya walio fanikiwa...
Mpoto anapiga hela kweli kweli kwa hiyo Lazima Afande kwa hali aliyo nayo atafute njia ya kumfanya mpoto aonekane mtu mbaya.........
Mleta mada ameuliza nani yupo sahihi kutokana na maelezo yaliyotolewa na hawa wasanii wawili na mimi nimejibu baada ya kusoma maelezo yao, labda jibu langu lingekuwa tofauti kama Mrisho Mpoto angesema mwenyewe kuwa hakutoa wasanii, badala yake amemjibu kwakutolea mifano ya baadhi ya wanaharakati bila ya kujua ya kuwa hao wanaharakati walikuwa wanafanya hivyo huku kukiwa na malipo yao so huo pia si uzalendo.
Sasa kama wewe unasema hamna wasanii waliotolewa then mada iwe nani yuko sahihi kati yako na Afande Sele
 
Mzalendo ni mtu anayeipenda NCHI YAKE na yupo tayari kuifia. Sasa mtu kama siyo RAIA maana yake nchi siyo yako utaipendaje?
 
Tujiulize kwanza kama ikitokea vita kati ya Tanzania na Kongo je Christian Bella ataisapoti Tanzania kutoka moyoni na kutaka tuishinde Congo? Kama jibu ni ndiyo kidogo atakuwa mzalendo
 
Mpoto yuko sawa sana hii dhana ya uzawa iko kwa nchi maskini sana pia inachangiwa sana na ubinafsi uliokubuhu kama jambo linafanyika kwa maslah mapana ya nchi hakuna haja yakuangalia ni nan anayelifanya ndio maana kwenye jesh la marekan kunawapare kibao mpaka wamatengo tukija kwenye soka ufaransa ni mfano tosha na balaa lake wote tunalijua namaliza kwakusema afande mbinafsi kwa kiwango cha kawaida kabisa
Unajua hoja hapa, ni kwamba, kukatwa wasanii wengine wa kitanzania ili tu kuingizwa mkongomani, hapo ndo penye shida.uzalendo upo wapi hapo? Laiti kungekua na nafasi ya kutosha kusingekua na shida.
 
Huyu anajiita afande wakati hata depo haijui nadhani bangi zinamuendesha vibaya sana
 
Mrisho Mpoto anachanganya uzalendo na uana mapinduzi!!

Mifano aliyoitoa haihusiani na uzalendo bali uanamapinduzi! Uzalendo ni utiifu na kuwa tayari kufia TAIFA lako! Uzalendo una uhusiano wa moja kwa moja na utaifa! Uzalendo hauna itikadi lakini uzalendo una mipaka. Haiwezekani, narudia, HAIWEZEKANI Mtanzania akawa Mzalendo kwa niaba ya Kenya... haiwezekani!

Kinyume chake, Uanamapinduzi unasukumwa na itikadi na wala hauna mipaka!! Mtu anaweza kuwa Mwanamapinduzi lakini asiwe mzalendo! Na mtu ambae ni Mwanamapinduzi lakini sio Mzalendo anaweza kupigana bega kwa bega na wageni dhidi ya taifa lake provided ana itikadi moja na hao wageni; itikadi ambayo haipo kwenye nchi yake!!

Kwa mfano, mimi naweza kuamini Ubebari ni mfumo wa kidhalimu, kinyonyaji, uonevu na ni mfumo unaopaswa kutokomezwa duniani! Sehemu mbalimbali duniani kunaweza kuwa na watu wenye itikadi kama yangu!!! Sasa wanaweza kutokea wanamapinduzi sehemu nyingine duniani wanaolenga kutokomeza ubepari duniani kwa gharama yoyote!

Wanamapinduzi hawa wanaweza kuona ubepari uliopo Tanzania ndio ubepari mbaya kabisa duniani na haupaswi kudumu japo kwa dakika moja nyingine na hivyo wakaamua kushika silaha na kuingia Tanzania ili kupambana na mfumo unaodumisha huo udhalimu!!

Mimi ingawaje ni Mtanzania, lakini kwavile naamini ubepari ni udhalimu kama wanavyoamini hao wageni; basi naweza kuungana nao dhidi ya nchi yangu kwa sababu tu nataka kuondoa mfumo ambao siuamini!!! Kesho na kesho kutwa naweza kusafiri maili elfu kadhaa kwenda nchi nyingine ili kupambana dhidi ya huo mfumo nisiouamini!

Kinyume chake, Mzalendo siku zote atapambana kuipigania nchi yake; PERIOD!!!!

Leo hii Mungu akitokea na kuniambia nichague ama aingamize DRC au Tanzania vinginevyo achague mwenyewe basi bila kusita nitamwambia angamiza DRC!!

Sasa Je, leo hii Christian Bella akipewa mtihani kama huo nae anaweza kufanya maamuzi bila kusita sita au atakuwa anajing'atang'ata upande mmoja akifikiria ndugu zake waliopo DRC na upande mwingine akifikiria washikaji zake waliopo TZ?!

Leo hii pakitokea vita kati ya Tanzania na DRC kisha nikaambiwa nibebe silaha kisha nichague upande wa kupigana; kwanza nitamtukana kuniambia nichague upande wa kupigana kwa sababu pasi na shaka yoyote nitapigana kwa niaba ya Tanzania!

Je, Christian Bella akikumbwa na mtihani wa namna hiyo; nae atabeba silaha na bila kusita atapigana kwa niaba ya Tanzania?!

Itoshe tu kusema kwamba Mtanzania HAWEZI kuwa mzalendo kwa niaba ya Kenya, Burundi, DRC n.k! Hao akina Okello walikuwa ni wanamapinduzi ambao kimsingi hawana mipaka lakini si kwamba walikuwa Wazalendo!!!

Watu kama akina Nyerere walikuwa ni Wazalendo na wakati huo huo ni wanamapinduzi! Na kwavile wanamapinduzi hawana mipaka, ndio maana hawakuishia kuipigania Tanzania peke yake bali Afrika mzima!!! Lakini hata wapigane mbali namna gani, kwa Mzalendo, NYUMBANI KWANZA!!
 
Back
Top Bottom