LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 252
Shemeji mwazima taa ilikuwa ya Salum AbdalahMarijani tungo kali na sauti nzuri vinamfanya awe na ladha ya kipekee. Mbaraka alikuwa ni muhuni, nyimbo zake za shemeji shemeji huku mwazima taa na mtaa wa saba zimedhihirisha
mambo ya kuzima taa ni soo, unaweza ikakuta njemba imeingia na dildo uwanjani ili kumshughulikia shemeji.Back to the topicShemeji mwazima taa ilikuwa ya Salum Abdalah
kwanini?
Mpaka mtu upewe jina la JABALI mana watu wamekubali mchango wako..Tungo za marijani zilikuwa nzuri na zenye maudhUi..ndo mana baadhi ya nyimbo zilitumika kufundishia mashuleni.
Hapo kwenye pombe si chai katoa elimu kwa wanaoanza pombe, wasije kuishia pabaya.Kwangu MARIJANI ni zaidi! Napenda kusikiliza mara kwa mara nyimbo Bwana Mashaka Tamaa Mbele, Dunia Uwanja Wa Fujo, Masudi, Namsaka Mbaya Wangu, Ndoa Ya Mateso, Pombe Si Chai, Rufaa Ya Kifo, Sikitiko, Talaka Kampa Nani, Tuishi Kwa Furaha, Ukatili Ni Unyama, Uke Wenza, Usia Wa Baba na Walimwengu
Kati ya hawa miamba wawili, ni yupi alikuwa na tungo nzuri zaidi ya mwenzie? Pia sauti ya nani ilikuwa na mvuto zaidi?
yani umenisoma % 100. Tatizo hata picha zao hatuzijui achilia mbali nyimbo zao. Niliwahi kuona picha ya marijani akiwa junk. Presley na marijani ni droo ila watz walishindwa kumtangaza
Ingawa sikuwepo lakini namsikiliza sana Marijani.
Jamaa alikua jembe sana,pia na Ndala Kasheba-Marashi ya pemba bado inakimbiza.
Mkuu Marijani amefariki mwaka 1995 bado tu ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa hujajitambua bado?
kinachomfanya marijani kuwa juu ya Mbaraka Mwinshehe ni aina ya tungo zake.. Tungo za marijani ni sawa na hadithi.. Mara nyingi tungo zake zilianza na A na kwisha na Z.. Kama mnaufahamu wimbo wake wa ndoa ya mateso ndo mtaelewa ninamaanisha nini.. Pia alikuwa anaingiza sana nahau na methali kwenye nyimbo zake.. Kitendo cha mashairi ya wimbo wake wa mwanameka kutumiwa kwenye mtihani wa kitaifa wa form 4 mwishoni mwa miaka ya 80 (au mwanzoni mwa 90) ni kielelezo tosha kwamba Marijani ni nguli aliesimama pekee juu..
Maneti hakustahili kuwepo kwenye hili kundi..