Naoa mwezi wa nane, naombeni ushauri

Hii ni kweli kabisa
 

Unaingia vitani, unaitaji silaha:

1. Za kiroho.
2. Fata sana ushauri wa wazee.
3. Hakikisha una hela.
4. Usifanye mipango na hela ya wife.

Ndoa:

Ngumu sana, nakueleza kijana, ngumu sana nje ya mpango wa Mungu kamilifu.

Ndoa ni jambo lisilowezekana, sijawahi m cheat mke wangu mimi, yeye akanipigia tukio.

Nakueleza kijana, ndoa ngumu sana ndugu, ngumu ndugu yangu.

Kamwe usiamini kitu anakuambia mwanamke, huwezi nielewa, ndoa ngumu sana.
 
Yani wewe Maisha yanaenda kukunyoosha unyooke kama Rula kama akili zenyewe ndio izo.
 
Hapo ndo unaenda kupotea mazma, I tell you yaan tumbo lako tu limekushinda afu unaenda kuongeza matumbo mengne mawili ya kuyalisha utatoboa kweli?

Afu ww umemaliza chuo 2018 then unaona eti umechelewa, umechelewa wapi? Mbona mwenzio nmemaliza chuo mwaka huo huo na sina chochote zaidi ya smartphone na wala sna pressure. Kuna classmate wangu wanapush ndinga kali, wana mijengo, wana ajira/biashara za hela ndefuuuuuu na wala siwazi

Oya: Run ur Race!!
 
Nakazia. Naongezea haya.

Mtoa mada kasema anaoa mwezi wa nane, sasa hata kutishauri si keshapanga tayari ataahirisha?

Pili, swala la baraka si kwa kila mtu na baraka zinatofautiana kama ulivyosema. Kinyume cha baraka ni laana hivyo ategemee matatu.
1. Wakiungana nyota zikubali mambo yawe mazuri
2. Wakiungana nyota zikatae mambo yawe mabaya
3. Wakiungana iwe kwaida tu hakuna tofauti na mwanza

Hapo ni betting. Pia kama ulivyosema bataka zipo nyinyi sio lazima rizik. Unaweza muoa akaleta baraka ya kutokua na mabalaa yaani majanga majanga ya maginjwa, nk yakapita mbali. Unaweza muoa akawa na baraka ya watoto yaani ni mwendo wa akina junior tu.

Kila la heri mkuu
 
 
Wak

Wakuu mnadanganya umma sana. Tunajua nyie mmeoa na life linaenda fresh basi msiwadanganye vijana kuwa wakioa mambo yatakaa sawa ni uongo sana. Tunajua mko na nia njema mnataka vijana waoe na sio kukataa ndoa ila maiwalubuni kwa wakioa mambo yatanyooa. Waambieni ukweli wajitafute walau wawe na uwezo wa kulisha familia kisha waoe.

Hapa ni experience inazungumza. Kuoa haina tofauti na kuwa single kwenye utafutaji lolote linawezabkutokea. Unaweza kuwa choka mbaya baada ya muda ukajipata, unaweza kuwa umejipata baada ya muda ukafilisika, unaweza kuwa huna kitu na ukaendeleankuwa huna kitu na unaweza kuwa umejipa na ukaendelea kuwa hivyo. Yote hay manne yanawesa kutokea ukiwa single au ukiwa umeoa, na sio guarantee kwamba ukioa ukiwa choka mbaya utabadili maisha hapana.

Wanangu ninao wajua wapo waliopitia hizi hali. Ila kuna mmoja alioa akiwa vizuri sana kiuchumi ila sasa hivi ni hio sana. Wengine life linasonga vilevile hakuna mabadiriko. Na kuna wengine ndio kila siku vizinga hali ni ngumu sana kwao. Kuna wanangu kama watatu wao wako vizuri baada ya kuoa ila wote hawa walioa penye kitu ili hali wao hawana kitu. Mmoja alioa binti wa kichaga ambae kwao wako vizuri, hivyo bunti aliwezeshwa ili asiwe tegemezi kwa mwenzie, hadi leo wanasonga fresh sana. Wawili walioa wanawake wenye uchumi mzuri kuliko wao wanaishi poa sana. Na mmoja kati yao wamejenga na wote wana push ndinga ila si kwa nguvu za me, ni ke ndio alikua vizuri yaani ke yupo vizuri kuanzia kwao. Kwa ke hakuna mtu lofa.

Sasa wakuu ni muda wa kutoa shauri za kweli sio kuwadanganya hawa vijana. Binafsi sijaoa na niko earl 30 ila mm sio kataa ndoa nitaoa ni swala la muda tu. Ninachoamini ni kuweka mambo sawa kwanza, nikiamini juhudi ni 99% na bahati ni 1% kama itakuja sawa na kama haitakuja ni sawa pia. Sio kuoa ukitegemea bahati, na ukiikosa.
 
Nilioa nikaacha asaivi natafuta mwingine at least mwenye shepu na mrefu kidogo hawa wafupi na wembamba wana wivu sana

Kuhusu rizk sijui maana sikuona utofauti wa mshahara ninaopokea toka nioe ni uleule haujazidi wala kupungua
 

Jijenge kwanza kabla ya kuoa...

Kama ni kweli kwamba baraka basi kila mwanaume mwenye maisha magumu angelioa...
 
Nilioa nikaacha asaivi natafuta mwingine at least mwenye shepu na mrefu kidogo hawa wafupi na wembamba wana wivu sana

Kuhusu rizk sijui maana sikuona utofauti wa mshahara ninaopokea toka nioe ni uleule haujazidi wala kupungua
 
Anaweza kuja na baraka au laana. Kuna kijana mwenzako alikuja na baraka, kachumbia leo kesho wakwe wakampa connection taasisi rasmi ya kazi. Sasa kama na unayemuoa kwao wanategemea wewe ndo uwatoe kwenye umasikini sijui itakuaje.
 
Nimeukumbuka uzi wa yule jamaa anayelalama mwanaye kutotumia common sense.

Hiihii akili ndiyo ulitobolea chuo mheshimiwa? Au unamaanisha chuo=madrasa?

Jiandae kuwa- disappointed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…