Naomba anayefahamu biashara ya Mbao anipe mchanganuo jinsi ya uendeshaji

1Afica54

Senior Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
115
Reaction score
68
HABARI WANA JAMII FORUM
N
aomba maelekezo juu ya biashara ya mbao
1,upatikanaji
2,usafirishaji
3,jinsi ya UENDESHAJI wa biashara
4, mtaji wa chini kiasi gani
5,namna ya kutafuta soko


 
Pata leseni ya ukusanyaji mazao ya misitu
.chagua mkoa wakununulia mbao sehemu ambapo mbao zinazalishwa kwa wingi mfano iringa, mafinga, njombe,kagera.
Pata watu wakukusanyia mzigo na kulundika eneo ambalo gari inafika kwa urahisi bila shida
.Fahamu ushuru wa halmashauri huska maana ushuru utafautiana kati ya halmashauri na halmashauri ila ushuru kwa ubao mmoja una range shilingi 300 adi 400 kwa ubao.
.kata kibali cha kusafrisha mbao cha TFS ambatanisha na leseni yako ya kukusanyaji mazao ya mistu pamoja na lisiti ya ushuru wa halmashauri ulipo chukulia mbao. Kabla ya kukata kibali cha kusafirisha mbao hakikisha umepata gari la kubeba mbao zako maana namba ya gari itaitajika kwenye kuandika kibali.
 
Aseee Kuna mlolongo mkubwa sana
 
Mtoa mada tafuta uzi wangu wa @naitaji vijana wa kuwasadia kuwekeza kwenye biashara ya mbao au njoo dm

Kwa maelezo ya kina sharti unitumie bukutano mana napoteza muda wangu kukuelekeza

Nitakuelekeza kuanzia kuanzia products mpaka sokoni
 

Attachments

  • IMG_20250203_093135_795.jpg
    559.6 KB · Views: 1
HABARI WANA JAMII FORUM
N
aomba maelekezo juu ya biashara ya mbao
1,upatikanaji
2,usafirishaji
3,jinsi ya UENDESHAJI wa biashara
4, mtaji wa chini kiasi gani
5,namna ya kutafuta soko


M nakufundisha jinsi ya kupiga wateja na nilichowashtukia wauzaji WA buguruni

Ukiona unapokelewa pale unaingizwa OFISIN mkuu noma wakati WA kutoka ukisikia TUNAANZIA chini
Chini n nn
Ile mtr inakatwa vipande inaunganishwa

Ukisoma mwisho tu UJUE umeumia narudia umeumia

1-15
Ipo1-7
Inakatwa
Inafungwa na 11nk
HAPO Wana mtr tatu kila mmbaoo

Biashara Moja nzuri ila ukijifunxa na kuibianwatu kama hivi
 
Mzee hii code nilelekeze vizuri umeiweka ki ndava Zaidi
 
Mzee hii code nilelekeze vizuri umeiweka ki ndava Zaidi
IKo hivi mkuu

Ile MITA yako si inasoma futi/mitaa
Moja mpaka mwisho

Unaponunua unalipankutokana na kile ulichopima


Wanachofanya wanakata vipande eg
MITA 1-20
Ikifika kwenye 8
Wanakata wanaunga na kuanzia 11

Kwahiyo kwenye 1-11
We unalipanmita 11
Uhalisia 9/10 hazipooooo

N NGUMU kushtuka mpaka uwe umepigwa ama ushtuliwe kama hivi

Soln nenda na Mita yako uikae siku ukakubali kupima urefu WA mbao kwa MITA zao n kilio
 
Aseee 🤣 🤣 🙌 atari sana kaka kumbe unaweza kufuta machozi sema kila biashara ukiingia kiboya unapigwa
 
K
Kwa mfano ndio naingia njombe kichukua mzigo uko napo upigaji upo
 
Kuna broo aliuza mzigo akiwa Njombe usiku unaingia kawekewa pistol kichwani anaambiwa toa pesa Leo umeuza mzigo asee broo karudi home hajui afanye nini
 
Vipi makadirio ya gharama na masoko ya kulenga
 
Kuna broo aliuza mzigo akiwa Njombe usiku unaingia kawekewa pistol kichwani anaambiwa toa pesa Leo umeuza mzigo asee broo karudi home hajui afanye nini
Yaaan n biashara nzuri na mbaya sana huwa wanauxana
 
Kuna mikoa ya Njombe, Iringa Mbeya huko nina experience nako. Faida wanapata sana, wanaonunua mti moja kwa moja kwa mkulima na kuprocess mbao kwa saizi tofauti tofauti na kusafirisha mbao mpaka yalipo masoko kama Zambia, Makambako n.k.

Faida
-Mkulima hajui uhalisia wa faida utakayoipata, kwa hio utanunua kwa bei ya chini mti wa mbao
-Uwepo wa nguvu-kazi ya kukufanyia kazi kama mafundi, wasogeza mbao na wasogeza magogo na wanalipwa ujira wa kawaida wenye faida kwako

Hasara zinazoweza kujitokeza
-Moto wa nyika ambao huweza kuunguza mbao au magogo
-Sura ya nchi isiyo rafiki mahali ilipo miti kama miteremko mikali
-Tabia ya nchi ya baridi kali hasa usiku.
-Miundombinu isiyo rafiki hasa wakati wa masika, Kuna maeneo hayaingiliki kabisa si chini ya miezi 7 masika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…