Mrisho Mpoto anachanganya uzalendo na uana mapinduzi!!
Mifano aliyoitoa haihusiani na uzalendo bali uanamapinduzi! Uzalendo ni utiifu na kuwa tayari kufia TAIFA lako! Uzalendo una uhusiano wa moja kwa moja na utaifa! Uzalendo hauna itikadi lakini uzalendo una mipaka. Haiwezekani, narudia, HAIWEZEKANI Mtanzania akawa Mzalendo kwa niaba ya Kenya... haiwezekani!
Kinyume chake, Uanamapinduzi unasukumwa na itikadi na wala hauna mipaka!! Mtu anaweza kuwa Mwanamapinduzi lakini asiwe mzalendo! Na mtu ambae ni Mwanamapinduzi lakini sio Mzalendo anaweza kupigana bega kwa bega na wageni dhidi ya taifa lake provided ana itikadi moja na hao wageni; itikadi ambayo haipo kwenye nchi yake!!
Kwa mfano, mimi naweza kuamini Ubebari ni mfumo wa kidhalimu, kinyonyaji, uonevu na ni mfumo unaopaswa kutokomezwa duniani! Sehemu mbalimbali duniani kunaweza kuwa na watu wenye itikadi kama yangu!!! Sasa wanaweza kutokea wanamapinduzi sehemu nyingine duniani wanaolenga kutokomeza ubepari duniani kwa gharama yoyote!
Wanamapinduzi hawa wanaweza kuona ubepari uliopo Tanzania ndio ubepari mbaya kabisa duniani na haupaswi kudumu japo kwa dakika moja nyingine na hivyo wakaamua kushika silaha na kuingia Tanzania ili kupambana na mfumo unaodumisha huo udhalimu!!
Mimi ingawaje ni Mtanzania, lakini kwavile naamini ubepari ni udhalimu kama wanavyoamini hao wageni; basi naweza kuungana nao dhidi ya nchi yangu kwa sababu tu nataka kuondoa mfumo ambao siuamini!!! Kesho na kesho kutwa naweza kusafiri maili elfu kadhaa kwenda nchi nyingine ili kupambana dhidi ya huo mfumo nisiouamini!
Kinyume chake, Mzalendo siku zote atapambana kuipigania nchi yake; PERIOD!!!!
Leo hii Mungu akitokea na kuniambia nichague ama aingamize DRC au Tanzania vinginevyo achague mwenyewe basi bila kusita nitamwambia angamiza DRC!!
Sasa Je, leo hii Christian Bella akipewa mtihani kama huo nae anaweza kufanya maamuzi bila kusita sita au atakuwa anajing'atang'ata upande mmoja akifikiria ndugu zake waliopo DRC na upande mwingine akifikiria washikaji zake waliopo TZ?!
Leo hii pakitokea vita kati ya Tanzania na DRC kisha nikaambiwa nibebe silaha kisha nichague upande wa kupigana; kwanza nitamtukana kuniambia nichague upande wa kupigana kwa sababu pasi na shaka yoyote nitapigana kwa niaba ya Tanzania!
Je, Christian Bella akikumbwa na mtihani wa namna hiyo; nae atabeba silaha na bila kusita atapigana kwa niaba ya Tanzania?!
Itoshe tu kusema kwamba Mtanzania HAWEZI kuwa mzalendo kwa niaba ya Kenya, Burundi, DRC n.k! Hao akina Okello walikuwa ni wanamapinduzi ambao kimsingi hawana mipaka lakini si kwamba walikuwa Wazalendo!!!
Watu kama akina Nyerere walikuwa ni Wazalendo na wakati huo huo ni wanamapinduzi! Na kwavile wanamapinduzi hawana mipaka, ndio maana hawakuishia kuipigania Tanzania peke yake bali Afrika mzima!!! Lakini hata wapigane mbali namna gani, kwa Mzalendo, NYUMBANI KWANZA!!