Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Siyo mm ni sababu ya mapendo...kumkosa kijana yule..... Marijani alikuwa na sauti nzuri sana na muziki wake kwa.ujumla ulikuwa mzuri
 
Mkuu Marijani Rajabu alikuwa wanafunzi wa Mbaraka Mwishekh, hata hivyo kila mmoja alikuwa na zama zake.
 
Kama tutakubaliana kuwa Mbaraka alikuwa ndiye Franco wa Tanzania basi naomba Maneti na Marijani wafuate nyuma yake.

Mbaraka sio tu kuimba tungo nyeti lakini mpini wake unautimamu wake
 
Marijani Rajabu ni mkali ile mbaya. Hakuna wa kumkamata. Haijapata kutokea na sijui kama itakuja kutokea akapatikana mkali zaidi yake.
Bado hajapatikana mwingine hadi sasa hivi?
 
Marijani .
Sio tu kwamba ni jabali wa muziki ila pia ni nguli haswa wa medani ya muziki wa dansi.
Ndio maaana hata chama cha muziki wa dansi tanzania (chamudata) kilimtangaza kuwa ndio mwanamuziki wa milenium iliyopita.)
Sitaki kuwadharau Mbaraka na Manet, wameitendea haki jamii ya Tanzania kwa upande wa burudani. Lakini Marijani( JABALI) Acha bwana. Huwezi kulinganisha jabali na mawe ya kawaida.
 
Marijani Rajab aliitwa jabari la muziki,
alifanya maajabu,alivumilia mikiki mikiki,
kinachonipa ghadhabu,sanaa ya bongo hailipi,
pamoja na umaarufu wake,ndugu yetu alikufa na dhiki,

sasa kipi ni kipi,maana ufanisi haufanyiki,
-prof.Jay(yataka moyo)
huu ni mfano mdogo kuwa acheni kufananisha jabari na kichuguu!
Marijani ni Bank hao wengine ni vibubu...
 
Unaweza ukawa sahihi lakini kwa heshima hebu mweke Maneti kando kwanza.. Hana sifa yoyote kwa namna yoyote ile kumlinganisha na hawa wakongwe. Tutakuwa hatuutendei haki muziki
 
Kwanza sioni sababu ya kumuingiza Marehemu Hemedi Maneti hapa, naheshimu sana kazi na kipaji cha Maneti, ila si haki kumuingiza kwenye ushindani na haya MAGWIJI WAWILI.

Nilichokiona kwa Mbaraka pamoja na kipaji, pia alikuwa Mtafutaji/Mfanyabiashara na mwenye mitazamo ya mbali sana kikazi, ndio maana hakutulia, alikuwa anahangaikia sana kazi zake kwenda Kenya kufuata studio bora ili kuhakikisha kazi zake zinatoka katika ubora, na hata ukisikiliza nyimbo za Mbaraka zipo kwenye ubora ukilinganisha na za Watanzania wengine ingawa alirekodi miaka ya nyuma sana.

Hata kifo chake kilitokana na ajali ya gari katika mihangaiko yake hiyo.

Ni bahati mbaya sana kuwa Mbaraka alituacha mapema, tangu 1979 hakuwepo tena kwenye anga ya Muziki.

Pia yaonyesha Mbaraka alikuwa na uwezo wa kuongoza/kusimamia kundi/bendi, inaonyesha Mbaraka alikuwa Mtu Mtulivu ukilinganisha na Marijani ambaye stori zake nyingi zinaashiria alikuwa 'Mtoto wa Mjini' sana.

Marijani alikuwa Mtunzi na mwenye uwezo mkubwa wa kupangilia kisa cha aina yoyote kuwa kwenye muziki na kikavutia kusikiliza.

Tukiwashindanisha kiutunzi nyimbo za Marijani zinaishi na zitaishi sana masikioni mwa kila kizazi, na zipo nyingi...tukikaa chini wawili wewe uorodheshe za Mbaraka na Mimi huku za Marijani nitakuacha mbali sana.

Kama tuki imagine sifa alizonazo mmoja aongezewe mmoja bado Marijani atatisha kwa mbali sana.
 
Ama kweli wewe ni hazaina tosha habari uliyoandika ni sahihi kabisa Marijani Rajabu alikuwa jabali la muziki haswa. Lakini nina shida moja najua kwamba Marijani alianzisha mtindo wa Mahepe ngoma ya wajanja na hata nimewahi kusikia hata baadhi ya nyimbo kwenye kumbi lakini hadi sasa sijapata kuzisikia zikipigwa popote je ni kwamba hakuzirekodi?
 
Huyu jamaa alikuwa kiboko ndiyo sorolist namba moja aliyeweza kupiga gita la nyuzi 12 pamoja na kuimba wakati huo huo kipindi hicho alikuwa yeye na marehemu Rashid Hanzuruni wa Kiko kids Tabora
Sent using Jamii Forums mobile app
 
umenena vyema ila umekosea kumshusha kiasi hicho Maneti labda iwe hakustahili kuwepo kwa kulinganisha mitindo yao sababu ilikuwa tofauti, huyo aliitwa Chiriku fatilia tungo zake zilivyopangiliwa na sauti nzuri ikizipamba. Hemed Manet Ulaya alikuwa ni Gwiji la Muziki Vijana Jazz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…