NANI ZAIDI: Nilikuwa na Mashaka na Simba kumbe ni kweli wanatumia fumbate

NANI ZAIDI: Nilikuwa na Mashaka na Simba kumbe ni kweli wanatumia fumbate

Mambo ya kuzidiana followers mtandaoni sio kipimo cha kuaminika cha timu kuwa na mashabiki wengi , uwezo nk mfano Diamond kamzidi Burna boy , Wizkidayo pamoja nawasanii wengine wakubwa kwa subscribers youtube lakini wakina Burna wanajua shows viwanja vikubwa na kuchukua tuzo kubwa kubwa na kumpiga group kubwa Diamond japo yeye ni King kwenye mitandao ya kijamii.

Sijui kama wataelewa na hili.

Simple & Clear.
 
Yanga ni timu ndogo sana ila nimegundua ina ndoto za kukua ila mbinu iliyojichagulia siioni kama italeta matunda


Mimi nadhani YANGA SC sio timu ndogo kwa sababu ina mataji mengi zaidi ya Ligi Kuu kuliko SIMBA SC.

Simba SC wanajivunia kimataifa ili hali they have nothing to show for it.
 
Mimi nadhani YANGA SC sio timu ndogo kwa sababu ina mataji mengi zaidi ya Ligi Kuu kuliko SIMBA SC.

Simba SC wanajivunia kimataifa ili hali they have nothing to show for it.
Mataji mengi mangapi?
 
Mleta mada naomba nikukumbushe Tu mambo kadhaa kuhusu Simba

1.Simba ndy club yenye vibe mtandaoni kuliko club yoyote kusini mwa jangwa la Sahara,na linapokuja swala km Hilo linakuwa km kumsukuma mlevi tu Kwa mashabiki wa simba

2.kwenye mitandao ya kijamii Simba imemwacha mbali sn yanga Kwa followers
Simba 934,000 wakati yanga 192,000(Twitter pekee)
Umejifunza nini hapa kuhusu hili linaloendelea?

3.Siku kadhaa nsemaji wenu white aliwahi kukiri kwamba Simba imemwacha mbali sn yanga kwenye hamasa za mtandaoni.Huoni hili Kwa Simba ni km kumwambia mtoto avunje biskuti?

4.Point yangu ya mwisho ni hii;Umesema kwamba huko nyuma Simba ilichangisha mil 60 Tu lkn umesahau kwamba wakati ule ilikuwa haishindani na yeyote lkn Simba linapokuja swala la kushindana,mashabiki wa Simba ni km wanakuwa vichaa Kwa kuisapoti timu Yao
Huko Twitter kwenye scandal ya mamilioni ya accounts fake ndio unatumia kama reference yako?
 
Jibu lako ni hili:

Simba ilianza mapema zaidi kufanya social media investiment.

Followers wote hao sio mashabiki wa simba.

Kama mnawafuasi na mashabiki wengi kwanini YANGA SC iliwapiga gape kubwa kwenye mapato ya gate collection msimu ulio pita?
Kwanza Twitter ina scandal ya account fake,Mwamedi anavyopenda sifa ashindwi kuwa na kikosi kazi cha I.T specialist wa kutengeneza accounts fake
 
Whydad ina follower 1m, etoil du sahel ina followers 100k, Es tunis ina followers 397k kwenye mtandao wa Instagram. Je hizo timu ni ndogo na za kawaida?

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
Hapana ukubwa wao unaonekana katika makombe wanavyochukuwa shida inakuja kama makombe ya club bingwa huchukui na hata ushiriki katika group stages yoyote na umepitwa kwa followers automatically ww ni timu ndogo kama ilivyokuwa Yanga mbele ya Simba
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana suala la hii kampeni ya Nani Zaidi?

Kwa uwiano uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga, inawezekana vipi wapiga kura wa Simba wawe wengi mara mbili zaidi kuliko wale wa watani zao Yanga?

Hata ukizingatia tu uwezo na msukumo wa uchangiaji kutoka kwenye kampeni yao ya Ujenzi wa uwanja...Huwezi kuona uhalisia baina ya kapeni hizi mbili.

(kumbuka kuwa Simba walitumia miezi 6 kufikisha milioni 60)

Tena kwa kutumia michango ya mashabiki. Tena pasi na kuwekewa kuwango zuizi cha uchangiaji!

Sasa wamewezaje kufika milioni 100 ndani ya mwezi mmoja...? [emoji23][emoji23]

Ukitumia ubongo wako mpenzi msomajinutagundua kuwa kampeni ya uchangiaji ilivamia na FUMBATE ya kuhamisha pesa ya klabu yao kwa lengo la kuwaaminisha wanachama na mashabiki wao kuwa wako vizuri, wakijua wazi kuwa mashabiki wao wataamini na hawatoweza hata kujiuliza maswali magumu.

Leo katika mkutano wa waandishi wa Habari wa klabu ndipo nikapata kuthibitisha shaka yangu kuwa niko sahihi 100%

Idara ya Klabu ya Yanga iliweka wazi mbinu iliyoyumika na simba ili kuuaminisha watu wao kuwa hawawezi kushindwa na Yanga kwenye kila kitu msimu huu.

Walichokifanya ni kutoe pesa mfuko wa kushoto na kupeleka kulia ili kuonyesha kuwa wako safi.

Hongereni Simba SC lakini msisahau kusajili kwa kuwa dirisha la CAF limesalia siku chache kutoka hii leo.
View attachment 2259739
Fedha wamehamisha sawa, kura nazo imekuwaje?
 
Bado niko pale pale uwingi wa followers kwenye mitandao ya kijamii HAU-AKISI wingi halisi wa MASHABIKI.


Kama ingekuwa UWINGI wa followers una AKISIKA katika kupima idadi ya MASHABIKI...YANGA SC asingeongoza kwa idadi ya mapato ya getini msimu 2020/21.
Kumbuka mapato ya mlangoni hayachangiwi na mashabiki wa Yanga pekee.
Labda nikuambie na ufanye utafiti mechi zijazo.
Inapocheza Yanga washabiki wa Simba wengi wanaingia kuona mchezo.
Inapocheza Simba washabiki wa Yanga wanakuwa kidogo sana.

Hivyo get collection ya Yanga inachangiwa sana na washabiki wa Simba kuliko kinyume chake.

Fanya utafiti mechi zijazo utaliona hili.
 
Kwa faida ipi? Mwamedi anafanya hivyo ili kuwapumbaza nyie mambumbumbu ili kuwapoza kwa machungu ya makombe msimu huu
Una ushahidi na unachosema ?
Kauli za mkosaji hizo.
Mwambieni GSM na Rostam nao wachangie maana wana pesa kumzidi MO.
 
Hata mechi ya Yanga na Simba ya mwisho uwanja wa Mkapa Mashabiki wa Yanga walikuwa wachache kuliko wale wa Simba.
Muwe mnakubali vitu vingine na sio kujiona ninyi ni bora maeneo yote.

Mngeongoza kwa michango msingeongea haya.
Kwa Africa Simba ni kati ya timu tano bora zinazojaza washabiki wake wengi uwanjani.
Takwimu zipo, hadi CAF wanawaruhusu kuingiza washabiki wengi kwenye mechi zao.
Kocha Ibenge amekiri hili. vipi mlishangae
 
Jibu lako ni hili:

Simba ilianza mapema zaidi kufanya social media investiment.

Followers wote hao sio mashabiki wa simba.

Kama mnawafuasi na mashabiki wengi kwanini YANGA SC iliwapiga gape kubwa kwenye mapato ya gate collection msimu ulio pita?
Washabiki wa simba ni vijana na wanapenda mpira,wao huingia mechi zote bila kujali nani anacheza,yanga mashabiki wao ni wazee na wamama hawaendi uwanjani wala hawana smart phone
 
Hii miaka minne mfululizo ya Pila Biriani na michuano ya Afrika Simba, imejiongezea washabiki wengi sana ndani na nje ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.

Kutokana na utandawazi wa kuona mpira karibu Tanzania Nzima.
Leo karibu kila Kijiji kina Umeme na wanaangalia mpira wa ndani na wakimataifa.
Ukienda Msumbiji ni hivyo hivyo Azam TV inawapa vijana wa huko Live Mechi zote za hapa nchini.

Timu inayoishia kutolewa makundi raundi ya kwanza miaka nenda rudi huku ikijivunia historia ya mababu zao, haiwezi kuwa kipaumbele kwa kizazi cha sasa kinachopenda soka.
 
Back
Top Bottom