Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Mkuu wakati anakumbana na umauti Marijani alikuwa ameacha kupiga dansi.. Alikuwa na duka lake ambalo alikuwa anauza nyimbo zake pamoja na nyimbo toka kwa wasanii wengine tofauti.. Kama ninakumbuka sawasawa competitive musik aliachana nao kwenye mwaka 1987 hivi (I stand to corrected)..

Hapa hata mimi sina uhakika sana aliacha kuimba lini, ngoja tumuite Balantanda afafanue maana yeye ndo ana kumbu kumbu nzuri na hawa wanamziki wetu wa zamani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nadhani hii line inaimbika hivi
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mchezo wa mapenzi..."

Enyi vijana sikilizeni
Mnapokuwa masomoni
Acheni mchezo na Mapenzi
Mnawapa uchungu ooh wazazi wenuu...

Wazazi wanakusomesheni
Kwa gharama nyingi sana
Matokeo ni kufukuzwa shule
Mapenzi na masomo vyote vyapoteaa
 
Konaball nawakubali hao wawili wa mwanzo ila Maneti mmh sijui, Marijani alikuwa ana powerful voice sikiliza ukewenza, DAH ZUWENA miaka hiyo ya 79-84 nilikuwa Sumbawanga kuna Mwanameka. ila wadau mimi hawa wana SIKINDE NGOMA YA UKAE ya wakati ule ilikuwa inatisha si mchezo, Kuna Huyu jamaa anaitwa Hassan Rehani Bitchuka(wakati ule) sauti yake kwa kweli haikuwa na mpinzani ilikuwa inapanda mpaka mwisho(Highet pitch) sasa hivi kwishnei, nna kanda yao yaani kila ikifika ijumaa naiweka kusikiliza ule wa wimbo wa wikiendi, tufurahi na wana sikinde tucheze leo ngoma ya ukae, ukitaka kufurahi, kila jumamosi njoo uburudike na wana sikinde oyee halafu wanataja majina ya kundi zima enzi hizo akina KING ENOCK, Mwanyiro, Gama, dah mpaka mwili unasisimka. Hapo msondo enzi hizo ilikuwa haioni ndani kwa sikinde, kuna vibao kama Duniani kuna mambo, Selina-WADAU kweli vipaji vilikwepo sasa hivi eti wanamziki wa Ubongo wa Fleva akauambia nilipata idea hiyo hapo hapo nikaanza kuandika verse nikaenda studio nikamkuta DUNGA tukapanga vyombo baada ya nusu saa track imekamilika kweli JAMANI? NDO MAANA INAITWA Bongo Flavour sababu ni ka fleva fulani hivi ka muda wa wiki kadhaa baada ya hapo kwishnei

nausikiliza Ubaya toka kwa Sikinde...
Solo Batholomayo Mulenga, Rythim Abdalah Gama na Bass kapiga Suleiman Mwanyilo, tumba kapiga Ally Jamwaka, saxa zimepigwa na King Enock Teacher, kwenye safu ya uimbaji imeongozwa na Maalim Mjomba, Maalim Hamis Juma, yupo Cosmas, na Rehani.
Kikosi kilikuwa kimekamilika kama cha AC Milan ya mwaka 1989
 
Kwanza Kabisa ningemtoa Hemedi Maneti, Kisha ningekuambia kua Marijani Rajabu alikua na kipaji cha pekee sana haswa ktk kuandika mashairi yanayogusa watu. Pia ningemtaja Mbaraka Mwishehe kuwa ni Mwanamuziki ambaye aliwafungua macho zaidi wanamuziki kuwa tunaweza bila kuiga watu wa nje.
 
Hapa hata mimi sina uhakika sana aliacha kuimba lini, ngoja tumuite Balantanda afafanue maana yeye ndo ana kumbu kumbu nzuri na hawa wanamziki wetu wa zamani.
Kiukweli waliompa Marijani jina la Jabali la Muziki hawakukosea......Huyu bwana alikuwa na kipaji hasa cha kutunga mashairi na ndio maana nyimbo zake mpaka le zinatamba....

Kwa kifupi Marijani Rajabu alikuwa mkali zaidi ya wote hao.....

Kihistoria kwa kifupi sana Marijani alizaliwa Kariakoo mwaka 1954 na alianza muziki mwaka 1972 akiwa na bendi ya STC Jazz ambayo hakukaa nayo sana kwani mwaka huohuo alihamia bendi ya Safari Trippers na baadae mwaka 1977 alijiunga na Dar International ( wana Super Bomboka) ambako alikutana na akina Abel Balthazar, Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......

Marijani alikaa na Dar International hadi mwaka 1986 bendi ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo....Naada ya Dar International kuvunjika Marijani alikosa bendi lakini baadae aliungana na wanamuzaiki wenzake zaidi ya 50 waliotamba miaka hiyo ya katikati na mwishoni mwa 80 na kuunda kundi(Zing zong) la Tanzania Stars .....Baadae katika kutafuta mkate wa kila siku Marijani alipiga Deiwaka Mwenge Jazz na baadae akajiunga na Kurugenzi Jazz ya Arusha na mwanzoni mwa miaka ya 90 akaanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Kundi hili lilikuwa likitumia vyombo vya kukodi/kuazima na halikudumu sana hali iliyopelekea kuvunjika mwanzoni mwa mwaka 1992....

Baada ya Afri Culture kufa hali ya Marijani kiuchumi ilikuwa mbaya sana hali iliyomlazimu afungue kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo mpaka mauti yalipomfika tarehe tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo ya moyo kuwa mkubwa.....Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nnne miaka hiyo....

Ingawa Historia yake ni ndefu sana lakini kwa kifupi sana naweza kusema hiyo ndiyo Historia fupi ya MARIJANI RAJABU a.k.a Bulldozer a.k.a Doza a.k.a JABALI LA MUZIKI
 
Hii niliiweka siku za nyuma nikimzungumzia Marijani Rajabu na Dar International....

Huyo ndio Jabali la muziki Marijan Rajab na Dar International mkuu...

Marijan Rajab kabla hajahamia Dar International alikuwa katika bendi ya Safari Trippers ambayo ilisambaratika mwaka 1977......Baada ya Safari Trippers kufa nini kilifuata?.....Mwaka huohuo 1977 mwanamuziki mwingine Nguli chini Abel Barthazar alianzisha bendi ya Dar Internatinal ambayo pamoja naye(Balthazar) pia walikuwepo Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,ALi Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......

Bendi hii ilianza kwa kutoka na vibao kama Nyerere mwanamapinduzi,Rufaa ya kifo,Mwana uoe,Betty,Margreth na Sikitiko,....Vibao hiivi vilitamba hasa na bendi ilianza kushika chati ya juu katika medani za muziki wa Dansi Tanzania.....Bendi hii ilikuwa maarufu ghafla na kwa kupitia Marijan Rajab ilipiga muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo(miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).....Mwaka 1978 baada ya Marijan Rajab kujiondoa bendi haikudumu sana kwani ilisambaratika baada ya wanamuziki nane(08) tegemeo wa bendi hiyo Abel Barthzar(aliondoka kabla ya wenzie),King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jef waliondoka na kwenda kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra(baadae DDC Mlimani Park Orchestra).....

Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....

Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........

Hao ndio Dar International Orchestra wana Super bomboka chini yake Jabali la muziki Hayati Marijan Rajab(R.I.P)......

https://www.jamiiforums.com/enterta...0-na-90-mitindo-yao-na-wanamuziki-wake-3.html
 
Kiukweli waliompa Marijani jina la Jabali la Muziki hawakukosea......Huyu bwana alikuwa na kipaji hasa cha kutunga mashairi na ndio maana nyimbo zake mpaka le zinatamba....

Kwa kifupi Marijani Rajabu alikuwa mkali zaidi ya wote hao.....

Kihistoria kwa kifupi sana Marijani alizaliwa Kariakoo mwaka 1954 na alianza muziki mwaka 1972 akiwa na bendi ya STC Jazz ambayo hakukaa nayo sana kwani mwaka huohuo alihamia bendi ya Safari Trippers na baadae mwaka 1977 alijiunga na Dar International ( wana Super Bomboka) ambako alikutana na akina Abel Balthazar, Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......

Marijani alikaa na Dar International hadi mwaka 1986 bendi ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo....Naada ya Dar International kuvunjika Marijani alikosa bendi lakini baadae aliungana na wanamuzaiki wenzake zaidi ya 50 waliotamba miaka hiyo ya katikati na mwishoni mwa 80 na kuunda kundi(Zing zong) la Tanzania Stars .....Baadae katika kutafuta mkate wa kila siku Marijani alipiga Deiwaka Mwenge Jazz na baadae akajiunga na Kurugenzi Jazz ya Arusha na mwanzoni mwa miaka ya 90 akaanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Kundi hili lilikuwa likitumia vyombo vya kukodi/kuazima na halikudumu sana hali iliyopelekea kuvunjika mwanzoni mwa mwaka 1992....

Baada ya Afri Culture kufa hali ya Marijani kiuchumi ilikuwa mbaya sana hali iliyomlazimu afungue kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo mpaka mauti yalipomfika tarehe tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo ya moyo kuwa mkubwa.....Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nnne miaka hiyo....

Ingawa Historia yake ni ndefu sana lakini kwa kifupi sana naweza kusema hiyo ndiyo Historia fupi ya MARIJANI RAJABU a.k.a Bulldozer a.k.a Doza a.k.a JABALI LA MUZIKI
Mkuu wewe mkali unatisha nashukuru kwa kumfahamu MARIJANI
 
Ndo maana nikapendekeza uje hapa utoe ufafanuzi, asante sana kwa ufafanuzi, na ni kweli pia alitaka kujiunga na Club ya Simba maana inasemekena pia alikuwa na kipaji cha mpira hasa nafasi ya Kaseja?
 
Hii niliiweka siku za nyuma nikimzungumzia Marijani Rajabu na Dar International....

Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........

Ha ha ha ha Mkuu Balantanda umenikumbusha hizo nyimbo.. Ila sijui kama unakumbuka nini kilichopelekea Marijani kutunga kibao hicho cha mpenzi Aisha.. Hiyo ni historia ya kweli kwamba Marijani alikutana na huyu bi Aisha Mwanza.. Na walikubaliana bibie aje Dar waje kukutana na Marijani pale.. Inasemekana Marijani aligandishwa pale Keys Hotel na bi Aisha ambae hakutokea tena.. Mara ya mwisho kama miaka miwili mitatu iliopita nilisikikia wanasema huyu bi Aisha yuko Marekani.. Ulishaisikia hii..?
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa wakuu! Lakini kwa Solo nafikiri Marijani hamfikii Mbaraka.
Ila kwa kuimba na kuongoza nyimbo...hapo ndipo Marijani "Jabali" anamzidi Mbaraka.

Hata hivyo hawapishani sana, kwangu mie nikigawa 100%, huenda ikawa 51% = Mariijani. na 49% = Mbaraka.

Hata hivyo mie namkubali Mbaraka kwa sababu ya nyimbo kama vile 'Shida', ambapo uwezo wake wa kupiga gitaa la solo ulikuwa wa pekee sana.

Kumshindanisha Marijani na Mbaraka ni sawa na kushindanisha; Franco na Tabu Ley..mmoja anaimba zaidi mwingene mzuri wa kupiga 'chombo'..inategemea mtu mwenyewe anapenda nini..huo ndo uzuri wa muziki.

Unapenda kile kinachokuvutia..asanteni wakuu kwa hoja zenu!
 
Dah hao wawili marijani na mbaraka sijui hata niwatofautisheje?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwanza kumuingiza Maneti humu ni kumuonea, Mbaraka na Marijani wanasimama kivyao. Ila kwa maoni yangu....na ndivyo ilivyo kwa kweli...MARIJANI bado hajatokea nchini. na tusibishane sana wanaosema Mbaraka waorodheshe nyimbo zake zilizowagusa na wanaosema Marijani wafanye hivyo, Wa Mbaraka watakaa. Nyimbo za Marijani hazichoshi kusikiliza na zimejaa ujumbe......

Jua laniangazia
Dada acha uvivu
Salama
Viki mtoto wa mama
Pombe sio chai
Matilda mtunze mwanao
Christina mapenzi yako yanipa wazimu

JABALI LA MUZIKI hana mpinzani na kwa kumuenzi huyu bwana hizi TUZO ZA KILI zingepewa jina lake.
 
Ila mkuu kwa nyimbo zenye ujumbe Hemed Maneti Ulaya aka Chiriku naye sio wa kumbeza, hebu tafuta hizi nyimbo usikilize ujumbe uliomo: Kuruka ukuta, Aza, Stella mtoto mwenye fikara nzuri, Jiko limenuna, Madaraka kwenye bar, Mary Maria na Magdalena halafu uje umalizie na Nilitaka iwe siri pamoja na ule aliokuwa anamsifia mke wake Chiku.

Lakini pamoja na kwamba hizo nyimbo zina ujumbe lakini nimenote tatizo lake nyimbo zake nyingi zilikuwa za mapenzi ingawa yeye alikuwa anaimbia bendi inayomilikiwa na chama cha siasa, hicho ndo kinachokuja kumpa Marijani credit kwa sababu alikuwa anagusa karibia kila angle ya maisha.

Kuna ule wimbo wa ukombozi, nadhani unaitwa sikitiko, na nyingine kama dunia imekwisha, dunia uwanja wa fujo na ukitaka kujua sauti yake ilikuwa decibel ngapi sikiliza wimbo unaitwa Mpenzi Aisha. Kweli Jabali la mziki.

Mbaraka naye pamoja na kwamba nyimbo zake nyingi ni fupi fupi na anarudia rudia sana verse, lakini nazo zina meseji: nyimbo kama Shida, Baba Mdogo, Regina, Dina.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa kati ya hao kuna wa kushindana na Mbaraka Mwinshehe...sioni... wote nina nyimbo zao nyiingi tu, nawapenda na nasikiliza saana nyimbo zao. sioni hata anayemkaribia Mwinshehe....
 
Balantanda usisahau kuwaambia hao kuwa Marijani ana sifa pekee ya uchoyo.
 
Ndo maana nikapendekeza uje hapa utoe ufafanuzi, asante sana kwa ufafanuzi, na ni kweli pia alitaka kujiunga na Club ya Simba maana inasemekena pia alikuwa na kipaji cha mpira hasa nafasi ya Kaseja?

Naomba umuulize Balantanda je kwa umahiri na ujabali wa Marijani je ilikuwaje akose bendi ya kuimba na kukaa benchi takriban miaka mitatu toka 1986 mpaka 89?

Na je pamoja na ujabali wake ilikuwaje Bendi alizoanzisha hazikuwa kali kama ambazo alikuta zimeshaanzishwa na yeye akajiunga nazo?
 
Ngoja nimuite mwenyewe aje, Balantanda nkwingwa njoo huku uzidi kutoa ufafanuzi kulingana na swali la mkuu Gang Chomba.
 
Last edited by a moderator:
Balantanda usisahau kuwaambia hao kuwa Marijani ana sifa pekee ya uchoyo.
Uchoyo ni hulka ya mtu....Kila mtu ana element za uchoyo.....Hata wewe u mchoyo katika nyanja fulani....Nadhani kama ni suala la uchoyo kwenye muziki basi Marijani asingeshirikiana na mwanamuziki yoyote yule katika kuimba nyimbo na kutengeneza muziki....Kitu pekee ambacho watu walikuwa hawakijui kwa Marijani ni kwamba alikuwa hapendi kunyonywa/kukandamizwa na alikuwa ana kipaji hali iliyomfanya ajiamini kwamba anaweza na ndio maana baada ya kuona ubabaishaji mwingi na watu wengi wanatajirika kupitia mgongo wake/kwa jasho lake alion ni bora aachane na muziki na kuamua kuuza kanda za muziki wake na maisha yakawa yanasonga mbele.....Hili watu kama akina Mbaraka Mwinyishehe hawakuliona ndio maana walinyonywa sana na kwa taarifa yako ukinda kwa mke wa Mbaraka Mwinyishehe (mama Taji) atakueleza ni jinsi gani wakenya walitajirika na kipaji cha mume wake na kuiacha familia yake masikini....Kitu hicho mtoto wa Kariakoo Doza alikiona na hakutaka kitokee maishani mwake ndio maana akaachana na muziki na kufungua kijiduka cha kuuza kanda zilizotokana na kipaji chake.......
 
Naomba umuulize Balantanda je kwa umahiri na ujabali wa Marijani je ilikuwaje akose bendi ya kuimba na kukaa benchi takriban miaka mitatu toka 1986 mpaka 89?

Na je pamoja na ujabali wake ilikuwaje Bendi alizoanzisha hazikuwa kali kama ambazo alikuta zimeshaanzishwa na yeye akajiunga nazo?

Ngoja nimuite mwenyewe aje, Balantanda nkwingwa njoo huku uzidi kutoa ufafanuzi kulingana na swali la mkuu Gang Chomba.

Wakuu wangu Gang Chomba na Nkwingwa Masuke.....Nataka tu niwaambie kwamba....

Kitu pekee ambacho watu walikuwa hawakijui kwa Marijani ni kwamba alikuwa hapendi kunyonywa/kukandamizwa na alikuwa ana kipaji hali iliyomfanya ajiamini kwamba anaweza na ndio maana baada ya kuona ubabaishaji mwingi na watu wengi wanatajirika kupitia mgongo wake/kwa jasho lake alion ni bora aachane na muziki na kuamua kuuza kanda za muziki wake na maisha yakawa yanasonga mbele.....Hili watu kama akina Mbaraka Mwinyishehe hawakuliona ndio maana walinyonywa sana na kwa taarifa yako ukinda kwa mke wa Mbaraka Mwinyishehe (mama Taji) atakueleza ni jinsi gani wakenya walitajirika na kipaji cha mume wake na kuiacha familia yake masikini....Kitu hicho mtoto wa Kariakoo Doza alikiona na hakutaka kitokee maishani mwake ndio maana akaachana na muziki na kufungua kijiduka cha kuuza kanda zilizotokana na kipaji chake.......

Ni kweli kwamba Marijani alikosa bendi kwa takribani miaka mitatu au minne.....Hapa ieleweke kwamba alichokosa ni bendi ya kudumu na si kwamba aliacha kabisa kupiga muziki, katika kipindi alichokosa bendi ya kudumu alikuwa akipiga deiwakakatika bendi za Mwenge Jazz ya Dsm na Kurugenzi Jazz ya Arusha mpaka alipoungana na wenzake kuunda kundi la Tanzania Stars na baadae kuanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Nataka nimwambie Gang Chomba kwamba Marijani amewahi kuanzisha bendi moja tu ya Afri Culture ambayo hakudumu nayo,ilikufa kutokana na uchakavu na ukosefu wa vyombo, bendi nyingine zote alizopitia za STC, Safari Trippers na Dar International alizikuta zimeanzishwa na wengine mfano Dar International ilianzishwa mwaka 1977 na mwanamuziki mwingine Nguli nchini Abel Barthazar akiwa na Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff na Marijani alijiunga baadae mwaka huohuo na kujiengua mwaka 1978 na mara baada ya kujiengua bendi hiyo ilisambaratika......Sababu kubwa ya bendi hii kusambaratika ni baada ya kupata umaarufu wa ghafla baada ya Marijani kujiunga nayo na umaarufu huo ghafla ni kwa sababu Marijan Rajab aliifanya bendi ipige muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na bendi yao kipenzi ya Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo mwaka 1978 (miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).

Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....Alikaa na Dar International iliyozaliwa upya mpaka mwaka 1986 bendi hiyo ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo na mmiliki wake kushindwa kuiendesha hali iliyopelekea Marijani aamue kutulia tu na kuamua kufanya Deiwaka Mwenge Jazz na Kurugenzi Jazz mpaka mwaka 1992 alipoanzisha bendi yake ya Afri Culture ambayo hata hivyo haikukaa sana, ilikufa kutokana na uchakavu wa vyombo....

Kitu pekee kilichokuwa kikimsumbua Marijani Rajabu ni uwezo mdogo/umasikini, hakuwa na uwezo wa kununua vyombo na hakufaidika kwa namna yoyote na muziki wake zaidi ya kuwafaidisha wamiliki wa bendi alizokuwa akizitumikia na ndio maana mwaka 1992 aliamua kuachana na muziki na
kufungua kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo ili angalau afaidi matunda ya kazi zake ....Pamoja na watu kumfuata ajiunge na bendi zao Marijani aligoma na maradhi ya moyo(ulikuwa mkubwa) yaliyokuwa yakimsumbua yalizidi mpaka mauti yalipomfika tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo hayo ya moyo kuwa mkubwa.....

Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya mashairi ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nne miaka hiyo....

Siku zote mtu mwenye kipaji hujiamini na hapendi kuburuzwa kutokana na kipaji chake hali ambayo humfanya mtu ahisi kwamba ni mchoyo/mbinafsi.....Mfano mzuri ni Haruna Moshi Shaaban a.k.a Boban wa Coastal Union ya Tanga....
 
Back
Top Bottom