Naomba Elimu namna utekelezaji wa bajeti za serikali ulivyo na jinsi Rais anavyoshukuriwa sana na wabunge

Naomba Elimu namna utekelezaji wa bajeti za serikali ulivyo na jinsi Rais anavyoshukuriwa sana na wabunge

mweki

Member
Joined
Nov 8, 2014
Posts
6
Reaction score
16
Wakuu nawasalimu, niende moja kwa moja kwenye swali , linahusu budge ya serikali na utekelezaji wake , bunge na Mheshiwa Rais

nianze na maelezo kidogo, Nijuavyo mimi, budget zote hupitishwa na bunge, na wabunge huwa wakali sana kwa mawaziri kama watekelezaji wa maamuzi ya bunge , mambo ya kushika shilingi n k hutokea hapo.

So Kwanini wabunge hao hao humshukurugi sana Rais kwa kuwajengea hili na kufanya yale, na wakati mwingine wanamshukuru sanaa kwa pesa zilizopitiswa na bunge?

Pili kwanini Rais hukopa bila bunge au kuomba misaada na ikija inaenda moja kwa moja kwenye miradi anayoamua yeye? badala ya kusaidia budge ya serikali? ili pia kupunguza upendeleo na kujijengea umungu mtu? Au katiba ina mruhusu kutafuta pesa huko na kuzipeleka moja kwa moja kwenye miradi?

Mfano unakuta kuna sehemu hazina shule, na mbunge ameomba sana Bungeni na budget haitoshi au pesa zimepigwa , kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa serikali n.k Lakini Rais akipata pesa anajiamulia yeye azipeleke wapi, pesa alizopata kwa jina la Mama Tanzania ,na kaombea kwa jina la mwenye anataka shule pia , ye anapeleka atakako.

utasikia namshukuru sana n.k
hii ipoje, why bunge huwa halimwadhibu Rais kugawa zake za miradi kama Bunge. n.k
 
Back
Top Bottom