Naomba design za nyumba jamani!

Naomba design za nyumba jamani!

Wazo zuri, kupata ushauri wa wana jamii wenzako. Ila tu mimi si designer ila uzeofu wangu katika hili (nimejenga nyumba tatu) tengeneza wazo lako mwenyewe unachotaka ndipo umtafute mtu mwingine aongezee utaaluma, utapata kitu kizuri kwa moyo wako. Kumbuka ukifanyiwa kitu ambacho kina utata kidogo utaishi na hiyo nyumba mapaka uihame au ufe, hivyo hakikisha moyo wako umeridhika.
wanasema designer mzuri wa jiko ni mpishi na sio mtengenezaji.
 
Kuna ramani moja mzuri sana standard ya kisasa nainafaa kwa sie wenye hali ya kawaida..nitaiscan niipost..ila hata kama ukipata nyingine hakikisha unapata building permission(nafikiri manispaa au wizarani) waikague na waridhike nayo..hii itasaidia watakupa ushauri zaidi.ni hayo tu
 
Mbeba Maonooo...
Nimefuatilia Kwa Kina Mawazo Yalotolewa Na Wajumbe Wa Jf...solution Ni Kumuona Architect....nadhani Mimi Ndio Huyo "architect" Unaweza Kuwasiliana Nami Kama Ungependa Kupata Ushauri Zaidi Wa Kitaalamu.
Kwa Upande Wa Malipo Ya Consultancy Service Nadhani Sio Makubwa Sana Lakini Kwa Mtu Anayetaka Kujenga Ni Bora Akayajua.
Malipo Yanaweza Kuwa % Ya Building Cost Ambayo Yana-range From 7-12% Au Yanaweza Kuwa Lumpsum Amount Ambayo Consultant Anai-derive From The Time Atakayotumia Kufanya Kazi Yako Plus Other Reimbursable Costs. Kwa Ufupi Unaweza Ukanitafuta Kwa Kupata Contacts Zangu Private.
 
  1. Mahitaji ya mtu humpa wazo la kujenga nyumba
  2. Fikira juu ya uwezo hufuatia
  3. Uunganishaji wa mahitaji na uwezo hufanyika
  4. Mtu anashuriwa kuhusu wazo lake
Kimsingi sioni tatizo la mtu kuangalia/kujifunza aina tofauti za ujenzi kabla ya kumwona mtaalam wa usanifu. Unaweza kuangalia nyumba za watu wengine pamoja na kutafuta kwenye mtandao wa intaneti.

Kosa kubwa mtu utakalofanya ni kufikiri kwama unaweza kupata mchoro wa nyumba kwenye mtandao. Pata wazo la jumla tu kwa kuangalia nyumba nyingine katika mazingira yako ama kuangalia kwenye mitandao!

Mkuu FM, kutafuta mawazo ya dream house yako ni sawa, ila isiwe mchoro wa nyumba yenyewe..... Mahitaji ya nyumba ni specific, then ushauri wa kuongea na mtaalam wa usanifu unasaidia kuweka wazo la anayetaka kujenga katika misingi ya taaluma husika.
 
Nimefuatilia mjadala huu na nadhani ushauri uliotolewa na wanaforum ni wa kuzingatia. La muhimu ni kwamba kama unataka kujenga usiogope kutumia wataalamu kwa kisingizio cha gharama kwa sababu kutokutumia wataalamu wa fani husika ni gharama zaidi kuliko kuwatumia.

Mara nyingi usanifu wa nyumba hasa za kawaida ni makubaliano tu ambayo hata si lazima iwe percentage ya gharama halisi ya nyumba kwa kuwa mara nyingi ni vigumu kumtoza mtu wa kawaida "real professional fee". Hivyo, kama una laki 250,000 - 300,000, mtafute Architech yeyote, zungumza naye na atakuchorea plan inayoendana na vigezo unavyohitaji, lakini pia kulingana na mazingira ya kiwaja unapotaka kujenga.
 
nashukuru walau unataka kujikomboa, umegundu pesa unazolipa unamnufaisha mtu, ramani ukitaka naweza kukutengenea na zipo ambazo ninazo lakini ni vigumu kuziweka hapa maana ni nyingi labda useme unataka nyumba ya aina gani,,, nadhani umenipata,,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom