Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Siyo mm ni sababu ya mapendo...kumkosa kijana yule..... Marijani alikuwa na sauti nzuri sana na muziki wake kwa.ujumla ulikuwa mzuri
 
Mkuu Marijani Rajabu alikuwa wanafunzi wa Mbaraka Mwishekh, hata hivyo kila mmoja alikuwa na zama zake.
 
Kama tutakubaliana kuwa Mbaraka alikuwa ndiye Franco wa Tanzania basi naomba Maneti na Marijani wafuate nyuma yake.

Mbaraka sio tu kuimba tungo nyeti lakini mpini wake unautimamu wake
 
Marijani Rajabu ni mkali ile mbaya. Hakuna wa kumkamata. Haijapata kutokea na sijui kama itakuja kutokea akapatikana mkali zaidi yake.
Bado hajapatikana mwingine hadi sasa hivi?
 
Marijani .
Sio tu kwamba ni jabali wa muziki ila pia ni nguli haswa wa medani ya muziki wa dansi.
Ndio maaana hata chama cha muziki wa dansi tanzania (chamudata) kilimtangaza kuwa ndio mwanamuziki wa milenium iliyopita.)
Sitaki kuwadharau Mbaraka na Manet, wameitendea haki jamii ya Tanzania kwa upande wa burudani. Lakini Marijani( JABALI) Acha bwana. Huwezi kulinganisha jabali na mawe ya kawaida.
 
Marijani Rajab aliitwa jabari la muziki,
alifanya maajabu,alivumilia mikiki mikiki,
kinachonipa ghadhabu,sanaa ya bongo hailipi,
pamoja na umaarufu wake,ndugu yetu alikufa na dhiki,

sasa kipi ni kipi,maana ufanisi haufanyiki,
-prof.Jay(yataka moyo)
huu ni mfano mdogo kuwa acheni kufananisha jabari na kichuguu!
Marijani ni Bank hao wengine ni vibubu...
 
Ila mkuu kwa nyimbo zenye ujumbe Hemed Maneti Ulaya aka Chiriku naye sio wa kumbeza, hebu tafuta hizi nyimbo usikilize ujumbe uliomo: Kuruka ukuta, Aza, Stella mtoto mwenye fikara nzuri, Jiko limenuna, Madaraka kwenye bar, Mary Maria na Magdalena halafu uje umalizie na Nilitaka iwe siri pamoja na ule aliokuwa anamsifia mke wake Chiku.

Lakini pamoja na kwamba hizo nyimbo zina ujumbe lakini nimenote tatizo lake nyimbo zake nyingi zilikuwa za mapenzi ingawa yeye alikuwa anaimbia bendi inayomilikiwa na chama cha siasa, hicho ndo kinachokuja kumpa Marijani credit kwa sababu alikuwa anagusa karibia kila angle ya maisha.

Kuna ule wimbo wa ukombozi, nadhani unaitwa sikitiko, na nyingine kama dunia imekwisha, dunia uwanja wa fujo na ukitaka kujua sauti yake ilikuwa decibel ngapi sikiliza wimbo unaitwa Mpenzi Aisha. Kweli Jabali la mziki.

Mbaraka naye pamoja na kwamba nyimbo zake nyingi ni fupi fupi na anarudia rudia sana verse, lakini nazo zina meseji: nyimbo kama Shida, Baba Mdogo, Regina, Dina.
Unaweza ukawa sahihi lakini kwa heshima hebu mweke Maneti kando kwanza.. Hana sifa yoyote kwa namna yoyote ile kumlinganisha na hawa wakongwe. Tutakuwa hatuutendei haki muziki
 
Kwanza sioni sababu ya kumuingiza Marehemu Hemedi Maneti hapa, naheshimu sana kazi na kipaji cha Maneti, ila si haki kumuingiza kwenye ushindani na haya MAGWIJI WAWILI.

Nilichokiona kwa Mbaraka pamoja na kipaji, pia alikuwa Mtafutaji/Mfanyabiashara na mwenye mitazamo ya mbali sana kikazi, ndio maana hakutulia, alikuwa anahangaikia sana kazi zake kwenda Kenya kufuata studio bora ili kuhakikisha kazi zake zinatoka katika ubora, na hata ukisikiliza nyimbo za Mbaraka zipo kwenye ubora ukilinganisha na za Watanzania wengine ingawa alirekodi miaka ya nyuma sana.

Hata kifo chake kilitokana na ajali ya gari katika mihangaiko yake hiyo.

Ni bahati mbaya sana kuwa Mbaraka alituacha mapema, tangu 1979 hakuwepo tena kwenye anga ya Muziki.

Pia yaonyesha Mbaraka alikuwa na uwezo wa kuongoza/kusimamia kundi/bendi, inaonyesha Mbaraka alikuwa Mtu Mtulivu ukilinganisha na Marijani ambaye stori zake nyingi zinaashiria alikuwa 'Mtoto wa Mjini' sana.

Marijani alikuwa Mtunzi na mwenye uwezo mkubwa wa kupangilia kisa cha aina yoyote kuwa kwenye muziki na kikavutia kusikiliza.

Tukiwashindanisha kiutunzi nyimbo za Marijani zinaishi na zitaishi sana masikioni mwa kila kizazi, na zipo nyingi...tukikaa chini wawili wewe uorodheshe za Mbaraka na Mimi huku za Marijani nitakuacha mbali sana.

Kama tuki imagine sifa alizonazo mmoja aongezewe mmoja bado Marijani atatisha kwa mbali sana.
 
Wakuu wangu Gang Chomba na Nkwingwa Masuke.....Nataka tu niwaambie kwamba....

Kitu pekee ambacho watu walikuwa hawakijui kwa Marijani ni kwamba alikuwa hapendi kunyonywa/kukandamizwa na alikuwa ana kipaji hali iliyomfanya ajiamini kwamba anaweza na ndio maana baada ya kuona ubabaishaji mwingi na watu wengi wanatajirika kupitia mgongo wake/kwa jasho lake alion ni bora aachane na muziki na kuamua kuuza kanda za muziki wake na maisha yakawa yanasonga mbele.....Hili watu kama akina Mbaraka Mwinyishehe hawakuliona ndio maana walinyonywa sana na kwa taarifa yako ukinda kwa mke wa Mbaraka Mwinyishehe (mama Taji) atakueleza ni jinsi gani wakenya walitajirika na kipaji cha mume wake na kuiacha familia yake masikini....Kitu hicho mtoto wa Kariakoo Doza alikiona na hakutaka kitokee maishani mwake ndio maana akaachana na muziki na kufungua kijiduka cha kuuza kanda zilizotokana na kipaji chake.......

Ni kweli kwamba Marijani alikosa bendi kwa takribani miaka mitatu au minne.....Hapa ieleweke kwamba alichokosa ni bendi ya kudumu na si kwamba aliacha kabisa kupiga muziki, katika kipindi alichokosa bendi ya kudumu alikuwa akipiga deiwakakatika bendi za Mwenge Jazz ya Dsm na Kurugenzi Jazz ya Arusha mpaka alipoungana na wenzake kuunda kundi la Tanzania Stars na baadae kuanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Nataka nimwambie Gang Chomba kwamba Marijani amewahi kuanzisha bendi moja tu ya Afri Culture ambayo hakudumu nayo,ilikufa kutokana na uchakavu na ukosefu wa vyombo, bendi nyingine zote alizopitia za STC, Safari Trippers na Dar International alizikuta zimeanzishwa na wengine mfano Dar International ilianzishwa mwaka 1977 na mwanamuziki mwingine Nguli nchini Abel Barthazar akiwa na Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff na Marijani alijiunga baadae mwaka huohuo na kujiengua mwaka 1978 na mara baada ya kujiengua bendi hiyo ilisambaratika......Sababu kubwa ya bendi hii kusambaratika ni baada ya kupata umaarufu wa ghafla baada ya Marijani kujiunga nayo na umaarufu huo ghafla ni kwa sababu Marijan Rajab aliifanya bendi ipige muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na bendi yao kipenzi ya Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo mwaka 1978 (miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).

Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....Alikaa na Dar International iliyozaliwa upya mpaka mwaka 1986 bendi hiyo ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo na mmiliki wake kushindwa kuiendesha hali iliyopelekea Marijani aamue kutulia tu na kuamua kufanya Deiwaka Mwenge Jazz na Kurugenzi Jazz mpaka mwaka 1992 alipoanzisha bendi yake ya Afri Culture ambayo hata hivyo haikukaa sana, ilikufa kutokana na uchakavu wa vyombo....

Kitu pekee kilichokuwa kikimsumbua Marijani Rajabu ni uwezo mdogo/umasikini, hakuwa na uwezo wa kununua vyombo na hakufaidika kwa namna yoyote na muziki wake zaidi ya kuwafaidisha wamiliki wa bendi alizokuwa akizitumikia na ndio maana mwaka 1992 aliamua kuachana na muziki na kufungua kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo ili angalau afaidi matunda ya kazi zake ....Pamoja na watu kumfuata ajiunge na bendi zao Marijani aligoma na maradhi ya moyo(ulikuwa mkubwa) yaliyokuwa yakimsumbua yalizidi mpaka mauti yalipomfika tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo hayo ya moyo kuwa mkubwa.....

Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya mashairi ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nne miaka hiyo....


Siku zote mtu mwenye kipaji hujiamini na hapendi kuburuzwa kutokana na kipaji chake hali ambayo humfanya mtu ahisi kwamba ni mchoyo/mbinafsi.....Mfano mzuri ni Haruna Moshi Shaaban a.k.a Boban wa Coastal Union ya Tanga....
Ama kweli wewe ni hazaina tosha habari uliyoandika ni sahihi kabisa Marijani Rajabu alikuwa jabali la muziki haswa. Lakini nina shida moja najua kwamba Marijani alianzisha mtindo wa Mahepe ngoma ya wajanja na hata nimewahi kusikia hata baadhi ya nyimbo kwenye kumbi lakini hadi sasa sijapata kuzisikia zikipigwa popote je ni kwamba hakuzirekodi?
 
Huyu jamaa alikuwa kiboko ndiyo sorolist namba moja aliyeweza kupiga gita la nyuzi 12 pamoja na kuimba wakati huo huo kipindi hicho alikuwa yeye na marehemu Rashid Hanzuruni wa Kiko kids Tabora
Mkuu JB, mimi natamba kuwa nilikuwepo wakati huo na nilingia muziki wa Mbaraka Mwinshehe mwaka 1972.
Huyu bwana ni Maestro, hana mwenzake.
Vocals zake zilikuwa nyororo na poetic na solo ndo usiseme.
Maudhui ya tungo zake zilikuwa zinagusa jamii nzima.
Mkuu umenikumbusha enzi ambazo sasa hazipo kabisa, tungo zilizo tamba
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mpenzi wa mapenzi..."
"Twawapongeza waandishi wetu"
"Expo 70"
"Hiloo oh oh ulijidai wewe mbabe sana"
"Moro yapendeza"

Na vibao vingine vingi.
Hii haina maana kuwa Jabali la muziki na Maneti hawakuwa wazuri,wakati wa Mbaraka hawa walikuwa watoto wadogo kimuziki.
Hata hivyo waliliendeleza libeneke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kinachomfanya marijani kuwa juu ya Mbaraka Mwinshehe ni aina ya tungo zake.. Tungo za marijani ni sawa na hadithi.. Mara nyingi tungo zake zilianza na A na kwisha na Z.. Kama mnaufahamu wimbo wake wa ndoa ya mateso ndo mtaelewa ninamaanisha nini.. Pia alikuwa anaingiza sana nahau na methali kwenye nyimbo zake.. Kitendo cha mashairi ya wimbo wake wa mwanameka kutumiwa kwenye mtihani wa kitaifa wa form 4 mwishoni mwa miaka ya 80 (au mwanzoni mwa 90) ni kielelezo tosha kwamba Marijani ni nguli aliesimama pekee juu..
Maneti hakustahili kuwepo kwenye hili kundi..
umenena vyema ila umekosea kumshusha kiasi hicho Maneti labda iwe hakustahili kuwepo kwa kulinganisha mitindo yao sababu ilikuwa tofauti, huyo aliitwa Chiriku fatilia tungo zake zilivyopangiliwa na sauti nzuri ikizipamba. Hemed Manet Ulaya alikuwa ni Gwiji la Muziki Vijana Jazz.
 
Back
Top Bottom