Mkuu wakati anakumbana na umauti Marijani alikuwa ameacha kupiga dansi.. Alikuwa na duka lake ambalo alikuwa anauza nyimbo zake pamoja na nyimbo toka kwa wasanii wengine tofauti.. Kama ninakumbuka sawasawa competitive musik aliachana nao kwenye mwaka 1987 hivi (I stand to corrected)..
Loh! Safi kweliMkuu picha zao mbona zipo sana, fuata hiyo link na Video moja ya Marijani Rajabu.
MBARAKA MWARUKA MWINSHEHE! - BongoCelebrity
KAMANDA WA MATUKIO
Mkuu nadhani hii line inaimbika hivi
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mchezo wa mapenzi..."
Konaball nawakubali hao wawili wa mwanzo ila Maneti mmh sijui, Marijani alikuwa ana powerful voice sikiliza ukewenza, DAH ZUWENA miaka hiyo ya 79-84 nilikuwa Sumbawanga kuna Mwanameka. ila wadau mimi hawa wana SIKINDE NGOMA YA UKAE ya wakati ule ilikuwa inatisha si mchezo, Kuna Huyu jamaa anaitwa Hassan Rehani Bitchuka(wakati ule) sauti yake kwa kweli haikuwa na mpinzani ilikuwa inapanda mpaka mwisho(Highet pitch) sasa hivi kwishnei, nna kanda yao yaani kila ikifika ijumaa naiweka kusikiliza ule wa wimbo wa wikiendi, tufurahi na wana sikinde tucheze leo ngoma ya ukae, ukitaka kufurahi, kila jumamosi njoo uburudike na wana sikinde oyee halafu wanataja majina ya kundi zima enzi hizo akina KING ENOCK, Mwanyiro, Gama, dah mpaka mwili unasisimka. Hapo msondo enzi hizo ilikuwa haioni ndani kwa sikinde, kuna vibao kama Duniani kuna mambo, Selina-WADAU kweli vipaji vilikwepo sasa hivi eti wanamziki wa Ubongo wa Fleva akauambia nilipata idea hiyo hapo hapo nikaanza kuandika verse nikaenda studio nikamkuta DUNGA tukapanga vyombo baada ya nusu saa track imekamilika kweli JAMANI? NDO MAANA INAITWA Bongo Flavour sababu ni ka fleva fulani hivi ka muda wa wiki kadhaa baada ya hapo kwishnei
Kiukweli waliompa Marijani jina la Jabali la Muziki hawakukosea......Huyu bwana alikuwa na kipaji hasa cha kutunga mashairi na ndio maana nyimbo zake mpaka le zinatamba....Hapa hata mimi sina uhakika sana aliacha kuimba lini, ngoja tumuite Balantanda afafanue maana yeye ndo ana kumbu kumbu nzuri na hawa wanamziki wetu wa zamani.
Huyo ndio Jabali la muziki Marijan Rajab na Dar International mkuu...
Marijan Rajab kabla hajahamia Dar International alikuwa katika bendi ya Safari Trippers ambayo ilisambaratika mwaka 1977......Baada ya Safari Trippers kufa nini kilifuata?.....Mwaka huohuo 1977 mwanamuziki mwingine Nguli chini Abel Barthazar alianzisha bendi ya Dar Internatinal ambayo pamoja naye(Balthazar) pia walikuwepo Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,ALi Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......
Bendi hii ilianza kwa kutoka na vibao kama Nyerere mwanamapinduzi,Rufaa ya kifo,Mwana uoe,Betty,Margreth na Sikitiko,....Vibao hiivi vilitamba hasa na bendi ilianza kushika chati ya juu katika medani za muziki wa Dansi Tanzania.....Bendi hii ilikuwa maarufu ghafla na kwa kupitia Marijan Rajab ilipiga muziki wenye mahadhi kama ya ule muziki uliokuwa ukipigwa na Safari Trippers hivyo kuzidi kumletea umaarufu Marijan Rajab kitu ambacho inadaiwa hakikupendezwa sana na wanamuziki wengine akiwemo Abel Barthazar ambao waliona kwamba watu wanaichukulia Dar International kama Safari Trippers....Walianza kumpiga vita Marijan Rajab ambaye hakupendezwa na hali hiyo hivyo kuamua kujitoa katika bendi hiyo(miezi 9 tu baada ya bendi kuanzishwa).....Mwaka 1978 baada ya Marijan Rajab kujiondoa bendi haikudumu sana kwani ilisambaratika baada ya wanamuziki nane(08) tegemeo wa bendi hiyo Abel Barthzar(aliondoka kabla ya wenzie),King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jef waliondoka na kwenda kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra(baadae DDC Mlimani Park Orchestra).....
Baada ya bendi kusambaratika,mmiliki wa Dar International Zachariah Ndebame alimuomba Marijan Rajab arudi kwa ajili ya kuisuka upya bendi hiyo ambapo alikubali na kurudi rasmi kwenye bendi,hapo akakutana na mpiga solo Hamza Kasongo ambaye kwa kushirikiana waliiongoza bendi hiyo kutoa vibao vitamu kama Zuwena,Vick na Mayasa......Vibao hivi viliurudisha umaarufu wa bendi hii kiasi cha kuzitisha bendi ilizozikuta zikitamba wakati huo kama Vijana Jazz,Juwata Jazz,Mlimani Park,Marquiz na Biashara Jazz.....Hali hii ilileta ushindani mkubwa miongoni mwa bendi hizo.....Baadae bendi hii ilipata wanamuziki chipukizi kama Fresh Jumbe ,Tino Masinge 'Arawa', Mohammed Mwinyikondo na wengine na kurekodi vibao vitamu kama Mzee Said,Baba Anna,Masudi amekuwa jambazi,Bwana Mashaka,Pondamali kufa kwaja, Mwajuma, Pendo si kulazimishana, Usimtese Mwana, Chakubanga na nyingine nyingi zilizotamba na kufunika ile mbaya enzi hizo.....
Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........
Hao ndio Dar International Orchestra wana Super bomboka chini yake Jabali la muziki Hayati Marijan Rajab(R.I.P)......
Mkuu wewe mkali unatisha nashukuru kwa kumfahamu MARIJANIKiukweli waliompa Marijani jina la Jabali la Muziki hawakukosea......Huyu bwana alikuwa na kipaji hasa cha kutunga mashairi na ndio maana nyimbo zake mpaka le zinatamba....
Kwa kifupi Marijani Rajabu alikuwa mkali zaidi ya wote hao.....
Kihistoria kwa kifupi sana Marijani alizaliwa Kariakoo mwaka 1954 na alianza muziki mwaka 1972 akiwa na bendi ya STC Jazz ambayo hakukaa nayo sana kwani mwaka huohuo alihamia bendi ya Safari Trippers na baadae mwaka 1977 alijiunga na Dar International ( wana Super Bomboka) ambako alikutana na akina Abel Balthazar, Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......
Marijani alikaa na Dar International hadi mwaka 1986 bendi ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo....Naada ya Dar International kuvunjika Marijani alikosa bendi lakini baadae aliungana na wanamuzaiki wenzake zaidi ya 50 waliotamba miaka hiyo ya katikati na mwishoni mwa 80 na kuunda kundi(Zing zong) la Tanzania Stars .....Baadae katika kutafuta mkate wa kila siku Marijani alipiga Deiwaka Mwenge Jazz na baadae akajiunga na Kurugenzi Jazz ya Arusha na mwanzoni mwa miaka ya 90 akaanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Kundi hili lilikuwa likitumia vyombo vya kukodi/kuazima na halikudumu sana hali iliyopelekea kuvunjika mwanzoni mwa mwaka 1992....
Baada ya Afri Culture kufa hali ya Marijani kiuchumi ilikuwa mbaya sana hali iliyomlazimu afungue kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo mpaka mauti yalipomfika tarehe tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo ya moyo kuwa mkubwa.....Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nnne miaka hiyo....
Ingawa Historia yake ni ndefu sana lakini kwa kifupi sana naweza kusema hiyo ndiyo Historia fupi ya MARIJANI RAJABU a.k.a Bulldozer a.k.a Doza a.k.a JABALI LA MUZIKI
Ndo maana nikapendekeza uje hapa utoe ufafanuzi, asante sana kwa ufafanuzi, na ni kweli pia alitaka kujiunga na Club ya Simba maana inasemekena pia alikuwa na kipaji cha mpira hasa nafasi ya Kaseja?Kiukweli waliompa Marijani jina la Jabali la Muziki hawakukosea......Huyu bwana alikuwa na kipaji hasa cha kutunga mashairi na ndio maana nyimbo zake mpaka le zinatamba....
Kwa kifupi Marijani Rajabu alikuwa mkali zaidi ya wote hao.....
Kihistoria kwa kifupi sana Marijani alizaliwa Kariakoo mwaka 1954 na alianza muziki mwaka 1972 akiwa na bendi ya STC Jazz ambayo hakukaa nayo sana kwani mwaka huohuo alihamia bendi ya Safari Trippers na baadae mwaka 1977 alijiunga na Dar International ( wana Super Bomboka) ambako alikutana na akina Abel Balthazar, Joseph Mulenga,Abdallah Gama,Cosmas Thobias Chidumule,Ali Rajab,Belesa Kakere,Marijan Rajab,Machaku Salum,King Michael Enock,Joseph(Yusuph) Bernard na Habib Jeff.......
Marijani alikaa na Dar International hadi mwaka 1986 bendi ilipokufa kutokana na uchakavu wa vyombo....Naada ya Dar International kuvunjika Marijani alikosa bendi lakini baadae aliungana na wanamuzaiki wenzake zaidi ya 50 waliotamba miaka hiyo ya katikati na mwishoni mwa 80 na kuunda kundi(Zing zong) la Tanzania Stars .....Baadae katika kutafuta mkate wa kila siku Marijani alipiga Deiwaka Mwenge Jazz na baadae akajiunga na Kurugenzi Jazz ya Arusha na mwanzoni mwa miaka ya 90 akaanzisha kundi lake la Afri Culture ambalo lilikuwa likitumia mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya wajanja' . Kundi hili lilikuwa likitumia vyombo vya kukodi/kuazima na halikudumu sana hali iliyopelekea kuvunjika mwanzoni mwa mwaka 1992....
Baada ya Afri Culture kufa hali ya Marijani kiuchumi ilikuwa mbaya sana hali iliyomlazimu afungue kijiduka kidogo cha kuuza nyimbo zake pale Kariakoo mpaka mauti yalipomfika tarehe tarehe 23/03/1995 kutokana na matatizo ya moyo kuwa mkubwa.....Pamoja na uwezo/kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika kutunga na kuimba Marijani alikuwa na maisha magumu sana mpaka umauti unamfikia.....Alikufa maskini mno licha ya nyimbo zake kutamba na nyingine (Mwanameka) kutumiwa na NECTA hata kwenye mtihani wa kidato cha Nnne miaka hiyo....
Ingawa Historia yake ni ndefu sana lakini kwa kifupi sana naweza kusema hiyo ndiyo Historia fupi ya MARIJANI RAJABU a.k.a Bulldozer a.k.a Doza a.k.a JABALI LA MUZIKI
Hii niliiweka siku za nyuma nikimzungumzia Marijani Rajabu na Dar International....
Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Bomboka.......Nyimbo nyingine zilizotamba za bendi hii ni pamoja na Mwanameka, Ukewenza, Sababu ya Mapendo, Usia wa Baba, Aisha Mtoto wa Mwanza, Siwema, Mama Maria, Paulina, Mateso ya ndoa, Ponda Mali Kufa Kwaja, Amekosa Nini Mama, Pesa Sabuni ya Roho, Ukatili Ni Unyama, Siwema No. 2, Mwana Acha Kidomo Domo, Mpenzi Christina, Uzuri wa Asali, Ninamsaka Mbaya Wangu, Emmy, Umevunga Ahadi, Alinacha, Nitajirekebisha, Ndugu Umepotea, Baba Anita, Ndugu umepotea No. 2, Pendo, Pombe si chai, Esther, Baruti, Vicky, Uzuri wa asili, Mapambano yanaendelea, Mwana mpotevu na nyingine nyingi...........
Ila mkuu kwa nyimbo zenye ujumbe Hemed Maneti Ulaya aka Chiriku naye sio wa kumbeza, hebu tafuta hizi nyimbo usikilize ujumbe uliomo: Kuruka ukuta, Aza, Stella mtoto mwenye fikara nzuri, Jiko limenuna, Madaraka kwenye bar, Mary Maria na Magdalena halafu uje umalizie na Nilitaka iwe siri pamoja na ule aliokuwa anamsifia mke wake Chiku.Kwanza kumuingiza Maneti humu ni kumuonea, Mbaraka na Marijani wanasimama kivyao. Ila kwa maoni yangu....na ndivyo ilivyo kwa kweli...MARIJANI bado hajatokea nchini. na tusibishane sana wanaosema Mbaraka waorodheshe nyimbo zake zilizowagusa na wanaosema Marijani wafanye hivyo, Wa Mbaraka watakaa. Nyimbo za Marijani hazichoshi kusikiliza na zimejaa ujumbe......
Jua laniangazia
Dada acha uvivu
Salama
Viki mtoto wa mama
Pombe sio chai
Matilda mtunze mwanao
Christina mapenzi yako yanipa wazimu
JABALI LA MUZIKI hana mpinzani na kwa kumuenzi huyu bwana hizi TUZO ZA KILI zingepewa jina lake.
Ndo maana nikapendekeza uje hapa utoe ufafanuzi, asante sana kwa ufafanuzi, na ni kweli pia alitaka kujiunga na Club ya Simba maana inasemekena pia alikuwa na kipaji cha mpira hasa nafasi ya Kaseja?
Ngoja nimuite mwenyewe aje, Balantanda nkwingwa njoo huku uzidi kutoa ufafanuzi kulingana na swali la mkuu Gang Chomba.Naomba umuulize Balantanda je kwa umahiri na ujabali wa Marijani je ilikuwaje akose bendi ya kuimba na kukaa benchi takriban miaka mitatu toka 1986 mpaka 89?
Na je pamoja na ujabali wake ilikuwaje Bendi alizoanzisha hazikuwa kali kama ambazo alikuta zimeshaanzishwa na yeye akajiunga nazo?
Uchoyo ni hulka ya mtu....Kila mtu ana element za uchoyo.....Hata wewe u mchoyo katika nyanja fulani....Nadhani kama ni suala la uchoyo kwenye muziki basi Marijani asingeshirikiana na mwanamuziki yoyote yule katika kuimba nyimbo na kutengeneza muziki....Kitu pekee ambacho watu walikuwa hawakijui kwa Marijani ni kwamba alikuwa hapendi kunyonywa/kukandamizwa na alikuwa ana kipaji hali iliyomfanya ajiamini kwamba anaweza na ndio maana baada ya kuona ubabaishaji mwingi na watu wengi wanatajirika kupitia mgongo wake/kwa jasho lake alion ni bora aachane na muziki na kuamua kuuza kanda za muziki wake na maisha yakawa yanasonga mbele.....Hili watu kama akina Mbaraka Mwinyishehe hawakuliona ndio maana walinyonywa sana na kwa taarifa yako ukinda kwa mke wa Mbaraka Mwinyishehe (mama Taji) atakueleza ni jinsi gani wakenya walitajirika na kipaji cha mume wake na kuiacha familia yake masikini....Kitu hicho mtoto wa Kariakoo Doza alikiona na hakutaka kitokee maishani mwake ndio maana akaachana na muziki na kufungua kijiduka cha kuuza kanda zilizotokana na kipaji chake.......Balantanda usisahau kuwaambia hao kuwa Marijani ana sifa pekee ya uchoyo.
Naomba umuulize Balantanda je kwa umahiri na ujabali wa Marijani je ilikuwaje akose bendi ya kuimba na kukaa benchi takriban miaka mitatu toka 1986 mpaka 89?
Na je pamoja na ujabali wake ilikuwaje Bendi alizoanzisha hazikuwa kali kama ambazo alikuta zimeshaanzishwa na yeye akajiunga nazo?
Ngoja nimuite mwenyewe aje, Balantanda nkwingwa njoo huku uzidi kutoa ufafanuzi kulingana na swali la mkuu Gang Chomba.